Friday, April 29, 2016

TAARIFA YA MKAGUZI WA TAWI LA CHUO KIKUU CHA IRINGA.

UTANGULIZI.
taarifa ya ofisi ya mkaguzi wa tawi la Chuo kikuu cha IRINGA.
Wapendwa katika bwana. Napenda kutoa shukrani Kwa Bwana wetu yesu kwani ndie kiongozi na mkaguzi wa matendo yetu yoto hapa duniani na wakili wetu siku ya ukumu kule Juu.
1. Glory madiwa(mkaguzi komfrenci) Kwa kunifundisha kazi na kunivumilia katika maswali yangu yoto. Kwakweli alijitoa kunisaidia na Mungu atakubariki. Nitumie pia fursa hii kuwashukuru mwanatawi letu Kwa ushirkiano wenu ndani ya mwaka huu wa 2015-2016 Kwa umoja na mshikamano wenu.
Katika safari hii yakwenda Kwa bwana tukumbuke kwamba njia yetu ni nyembamba hivyo kama tulikosana tusameane kwani hayo ndiyo miba, mawe, yanayopatikana ndani ya njia hiyo.

UTENDAJI WA KAZI NDANI YA MWAKA 2015-2016.
- tumefanikiwa kufanya kazi Kwa pamoja na vyongozi japo walikua baathi tu.
- ofisi ya mkaguzi (CAG wakanisa) tumefanikiwa kukagua taarifa zote za fedha za tawi Bila kupoteza hata shilingi ya tawi nakufanya tawi letu kupewa Hati Safi kwani kila robo taarifa ya mkaguzi ilikua ikibaini changamoto na siyo matumizi mabaya ya pesa. Kitu iliyofanya kila robo mkaguzi kutuma Hati Safi Kwa kiongozi Wa Kanda.
- ofisi ya mkaguzi ilifanya kazi masaa 24 na kupelekea kila kiongozi kuwajibika japo wengine walifanya mambo Yao Kwa kuificha ofisi ya CAG.
CHANGAMOTO.
1. vyongozi kutumia madaraka Vibaya toka mwenyekiti, katibu, mtunza azina. Mfano. Kutoa pesa njee ya tawi Bila kuwasiliana na ofisi ya CAG.
2. Kutokutoa taarifa za utendaji Kwa kila idara kama mawasiliano, na kuperekea vyombo au vifaa kupotea, kuaribia na tawi kufanya matumizi yasiyo yalazima kama kununua na kutengeneza vifaa vya tawi.
3. Vyongozi kutokufahamu mipaka ya madaraka Yao na kufanya wengine kuwa vyongozi hewa bila kufanya kazi. Mfano m/kiti kupata taarifa na kutuma moja Kwa moja Kwa wanachama bila kujali kazi ya kiongozi Wa mawasiliano na kufanya huvujifu wa mishingi ya uongozi yani (Lider ship ethics).
MWISHO.
Baba Mungu wabariki vyongozi wapia.
By. Baraka Boniphace.
CAG wa tawi letu. 

Tuesday, April 26, 2016

Kimenuka bungeni - Nondo zilizomo kwenye report ya CAG::

::Kimenuka bungeni - Nondo zilizomo kwenye report ya CAG::

=> Ulaji na uzembe vinatajwa kubeba sehemu kubwa ya ripoti hii.

=> Misamaha ya kodi 2014/15 ni asilimia 2 ya pato la taifa kinyume cha asilimia 1

=> Halmashauri 40 hivi ndo zenye hati safi kati ya halmashauri zaidi ya 1

=> Bidhaa a bilioni 9 za kupelekwa nje ziliuzwa hapa hapa nchini. Upigaji huo wa ukwepaji kodi.

=> Bidhaa za bilioni 89 za nje hakuna ushahidi kama zilienda Rwanda, Burundi na Uganda.

=> Rufaa za kodi nyingi mno zimedoda mahakamani na hivyo kuikosesha serikali kodi

=> Deni la Taifa hadi Juni 2015 lilifikia trilioni 33.5. Ndani ya mwaka mmoja lilikua kwa trilioni 7!

=> Malipo kwa deni kwa mwaka ni trilioni 4.

=> Deni na mishahara inamaliza mapato yote ya taifa. CAG anahoji, tutapata wapi pesa za maendeleo?

=> CAG Anataka maduka ya fedha za kigeni yadhibitiwe

=> Vyama vya siasa, kimoja tu kimewasilisha hesabu. Vyama 21 bado, Msajili afiatilie. Hajakitaja chama kilichowasilisha

=> Mishahara hewa katika Taasisi za umma 16 ni Shilingi bilioni 390. Mishahara ambayo haikulipwa na haikurejeshwa hazina ni bilioni 2

=> Sh. Milioni 700 za makato ya watumishi kwa Katavi na Kilimanjaro hayakuwasilishwa kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

=> Sh. Milioni 827 za vifaa vya upigaji kura zilitumika kwa kazi isiyo na tija katika Uchaguzi 2015

=> Nakala 158,003 za Katiba Pendekezwa hazikusambazwa kwa walengwa wakati wa mchakato wa Katiba Mpya

=> Manunuzi yenye thamani ya Sh. Bilioni 27 yalifanywa na Mashirika ya Umma bila ushindani

=> Cheti cha uendeshaji ATC kimeisha muda tangu 2010. ATC ina Wafanyakazi wengi kuliko kazi zilizopo

=> CAG ataka UDA irejeshwe serikalini. Mwenyekiti wa Bodi ya UDA, Idd Simba aliwekewa sh. milioni 320 ktk akaunti yake binafsi.

=> Kampuni ya SAAFI inadaiwa Sh. bilioni 17. Hii ni ya mwanasiasa mkongwe, Mzindakaya.
MPEKUZI

Tanzania Entertainment News,Politics News ,Celebrity Gossip and Live Updates

HomeEnglish NewsDisclaimerAdvertise Here

Tuesday, April 26, 2016

Ripoti ya CAG Yaanika 'Madudu' Kibao Serikalini

Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti mpya ya ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo. 

Ripoti hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa Juma Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano. 

 

Ripoti hiyo ya pili ya Professa Assad tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo mwaka juzi, imegusa taasisi zilizowahi kuwa chini ya Rais John Magufuli na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi Asha Rose Migiro, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba. 

 

Ripoti hiyo pia inaonyesha ufisadi katika ununuzi na uingiaji mikataba uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), matumizi yasiyo ya lazima kwenye Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jeshi la Wananchi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na mkoa wa Tabora. 

 

Pia ripoti hiyo imebainisha kuwa mapendekezo mengi ambayo CAG amekuwa akiyatoa kwa takribani miaka saba sasa, hayatekelezwi. 

 

Katika ripoti hiyo, CAG anaonyesha dosari kwenye utendaji wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (Temesa), na Wakala wa Barabara (Tanroads), taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ambayo wakati huo ilikuwa ikioongozwa na Dk Magufuli. 

 

Profesa Ndalichako alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), wakati NEC imeguswa na ripoti hiyo katika suala la mchakato wa kuandika Katiba upya ulioongozwa na Wizara ya Katiba na Sheria. 

 

Ripoti hiyo ya Profesa Assad pia imebainisha kuwa Deni la Taifa, ambalo hutokana na fedha zinazopowa kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kugharimia matumizi ya Serikali, limekuwa kwa tofauti ya Sh7 trilioni. 

 

Tangu aingie madarakani Novemba 5 mwaka jana, Dk Magufuli amekuwa akitumia ripoti zilizopita za CAG kusimamisha kazi au kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi, lakini amekuwa akikosolewa kuwa hajaweka mfumo wa kukabiliana na hali hiyo. 

 

Katika ripoti hiyo, CAG anasema Temesa ilinunua kivuko chenye kasi ndogo kuliko ilivyotarajiwa na hadi ulipokuwa unafanyika ukaguzi Agosti 2015, chombo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya mwaka. 

 

“Kuhusu dosari katika ununuzi wa kivuko chenye thamani ya Sh7,916,955,000, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Umeme, mitambo na ufundi (Temesa) iliingia mkatabana M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade 10, DK 2100 Copenhagen Oe Denmark wa ununuzi wa kivuko cha Dar es Salaam –Bagamoyo chenye thamani ya Dola za Marekani 4,980,000 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),” anasema CAG. 

 

“Dosari zifuatazo zilibainika katika manunuzi hayo. Kasi ya kivuko haikuzingatia matakwa ya mnunuzi.  Ripoti ya mtaalamu wa ukaguzi ilibainisha kwamba kiwango cha juu na chini cha kasi ya kivuko wakati wa majaribio kilikuwa na kiwango kati ya knots 19.45 na knots 17.25 kinyume na makubaliano yaliyoainishwa kwenye mkataba wa kasi ya kiwango cha 20,” anafafanua.

 

“Pili kivuko kilikabidhiwa bila hati ya makabidhiano Novemba 17, 2014 baada ya ucheleweshwaji wa siku 16; Pia nilibaini kwamba mpaka wakati wa ukaguzi, Agosti 2015, hati ya makabidhiano ilikuwa haijatolewa na mzabuni.” 

Ununuzi wa feri hiyo uliwahi kuzua sakata bungeni huku wabunge wa upinzani wakilalamika kwamba kilikuwa bomu kwani kinatumia zaidi ya saa tatu kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo badala ya dakika 45 za gari. 

 

Eneo jingine lililoguswa na CAG ni la malipo yaliyofanywa na Tanroads kwa makandarasi waliomaliza kazi zao. Kwamba moja ya matatizo makubwa ya taasisi hiyo ni udhaifu katika menejimenti. 

 

“Wakala wa Barabara (Tanroads) iliingia mikataba mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja. 

 

"Wakati wa ukaguzi nilibaini kwamba baadhi ya mikataba haikukamilika kwa muda uliopangwa kutokana na kuchelewa kwa ulipaji wa fedha. 

  

"Pia, nilibaini kwamba ucheleweshwajiwa malipo ya kati ya mikataba 16 ulisababisha ulipaji wa riba kiasi cha Sh 5,616,652,022 na Dola za Marekani 686,174.86,” alisisitiza CAG. 

 

Profesa Assad amezungumzia pia ukaguzi maalumu alioufanya kuhakiki fedha zilizowahi kutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa taasisi mbalimbali zilizoko chini yake. 

 

Ukaguzi huo ulifanywa kutokana na ombi lililowasilishwa na katibu wa Bunge kwa barua yenye Kumb. NaCBC.155/188/01/26 ya Desemba 19, 2013. 

Bunge lilitaka kujua kama fedha zilizotolewa na wizara hiyo kwenda idara na taasisi zilizo chini yake zilipokewa na kutumiwa na wahusika kama ilivyopangwa. 

 

Katika ukaguzi huo, CAG alibaini kasoro katika vitabu vya akaunti za fedha vya Necta mwaka 2010, Sekretarieti ya Elimu ya Jumuiya ya Madola, Chuo Kikuu Huria (OUT), na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem). 

 

“Udanganyifu wa malipo ya Sh185,350,000 yaliyolipwa Necta. Aprili 2010 kiasi cha 185,350,000 kilitumwa Necta kama matumizi ya kawaida. Wakati wa ukaguzi ilibainika kuwa kiasi hiki cha fedha hakikuandikwa kwenye vitabu vya uhasibu vya Necta. Hata hivyo, ilibainika kuwa stakabadhi ya mapokezi ya fedha hizo iliyotolewa na watumishi wasio waaminifu wa Necta ilikuwa ya kugushi,” anasema. 

 

“Kuhusu fedha zilizopelekwa OUT ni kwamba kati ya mwaka 2009/2010 Wizara ilihamisha Sh90,000,000 kwenda Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ni kiasi cha Sh40,734,000 ambacho kilipokewa huku Sh49,266,000 hakijulikani. 

 

“Pia katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara ilipeleka OUT Sh10,486,252,913 lakini ni Sh10,427,109,020 tu zinazoonekana kwenye vitabu huku Sh59,143,893 zikiwa hazimo kwenye vitabu.” 

Vilevile, CAG amesema katika ukaguzi huo Sh188, 838,528 zilizopelekwa Adem mwaka 2009/2010 zimeyeyuka. Mwaka huo Wizara ilipeleka Sh712,798,788 kwa taasisi hiyo, lakini vitabu vinaonyesha Sh523,960,260 zilipokewa na kurekodiwa, huku Sh188, 838,528 zikikosekana kwenye vitabu. 

 

Mbali ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya fedha, pia ameonyesha matumizi mabaya ya Sh7,080 milioni katika mchakato wa uchapaji Katiba Inayopendekezwa. 

 

“Katika ukaguzi wangu nilibaini kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilipokea fedha kiasi cha Sh7,125 milioni kwa ajili ya kulipia gharama za kuchapisha vitabu vya Katiba Inayopendekezwa. 

"Kutokana na ufinyu wa muda, Wizara iliomba na kupewa kibali na Wakala wa Huduma za Manunuzi Serikalini kufanya manunuzi kwa njia ya dharura kupitia barua yenye kumbukumbu Na CAD.124/318/01/25 ya Desemba 11, 2014,” anasema CAG. 

 

“Katika ukaguzi wangu nilibaini vitabu vya katiba vilipokelewa kabla ya kuingia mkataba. Nilibaini kuwa mkataba ulisainiwa Februari 2, 2015, lakini vitabu vya katiba vilipokelewa Januari 26, 2015.” 

Ukaguzi uliofanywa Oktoba Mosi, 2015 umebaini kuwa nakala 158,003 za Katiba Inayopendekezwa zenye thamani ya Sh559,330,620 bado viko stoo au havijatumwa kwa wananchi ili vitumike kwa uhamasishaji. 

 

“Kwa hiyo, haikuwa rahisi kujua kama thamani halisi ya fedha ilipatikana na lini vitabu hivi vitasambazwa kwa walengwa. Pia, ilibainika kuwa vitabu hivyo havikujumuishwa kwenye Taarifa za Fedha za Mwaka husika,” anasema. 

 

Katika ripoti hiyo ya mwaka 2015/16, CAG Assad anasema ukaguzi wake umebaini matumizi ya mabilioni ya fedha katika ununuzi wa vitu visivyokuwa vya lazima au bila kuonyesha ushahidi wa malipo husika. 

 

Alibainisha matumizi ya zaidi ya Sh53 bilioni zilizotumiwa na taasisi sita pamoja na Sekretarieti mbili za mikoa katika mambo ambayo hayakuwa ya lazima, kama faini za kuchelewa kulipa kodi ya pango. 

 

Taasisi hizo ni Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na Mkoa wa Tabora. 

 

CAG Assad amebainisha matumizi ya ziada ya Sh109,722, 539 kwa ajili ya ununuzi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 kwa Sh297.5 milioni kutoka kampuni ya Toyota (T) badala ya kutumia mfumo wa ununuzi wa pamoja ambao ungefanya gari hilo lipatikane kwa Sh187.8 milioni. 

 

Alisema katika kipindi hicho, wizara 17, balozi mbili na sekretarieti za mikoa 11 zilitumia zaidi ya Sh11.3 bilioni bila kuwapo vielelezo vyovyote, hivyo kusababisha ashindwe kujua uhalali wa malipo hayo. 

==> Kwa taarifa zaidi, pitia  ripoti hizi za CAG

 

1. Ripoti ya Jumla ya Serikali Kuu 2014/2015

2.Ripoti ya Jumla ya ufanisi na Uchunguzi 2014/2015

3. Ripoti ya Jumla ya Mashirika ya Umma 2014/2015

4. Ripoti ya Jumla ya Miradi ya Maendeleo 2014/2015

5. Ripoti ya Jumla ya Serikali za Mitaa 2014/2015

 

==

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Mpekuzi Blogkwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

› Halmashauri 47 tu zilizopata Hati zinazoridhisha

1.Arusha DC 2.Makambako TC 3.Butiama DC 4.Kahama TC 5.Arusha CC 6.Wanging’ombe DC 7.Kyela DC 8.Ushetu DC 9.Monduli DC 10.Buhigwe DC 11.Busokelo Dc 12.Msalala DC 13.Bagamoyo DC 14.Kakonko DC 15.Kilombero DC 16.Bariadi TC 17.Kibaha DC 18.Uvinza Dc 19.Kilosa DC 20.Itilima DC 21.Kibaha TC 22.Moshi MC 23.Morogoro MC 24.Busega DC 25.Temeke MC 26.Siha DC 27.Gairo DC 28.Singida MC 29.Dar es Salaam CC 30.Lindi MC 31.Ilemela MC 32.Ikungi DC 33.Kinondoni MC 34.Mbulu DC 35.Nyang’hwale DC 36.Mkalama DC 37.Chemba DC 38.Simanjiro DC 39.Mbogwe DC 40.Bumbuli DC 41.Mufindi DC 42.Kiteto DC 43.Mlele DC 44.Kaliua DC 45.Iringa DC 46.Tarime TC 47.Nsimbo DC

Halmashauri 105 zilizopata Hati zenye Mashaka

1.Meru DC 2.Kongwa DC 3.Bukoba MC 4.Kilwa DC 5.Ngorongoro DC 6.Mpwapwa DC 7.Muleba DC 8.Lindi DC 9.Kisarawe DC 10.Dodoma MC 11.Karagwe DC 12.Liwale DC 13.Mafia DC 14.Iringa MC 15.Kyerwa DC 16.Nachingwea DC 17.Mkuranga DC 18.Kilolo DC 19.Kibondo DC 20.Ruangwa DC 21.Rufiji/Utete DC 22.Ludewa DC 23.Kigoma DC 24.Babati DC 25.Ilala MC 26.Njombe DC 27.Moshi DC 28.Hanang’ DC 29.Chamwino DC 30.Njombe TC 31.Mwanga DC 32.Babati TC 33.Kondoa DC 34.Makete DC 35.Rombo DC 36.Serengeti DC 37.Bahi DC 38.Biharamulo DC 39.Same DC 40.Musoma DC 41.Rorya DC 42.Ngara DC 43.Magu DC 44.Bunda DC 45.Tarime DC 46.Missenyi DC 47.Misungwi DC 48.Musoma MC 49.Mbeya DC 50.Ulanga DC 51.Ukerewe DC 52.Mpanda TC 53.Rungwe DC 54.Morogoro DC 55.Geita TC 56.Mpanda DC 57.Chunya DC 58.Mvomero DC 59.Geita DC 60.Tunduru DC 61.Mbeya CC 62.Masasi TC 63.Bukombe DC 64.Songea DC 65.Mbozi DC 66.Masasi DC 67.Chato DC 68.Nyasa DC 69.Ileje DC 70.Mtwara DC 71.Sumbawanga DC 72.Shinyanga DC 73.Mbarali DC 74.Newala DC 75.Nkasi DC 76.Shinyanga MC 77.Momba Dc 78.Tandahimba DC 79.Sumbawanga MC 80.Kishapu DC 81.Meatu DC 82.Nanyumbu DC 83.Korogwe DC 84.Maswa DC 85.Bariadi DC 86.Mtwara MC 87.Korogwe TC 88.Nzega DC 89.Manyoni DC 90.Mkinga DC 91.Kilindi DC 92.Sikonge DC 93.Singida DC 94.Lushoto DC 95.Igunga DC 96.Tabora DC 97.Pangani DC 98.Muheza DC 99.Urambo DC 100.Tabora MC 101.Tanga CC 102.Handeni DC 103.Karatu DC 104.Hai DC 105.Kigoma/Ujiji MC

Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu

1. Karatu DC 2. Hai DC 3. Kigoma/Ujiji MC

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya

Tunduma Town Council

· Hawa walificha vitabu 79 vya mapato

· Walificha hati za malipo(voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580

· Malipo ya SHS.17,158,500 hayakuwa na viambatanisho

· Hawakuandaa vitabu vya hesabu

Home

View web version