Tuesday, September 12, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI MKUU FROF. IBRAHIM HAMIS JUMA, 

 Rais Dk John Magufuli akimuapishaJaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Profesa Ibrahim anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande na kuwa jaji wa nane kushika wadhifa huo tangu nchi ipate uhuru huku akiwa Mtanzania wa sita. Wapili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi

 Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma akisaini hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akitia saini hati ya kiapo cha Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma baada ya kumuapisha 

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi hati ya kiapo Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma 

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Mhe. Profesa Ibrahimu Hamisi Juma leo 

Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma akizungumza baada ya kuapishwa leo 

 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Juma kuapishwa

 Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) akiteta jambo na  Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande (kulia) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju wakati wa hafla hiyo ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu wa Tanzania 

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya majaji waliohudhuria hafla ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania 

 Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi akifuatilia kwa makini hafla hiyo

 Jaji Kiongozi Ferdinand Wambaliakiteta jambo na  Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande (kulia) wakati wa hafla hiyo

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla hiyo.  

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Hamisi Jum. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumz na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wakati wa hafla hiyo

 Rais Dk. John Magufuli akiwa na Jaji Mkuu na Spika wa Bunge wakati wa hafla hiyo


Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai na Majaji mbalimbali, mwisho mwa hafla hiyo,leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment