Monday, May 10, 2021

VIDONDA VYA TUMBO -AINA, CHANZO, DALILI & TIBA.

UTANGULIZI – UJUE UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo. Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito. AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers) Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa 2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu) duodenal-ulcer CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni; Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori) Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine) Kuwa na mawazo mengi Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi Kunywa pombe na vinywaji vikali Uvutaji wa sigara Kuto kula mlo kwa mpangilio DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama; gastrita Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito Kushindwa kupumua vizuri JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO Kunywa maji mengi Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol) Usivute sigara Punguza au acha kunywa pombe Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9 TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa. DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO Tuna dawa ya kutibu Vidonda vya tumbo ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu, ukianza kutumia baada ya wiki moja mgonjwa huanza kupona na huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa. Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya. MAWASILIANO roryamaendeleo@gmail.com 0768441610