Tuesday, July 12, 2016

RAIS MAGUFULI APUUZWA MCHANA KWEUPE,NA DC NA MKUREGENZI WAKE,SOMA HAPO KUJUA




 John Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MARRY Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mwanza na Housian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la hilo wamekiuka agizo la Rais John Magufuli la kufanyika kwa sherehe za kupongezana pindi mtumishi wa umma anapoteuliwa kushika nyadhifa, anaandika Moses Mseti.

Machi mwaka huu, Rais Magufuli akiwaapisha wakuu wa mikoa jijini Dar e Salaam, aliwataka kutosherehekea kuteuliwa kwao na kwamba, wafanye hivyo siku wakitimuliwa.

Rais Magufuli pia aliwaagiza wakuu hao wa mikoa kuwekeza nguvu zao katika kuondoa tatizo sugu la madawati kwenye shule za umma, agizo ambalo muda wake ulikamilika Juni 30 mwaka huu huku Mkoa wa Mwanza ukikwama kufikia malengo hayo.

Sherehe za kumkaribisha mkuu huyo wa Wilaya ya Nyamagana na kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Baraka Konisaga maarufu mtumishi wa Mungu, ziliandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza chini ya kaimu mkurugenzi huyo.

Sherehe hizo zilizofanyika katika Hoteli ya New Mwanza ambapo zaidi ya watu 100 wakiwemo watumishi wa Jiji la Mwanza wakihudhuria ambapo kiasi cha zaidi ya Sh. 30 milioni zikitajwa kutumika.

Sherehe hizo zilizoanza saa 12 jioni hadi saa 4 usiku, waandishi wa  vyombo mbalimbali vya habari  walitimliwa na kutakiwa kutoripoti habari hii.

Awali, waandishi walialikwa na baadhi ya viongozi hao wakiwemo wakuu wa wilaya kwa ajili ya kuripoti lakini baadaye ikaibuliwa hoja ya kwamba, inaweza kusababisha tatizo hasa kutokana na kutokamilika kwa fedha za ununuzi wa madawati.
Hosian Kusiga, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo alipotafutwa kuzungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika kuandaa sherehe hiyo hazikutoka katika mfuko wa serikali na kwamba, walichangishana baadhi ya watumishi wa jiji na taasisi mbalimbali.
“Wewe kama ulivyoona mwenye katika sherehe hiyo yalikuwepo makundi mbalimbali, ikiwemo Mwauwasa (Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira) mkoani Mwanza na sio fedha kutoka Jiji,” amesema Kusiga ambaye pia ni Ofisa Mipango wa Jiji.
Tesha, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana akizungumzia suala hilo amesema kuwa, fedha zilizotumika katika sherehe hiyo sio fedha za serikali.
“Pesa zilizotumika sio za serikali, unaniuliza fedha zilizochangwa eti kwanini hazijapelekwa kwenye madawati, mimi ningewakataza wasifanye sherehe, hivi wewe vipii… mbona sikuelewi,” amesema.

HOT NEWS,DOKTA MWAKA AFUNGIWA RASMI,SOMA HAPO KUJUA

HOT NEWS,DOKTA MWAKA AFUNGIWA RASMI,SOMA HAPO KUJUA




Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

PIGO TENA--HOTELI KUBWA ZAANZA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI WAKE,BAJETI YA JPM YATAJWA,TRA WASEMA HAKUNA JINSI,SOMA HAPO KUJUA

PIGO TENA--HOTELI KUBWA ZAANZA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI WAKE,BAJETI YA JPM YATAJWA,TRA WASEMA HAKUNA JINSI,SOMA HAPO KUJUA



Pichani ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,John Magufuli.


MACHANGU ya Bajeti ya  mwaka 2016/2017  yameaza kujionesha kwa kasi baada Hoteli kubwa  nchini ambazo zilikuwa zinatumika kuwapokea watalii kuanza kupunguza wafanyakazi katika hoteli hizo kwa kile wanachodai ukata wa fedha umezikumba Hoteli.(Mtandao huu umelezwa).Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.

Taarifa za kuamika ambazo Fullhabari.blog imezipata kutoka kwenye Hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam ambayo nayo imewaandikia baadhi ya wafanyakazi wake ikiwataka warudi nyumbani kwa kile wanachodai Hoteli hiyo inajiendesha kihasara.
 
Taarifa hiyo inasema kinachotwajwa kupelekea mpaka hoteli hiyo kuwa katika hali hiyo inatokana na hutua ya serikali kukataza mikutano yote ya serikali kufanyika kwenye Hoteli hizo huku ikitoa maelekezo kuwa mikutano yote ifanyike kwenye kumbi za serikali jambo ambalo linolotajwa kuliangamiza hoteli hizo  kwa kuwa  mikutano hiyo ni chanzo cha mapato.

YALIO JIRI IKULU LEO RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ONGEA NA WAKURUGENZI WATEULE WA HALMASHAURI, MIJI, MANISPAA NA MAJIJI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JULAY 12,201


1

8Rais Dkt. John pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wateule wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji Ikulu jijini Dar es salaam Julay 12,2016 
11

5Baadhi ya Wakurugenzi wateule wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam Julay 12,2016
9Mkurugenzi wa halmashauri ya Itigi Luhende Pius Gerald akionyesha vyeti vyake vya masomo kwa wandishi wa habari, Luhende alichafuliwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa elimu yake ni cheti cha usimamizi wa Hoteli, amewaonesha wandishi wa habari kuwahakikishia kuwa Elimu ya Uzamili
13

14Picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji 185

Monday, July 11, 2016

Ni nini maana ya kuwa mwili mmoja katika ndoa?

Ni nini maana ya kuwa mwili mmoja katika ndoa?



Swali: "Ni nini maana ya kuwa mwili mmoja katika ndoa?"

Jibu: 
neno "mwili mmoja" linatokana na Mwanzo akaunti ya uumbaji wa Hawa. Mwanzo 2:21-24 inaelezea mchakato wa jinsi Mungu alimuumba Hawa kutoka ubavu uliochukuliwa kutoka upande wa Adamu akiwa amelala. Adamu alitambua kuwa Hawa ni sehemu yake hakika-walikuwa "mwili mmoja." Neno "mwili mmoja" lina maana kwamba kama miili yetu ni chombo kimoja kizima na haiwezi kugawanywa katika vipande na bado iwe mwili mmoja, hivyo ndivyo Mungu alinuia uhusiano wa ndoa uwe. Wao tena sio vitu viwili (watu wawili), lakini sasa kuna chombo kimoja (wanandoa). Kuna idadi ya mambo ya muungano huu mpya.

Mbali na kuingiza hisia, kitengo mpya kinachukua usukani juu ya uhusiano uliopita na ujao (Mwanzo 2:24). Baadhi ya washirika wa ndoa huendelea kuweka uzito mkubwa juu ya mahusiano na wazazi kuliko na mpenzi wao mpya. Hii ni kichocheo kwa ajili ya maafa katika ndoa na ni upotoshaji wa nia ya Mungu ya awali ya "kuachana na kuambatana." Tatizo sawia linaweza kutokea wakati mwanandoa huanza kumkaribia mtoto ili kukidhi mahitaji ya hisia badala ya mpenzi wake.

Kihisia, kiroho, kiakili, kifedha, na katika kila njia nyingine, wanandoa wanapaswa kuwa kitu moja. Hata kama vile sehemu moja ya mwili inajali sehemu zinginezya mwili (tumbo husiaga chakula kwa ajili ya mwili, ubongo unaongoza mwili kwa ajili ya mema ya yote, mikono hufanya kazi kwa ajili ya mwili, nk), hivyo kila mshirika katika ndoa ni mhudumu kwa wengine. Kila mwanaharusi hapaswi kuona fedha kuwa "zake pekee"; bali badala yake kama "zao". Waefeso 5:22-33 na Mithali 31:10-31 inatoa matumizi ya neno "umoja" na jukumu la mume na mke, sawia.

Kimwili, wanakuwa mwili mmoja, na matokeo ya mwili huo mmoja unapatikana katika watoto na muungano wao huzaa; watoto wenye miliki ya maumbile maalum, sawia na muungano wao. Hata katika nyanja ya ngono ya uhusiano wao, mume na mke hawafai kuchukulia miili yao kama yao wenyewe, bali kama mali ya mpenzi wao (1 Wakorintho 7:3-5). Wala wao kuzingatia radhi yao wenyewe, bali kutoa furaha hiyo kwa wenzi wao.

Umoja huu na hamu ya kufaidishana kila mmoja si ya moja kwa moja, hasa baada ya mwanadamu kuanguka katika dhambi. Mume katika Mwanzo 2:24, anambiwa "aambatane" na mke wake. Neno hili lina mawazo mawili ndani yake. Moja ni kuwa "kushikanishwa" na mke wake, picha ya jinsi ambavyo ndoa inapaswa kuwa dhabiti. Sababu nyingine ni "kukaza mbele kwa sababu ya" mke. Hii "kutafuta mke kwa bidii" ni kwenda zaidi ya uchumba na kusababisha ndoa, na inafaa kuendelea katika ndoa. Tabia ya mwili ni "kufanya kile unahisi ni kizuri kwangu" badala ya kufikiria ni nini kitafaidisha mke. Na huu ubinafsi ndio chanzo cha ndoa kuvunjika mara moja pindi tu "fungate imeisha." Badala ya kila mwanandoa kushinda kulalama jinsi mahitaji yake mwenyewe hayafikiwi, yeye anapaswa kundelea kulenga katika kukidhi mahitaji ya mwenziwe.

Inaweza kuwa vizuri kwa watu wawili kuishi pamoja kukidhi mahitaji ya kila mmoja, Mungu ana wito zaidi kwa ndoa. Vile walikuwa wanamtumikia Kristo na maisha yao kabla ya ndoa (Warumi 12:1-2), sasa wao wanapaswa kumtumikia Kristo pamoja kama kitengo kimoja na kulea watoto wao kumtumikia Mungu (1 Wakorintho 7:29-34, Malaki 2: 15; Waefeso 6:4). Priska na Akila, katika Matendo 18, watakuwa mfano mzuri wa hili. Wanandoa wanapotafuta kumtumikia Kristo pamoja, furaha ambayo Roho huleta itajaza ndoa yao (Wagalatia 5:22-23). Katika Bustani ya Edeni, kulikuwa na watu watatu (Adamu, Hawa, na Mungu), na kulikuwa na furaha. Hivyo, kama Mungu ni mkuu katika ndoa hiileo, kuna pia kutakuwa na furaha. Bila Mungu, kama hakuna umoja wa kweli na kamili kamwe haiwezekani.

Hivi kwa nini unaogopa kuoa au kuolewa?Unajua nini maana ya Ndoa?Biblia inasemaje?

UTANGULIZI

Ndoa ilianzishwa (instituted) na Mungu. Mungu aliumba mke kwa ajili ya Adamu kwa kuwa Mungu aliona "Haikuwa vema" kwa Adamu kuwa peke yake.

Mungu alimuumba mke (Eva) kuwa msaidizi (suitable helper) wa Adamu kutawala dunia, kulea familia na kumuabudu Mungu.
(Mwanzo 2:18, 42)
Ndoa ni mke mmoja na mume mmoja (monogamous). 
Mungu alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu na si Eva na Jane, Ingawa Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba wanawake wengi kadri anavyoweza ila alimuumba Eva peke yake kwa ajili ya Adamu. Agano la kale kulikuwa na polygamist na matokeo yake hakukuwa na amani.
(Mwanzo 2:22)

Ndoa ni mke na mume. Biblia haizungumzii kuumbwa kwa Adamu na James au Eva na Linda na kufanya ndoa bali Adamu na Eva.
(Mwanzo 2:22, 1:28)

Ndoa inahusisha Mume kuondoka kwa wazazi ili kuanza familia yake kama mke na mume na pia kuna kuwa na taarifa kwa jamii (public recognition) kwamba fulani na fulani ni mke na mume hata kama formalities au tamaduni hutofautiana.

Ndoa inawafunga mke na mume hadi kifo.
Marko 10:9 
1Wakorintho 7:39 
Warumi 7:2-3
Ndoa inahusisha wajibu wa kila mmoja katika mahusiano kwa mke kutii (submissive) na Mume kumpenda mke wa kujitoa sadaka (sacrificial love)
Efeso 5:22-24, 25-28)

Ndoa huhusisha mume kuwa kichwa cha nyumba au mke kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa
Efeso 5:23
1Wakorintho 11:3

Ndoa ni suala zito ni uamuzi wa pili kwa uzito duniani (kwanza ni wokovu na pili ni ndoa) hivyo si kuingia tu kwa kadri unavyijisikia kwani barabara unayoingia ni dead end hakuna kutoka hadi kifo.

Dunia imejaa udanganyifu wa kila aina kuhusiana na suala la ndoa jambo la msingi ni kujua kweli na kweli itakuweka huru.

Unapoingia kwenye ndoa unahitaji kuwa makini, mbele ya safari kujitetea eti nilikuwa bado nina akili ya kitoto, au nilidhani atabadilika au sikuwa na akili timamu au sikujua kama itakuwa hivi haitakusaidia kwani ukiingia ni hadi kifo kitakapowatenganisha hivyo kama hujaoa au kuolewa please be extra carefull siyo unabeba bora liende then kesho unasema "I made a terrible mistake" naweza kuachana naye! hakuna kitu kama hicho.

MWANAMKE WAKO AMEKUWEKA KUNDI GANI?

MWANAMKE WAKO AMEKUWEKA KUNDI GANI?


KATIKA mapenzi kuna mambo mengine yanaumiza lakini ni vizuri kujifunza. Ukijua inakuwa rahisi kukaa nayo mbali. 
Kuna kitu nataka kukupa rafiki yangu mpendwa. 
Je, unajua kuwa baadhi ya wanawake huwaweka wanaume katika makundi? Ndugu zangu baadhi ya wanawake wasio waaminifu wenye wanaume zaidi ya mmoja huwaweka wanaume kwenye makundi matatu.
Unaweza kuwa na msichana mkapendana sana, kwa sababu ya upofu wa mapenzi usijue amekuweka kundi lipi. Ni vizuri kuyafahamu makundi hayo kisha kujichunguza ili ujue kundi ulilopo.
MAKUNDI
Makundi hayo ni starehe, kutoshelezwa kimapenzi  na fedha. Lazima uwe makini sana ili uweze kujua tabia za makundi hayo.
Inahitajika utulivu na umakini wa hali ya juu maana wakati mwingine, mwanamke anaweza kuonyesha dalili ya wazi ya kundi fulani lakini kutokana na kupumbazwa na mapenzi ukaamini kwamba umefika kwenye kiota cha raha za wapendanao.

KUNDI A
Unaweza kuwa kwenye kundi la starehe. Mwanamke akawa na wewe kwa lengo la kuwa na uhakika wa kupata starehe kila wiki. Hebu angalia tabia za mpenzi wako, yukoje?
Haina maana kwamba mwanamke akipenda starehe ni tatizo, lakini ukiona mazungumzo yake yanaonekana kujali zaidi starehe kuliko mambo mengine muhimu, ujue hapo upo kwenye mikono isiyo salama.
Mwanamke mwenye upendo wa dhati hawezi kuendekeza starehe, sana sana atakusubiri umshinikize mtoke.

KUNDI B
Wapo wanawake ambao wapo na wanaume kwa ajili ya kujipajia fedha. Fikra zao zote ni kupata fedha na siyo kitu kingine chochote. Atafanya kila kitu, atatafuta kila sababu lakini lengo lake ni kukuchuma.
Wanawake hawa wapo wa aina mbili, wengine huchuna fedha na kwenda kula raha na wanaume wengine huku wengine wakiwa ni wachumi kwa manufaa yao wenyewe.
Wachumi mara nyingi huwa na wanaume wengi wakiwa na lengo la kujipatia fedha. Ni kama wanajiuza lakini hawapo sokoni rasmi. Mwanamke wako yukoje? 

KUNDI C
Kundi la mwisho ni lile la wanawake wanataka wanaume wa kuwatumia kimapenzi tu. Huyu hata usipompa fedha, shida yake kubwa huwa ni faragha.
Mara nyingi mwanamke wa aina hii anaweza kuwa mkubwa kiumri kuliko mwanaume lakini wakati mwingine anaweza kuwa na umri wa kati, sawa au chini ya mwanaume lakini haonyeshi nia ya malengo ya ndoa siku zijazo.
Huyu ni rahisi kumgundua hata katika mawasiliano tu. Anaweza kukuambia waziwazi anakutaka faragha, tena mara kwa mara. Hazungumzii maendeleo, hataki kujua habari zako, anachotaka ni mapenzi tu.


Asilimia kubwa ya wanawake wa namna hii ni wale ambao wana wenzi wengine wenye malengo nao lakini hawawatimizi haja zao za kimapenzi. Ni vizuri kuwa makini, kuchunguza na kupata uhakika kisha kuchukua hatua.

LOVE SMS MPYAAAA............

LOVE SMS MPYAAAA

CHAGUA MOJA KISHA MTUMIE MPENZI WAKO

Mpenzi wangu wa moyo, kumbuka kuwa upo masomoni kwa ajili ya kusaka elimu, uzuri wako utawachanganya wengi kama mimi nichanganyikiwavyo, lakini dear kumbuka kuna mtu anayekupenda, usinisaliti dear! Nakupenda...
*****
Last night I matched each star with a reason for loving you. I was doing great until I ran out of stars!
****
Wengi wananiuliza kwanini nimekupenda na jibu langu kwao ni kwamba nimekupenda kwa sababu nakupenda! Tusiwape nafasi wanafiki kuingilia letu penzi! Nakuhitaji dear...
***
God is wise when he did not put a price tag on you darling. If he did, I won’t be able to afford to have a boyfriend as precious as you. I luv you!
*****
Ni usiku sasa lahazizi wangu, naliwaza joto lako tamu, nafikiria penzi lako la dhati, lala salama dear ukijua kuna mtu anayekuwaza na kutesekea penzi lako. Nakupenda muhibu wangu...
*****

My heart for you will never break. My smile for you will never fade. My love for you will never end. I love you!
*****
Nalala nikikuwaza, chukua mto wako mpenzi, nami nichukue wangu, kumbatia nami nikumbatie, tulale pamoja mawazo yetu yakiamini tupo pamoja. Nakupenda sana mpenzi wangu!

JINSI YA KUOMBA MSAMAHA KWA MPENZI WAKO......

OMBA MSAMAHA KWA MPENZI WAKO:
Mpenzi wangu naomba unisamehe, nakupenda sana dear na ni kweli kuna wakati nakukosea, lakini amini nakupenda. Sijawahi kujuta na sitajuta kamwe kuwa na wewe! Naamini nitaendelea kuwa mwaminifu kwako, sio leo tu, bali siku zote za penzi letu!
*****
Tukae kimya sheteni apite, naamini haikuwa akili yangu bali ni ushawishi wa sheteni ambaye siku zote amekazania kuharibu penzi letu!
*****

Wewe kwangu ni kila kitu, sipendi kuyaona machozi yako mpenzi wangu! Sogea nikufute na unirudishe tena mikononi mwako, nakupenda sana dear!
*****
Wewe ni taa kwangu imulikayo gizani, nakupenda sana mpenzi wangu wa moyo, utakuwa wangu siku dear! Kosa nililofanya ni kwa bahati mbaya, naomba unisamehe na ninaahidi kutorudia tena katika penzi letu!
*****
Tega sikio dear, nakupenda sana, ukweli wa ile sms uliyoifuma kwenye simu yangu, haikuwa yangu bali mtumaji alikosea kwa bahati mbaya! Nipo tayari tumpigie tukiwa pamoja tumuulize, kweli niamini dear! Naomba usiniache maana maisha yangu bila wewe ni sawa na giza nene!
****
Mimi kwako ni kipofu, nishike mkono tuvuke barabara, magari ni mengi na yanapita kwa kasi, siwezi kuona zaidi ya kusikia yakiunguruma, honi za magari siwezi kupima umbali wake, usiniache katikati ya barabara nitagongwa na kufa mara moja! Njoo niokoe nitagongwa mpenzi wangu! Forgive me dear...

Nyingine ya mwaka!! kuhusu waliokua wakifanya mapenzi chumba jirani na cha Mahakama kesi ikiendelea


Screen Shot 2014-05-22 at 11.26.43 AMKatika vituko vikubwa au vioja Mahakamani nilivyowahi kuvisikia kutoka Tanzania, vyote nilivipata kutoka 88.1 Mwanza pale ambapo Mahabusu mmoja alitumia njia ya kuvua nguo na kujipaka choo ili akitoroka mtu aogope kumshika lakini hakufanikiwa… pia kituko kingine ni cha May 2014 ambacho Mahabusu mmoja alivua nguo na kupaza sauti kwamba amesingiziwa kesi ya mauaji na anashikiliwa kwa kipindi kirefu.
Kituko kingine cha tatu leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea.
Jaji Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze baada ya kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo wawili hao walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani.
Taarifa kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya wawili hao anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa  na hii ni kwamujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama.
Screen Shot 2014-05-22 at 11.27.10 AMBaada ya hii ishu ilibidi tu Jaji aamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka wakati mwingine muda mfupi tu baada ya wakili Sabrina Monteverde kuanza kuzungumzia kesi ya hiyo ya Mmorocco Yasin Mahmoud ambae anashtakiwa kuua jambazi katika bandari nchini Italy mwaka jana.
Mmoja kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wakili ndio kwanza alianza kuzungumza, jaji akasikia kelele za mahaba na alipoangalia juu na kuona miili miwili ikiwa uchi ilifanya kila mtu akatazama ambapo tuliona watu wawili wakifanya mapenzi na inaonesha walikua hawajui kama wanaonekana na wakati tunawatazama bado walikua wanaendeleza.
Kesi ilisimamishwa na wawili hao waliondoshwa eneo hilo na kupata mshtuko ambapo majina yao hayajatajwa huku mzungumzaji wa Genoa Court  akisema kesi imesimamishwa kwa muda na tukio hilo limeshashughulikiwa na haitakuwa sawa kuzungumzia zaidi
.

ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA

ATHARI ZA KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA


SeeBait

Wapenzi wengi hasa wale ambao uhusiano wao ni mchanga hupenda sana kufanya mapenzi kila wanapokutana au wanapohisi wamehemkwa na miili yako.

 Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono. 

Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu. 

 Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kila siku anatumia ‘chakula cha usiku’ kwa sababu tu hakuna wa kumkataza na kwamba ana haki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari. 

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.

 Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana hata kwenye nguzo ya umeme na chini ya miti kwa vile tu miili imetaka kufurahika. 

 KUPOTEZA HAMU YA TENDO
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

 Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.

 Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi  kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

 KUUJAZA MWILI TAMAA KUBWA
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani

 Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake. 

Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi. 

Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi. 

 KUPOTEZA RAHA KAMILI YA TENDO
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.

 Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!

 KUPOTEZA NGUVU ZA MWILI
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili. 

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. 

Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

 Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

 KUPATA MAGONJWA
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

Ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.

 Baada ya kungalia madhara hayo machache ni vema kwa wapenzi kupunguza kiwango cha kufanya mapenzi ili kuifanya miili iwe na uvumilivu unaoweza kumsaidia mtu kukaa kwa muda mrefu bila kumsaliti mpenzi wake hata kama atakuwa amesafiri mbali naye kimasomo, kikazi au kibiashara.

HASARA ZA KUTOFANYA MAPENZI KWA MUDA MREFU

WOMEN-STRESS-facebook

by rorya maendeleo

Ukidumu bila tendo la ndoa muda mrefu, baadhi ya madhara madogo madogo yanaweza kujitokeza kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa kiafya  karibu twende sawa katika  darasa la leo Mwalimu ndio nshakuandalia vitu vitamu jisomee ili ufaulu somo Mapenzi.

Zifautazo ni athari hasi za kutofanya tendo la ndoa kwa muda mrefu;

1.Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo Mara kwa mara huwa anakasirishwa na vitu vidogo hata visivyokuwa na maana yeye huvitilia maanani .

2.Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mwanamke), Tafiti zinaonesha kuwa mwanamke anapokuwa kwenye mzunguko wake wa siku 28 kama hatoshiriki tendo la ndoa kwa kipindi kirefu basi hupoteza damu nyingi wakati wa hedhi.

3.Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu) hii pia ni tabia inayoibuka kisaikolojia kutokana na kile watoto wa mtaani wanachoita mizuka inampanda kwa yasiyo muhusu.

4.Kuumwa na kichwa, Wataalamu wametaja maumivu ya kichwa mara kwa mara wakati mwingine husababishwa na kutofanya mapenzi kwa muda mrefu.

5.Kukakamaa mgongo (wanaume), Inasemekana kuwa mwanaume akikaa bila kufanya mapenzi kwa muda mrefu husumbuliwa na maumivu ya mgongo ya mara kwa mara.

6.Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba, Hii imeelezwa ni kutokana na ndoto zile utakazoota kifikra kwamba unafanya tendo la ndoa ndio hupelekea kumkaribisha jini mahaba katika mwili wako.

7.Kupoteza umakini katika kazi, Wataalamu wa mambo wanasema kwamba pindi unapokaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa unapoteza uwezo wa kufanya kazi kwa umakini unaotakiwa.

8.Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno, Inasemekana utakuwa umekamia mechi hivyo utauanza mchezo bila maandalizi yanayotakiwa hivyo msuguano utakuwa mkali na kuleta madhara.

Ethiopia yazima Facebook kwa sababu ya mtihani

Ethiopia yazima Facebook kwa sababu ya mtihani


Image copyrightEPA
Image captionEthiopia imezima mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii nchini Ethiopia imezimwa kwa sababu ya mtihani wa taifa. Waethiopia waliamka Wikiendi wakajipata hawana huduma hizo za mitandao kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber.
Serikali imefunga mitandao hiyo tangu Jumamosi usiku.
Msemaji wa serikali ameiambia shirika la habari la AFP kuwa serikali ilichukua hatua hiyo kama njia ya kuzuia wanafunzi wasivurugwe na ushawishiwa mitandao hiyo ya kijamii.
Hatua hiyo vilevile imetokea majuma kadhaa baada ya baadhi ya makaratasi ya mitihani kuchapishwa kwenye mitandao ya kijamii na kulazimu serikali kufutilia mbali mitihani hiyo iliyodukuliwa.
''Serikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano.
Tumegundua kuwa mitandao ya kijamii huvuruga kabisa ratiba ya vijana na haswa wanafunzi'', alisema msemaji wa serikali Getachew Reda .
Image copyrightTHINKSTOCK
Image captionSerikali imechukua hatua hiyo kwa muda hadi siku ya Jumatano mitihani itakapokuwa imekamilika
Hatu hiyo bila shaka imewaudhi wanaharakati wa kupigania uhuru wa habari nchini Ethiopia.
Mwanabloggu mashuhuri Daniel Berhane amechapisha kwenye mtandao wake wa Twitter maswali ambayo anataka yajibiwe.
Je ni nani aliyechukua uamuzi huu?
Aliwashauri kina nani ?
kwanini alichukua hatua hiyo?
Je hii haitakuwa mwanzo wa tatizo jipya la kukandamiza uhuru wa kujieleza ?

Marufuku wanawake waislamu kufunika uso Rwanda

Marufuku wanawake waislamu kufunika uso Rwanda


Image copyrightPA
Image captionWanawake waislamu wazuiliwa kufunika nyuso Rwanda
Wanawake waislamu nchini Rwanda,wapigwa marufuku wasijifunike nyuso zao.
Hatua hiii imechukuliwa na jumuiya ya waislamu nchini humo iliyofikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab linalovaliwa na wanawake.
Vazi hilo hufunika uso wote wa mwanamke.
Jumuiya hiyo imesema marufuku hiyo inatokana na sababu za kiusalama kwa waislamu na vilevile warwanda.
Image copyrightGETTY
Image captionHapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi la Islamic State
'' Hili vazi ni la kiislamu hata hivyo limeanza kutumika vibaya kwa madhumuni ya kudhuru usalama wa waisilamu na vitendo vinavyokinzana na mafunzi ya dini ya Kiislamu''
''Jambo la pili ni usalama wa nchi. kwa sababu watu wanajificha na kutenda vitendo pasi na kutaka kuonekana''.
''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa Sindayigaya.
Uamuzi huo umetokea wakati kundi la watu 17 wa kiislam wanazuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kutaka kujiunga na kundi la IS na kufundisha itikadi za kundi hilo.
Katika msikiti mkuu wa Nyamirambo jijini Kigali ni wakati wa swala ya adhuhuri,,,waislam wengi wanaingia msikitini …lakini huwezi kuona hata mmoja anayevaa niqab miongoni mwa wanawake au mabinti wanaoingia hapa msikitini
Image copyrightGETTY
Image caption''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa Sindayigaya.
Wanawoiunga mkono kauli hiyo ya jumuiya ya waislam nchini Rwanda wanasema kuwa Niqab ilikuwa imeanza kutumika kuficha maoavu mengi katika jamii.
Aidha wanasema kuwa wanawake waislamu wanapaswa kuwajibika kwa kujiepusha na maovu ambayo sasa yameanza kuchipuka kwa kisingizio cha Niqab.
Kuna wengine walioghadhabishwa na uamuzi huo lakini hawakutaka kuzungumzia suala hilo wakisema wanahofia usalama wao.
Hapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi la Islamic State na pia kueneza itikadi za kundi hilo.

Uganda yatuma wanajeshi mpaka wa Sudan Kusini

Uganda yatuma wanajeshi mpaka wa Sudan Kusini


Image copyrightREUTERS
Image captionNdege zatumika katika mapigano Sudan Kusini
Uganda imetangaza kwamba itatuma wanajeshi wake katika mpaka wake na Sudan Kusini baada ya mapigano kuzuka upya nchini humo.
Msemaji wa jeshi la Uganda Paddy Ankunda amesema wanajeshi hao watatumwa kuzuia mapigano kuenea hadi maeneo ya Uganda.
Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa mataifa, linawaomba viongozi wakuu wa serikali ya Sudan Kusini, kuyadhibiti majeshi yao.
UN inasema kuwa mashambulio dhidi ya raia na makao makuu pamoja na kambi ya Jeshi ya Umoja wa mataifa, ni uhalifu wa kivita.
Walinda amani wawili wa umoja wa mataifa kutoka Uchina, wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa.
Umoja wa mataifa unasema kwamba, mataifa jirani na Uchina yanafaa kujiandaa kutuma majeshi zaidi nchini humo, ikiwa hali ya usalama itaendelea kudorora .
Image copyrightREUTERS
Image captionWanajeshi wakishika doria mabarabarani katika mji mkuu wa Juba
Hata hivyo baraza hilo litahitaji kuidhinisha vikosi zaidi.
Kwa sasa wanajeshi wa umoja wa mataifa walioko Juba ni elfu 13 pekee.
Umoja wa mataifa unasema kuwa, walinda amani wanafaa kutumia kila mbinu kuwalinda raia.
Waandishi wa habari wameiambia BBC kuwa ndege za helikopta zimetumika kurusha risasi pande zote huku zikishambulia majengo ya maskani ya bwana Machar.
Image copyrightAFP
Image captionWanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir na wale watiifu kwa Riek Machar wamekuwa wakipigana tangu Alhamisi
Milio mikubwa ya risasi ilisikika katika makao makuu ya kambi ya kijeshi ya umoja wa mataifa.
Vifaru vya kivita vinaonekana katika barabara za mji mkuu Juba, huku wakaazi wakijifungia ndani ya majumba yao.
Mamia ya watu wameuwawa tangu ghasia hizo zianze upya siku tano zilizopita.
Mapigano yaliyoripotiwa kutokea katika uwanja wa ndege mjini Juba, yamesitishwa, huku mashirika mbalimbali ya usafiri wa ndege kuingia na kutoka mjini Juba, likiwemo shirika la ndege nchini Kenya -KQ yamesitisha usafiri.