Wednesday, July 22, 2015

Maneno ya MSEKWA kwa KINGUNGE, LEMBELI na sababu za kumtoa CCM, BVR Dar ni leo..#MAGAZETINI JULY22


Maneno ya MSEKWA kwa KINGUNGE, LEMBELI na sababu za kumtoa CCM, BVR Dar ni leo..#MAGAZETINI JULY22

News Microphone Computer Online Podcast
MWANANCHI
Baada ya vuta vikuvute ya muda mrefu, hatimaye leo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano maalumu utakaofanyika jijini Mwanza.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa chama hicho Kanda ya Ziwa Magharibi na makao makuu zilisema kuwa leo mgombea huyo atatangazwa mkoani hapa huku zikibainisha kuwa anayepewa nafasi kubwa ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa.
Taarifa hizo zimekuja wakati kukiwa na tetesi kuwa chama hicho kilikuwa kinafanya mazungumzo na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyekuwa anawania urais kupitia CCM na kutemwa katika hatua za awali, huku vyanzo mbalimbali vikisema mazungumzo hayo yanachukua muda mrefu na kuna uwezekano mkubwa wa kutozaa matunda.
Jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe pamoja na baadhi ya wabunge walikaririwa wakitoa matamko ya kumkaribisha Lowassa kuingia Chadema lakini kwa sharti la kufuata kanuni na taratibu za chama hicho, lakini Dk Slaa alisita kumzungumzia kiongozi huyo akiahidi kuzungumza mambo yatakapokuwa sawa.
Mratibu wa Operesheni za Chadema Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu alisema mgombea huyo (bila kumtaja jina), atatangazwa katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Ilemela kuanzia saa nane mchana.
Njugu alisema katika mkutano huo, viongozi wakuu wa Ukawa wanatarajia kuwapo na maandalizi yake yamekamilika.
“Kesho (leo) tutakuwa na mkutano mkubwa kwenye viwanja vya Magomeni,” alisema Njugu na kuongeza: “Mgombea urais kupitia Ukawa atajulikana hapo, kwani tunatarajia viongozi wakuu wa Ukawa watamtangaza.”
Katika mazingira tofauti, akihutubia mkutano wa hadhara mjini Geita juzi, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alidokeza jina la Dk Slaa kama mgombea urais wa chama hicho, kitendo kilichoibua hamasa na umati kumshangilia, lakini akawapoza akisema ulimi umeteleza.
Alipoulizwa kuhusu mkutano huo, Mwenyekiti wa NLD, Dk Emmanuel Makaidi alikiri kuwa leo kulikuwa na mpango wa kumtangaza mgombea wa Ukawa, lakini alidhani ingekuwa Dar es Salaam, hivyo kwa kuwa wameamua iwe Mwanza angefanya utaratibu wa ndege ili aweze kuwahi.
Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia hakupatikana kuzungumzia mkutano huo, lakini Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe alisema hakuwa na taarifa hizo, hasa kwa kuwa vikao vya mwisho vilivyofanyika Jumapili na Jumatatu vilihusisha wenyeviti wa vyama pekee.
Hata hivyo, alisema ilibidi mgombea huyo atangazwe ama jana au leo. Chama cha CUF kimekwishatangaza kuwa kinasubiri uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi litakaloketi Julai 25 kuamua juu ya hatima yake ndani ya Ukawa.
Alipotakiwa kudokeza ni nani atasimama kuwakilisha Ukawa, Njugu alisema jukumu hilo ni la viongozi wa juu na kwamba yeye akiwa kiongozi wa Kanda anatambua mgombea urais wa Ukawa atatangaziwa Mwanza leo.
MWANANCHI
Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amemrushia kombora kada mkongwe wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru kuwa, hazijui vyema kanuni zinazoongoza mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho tawala.
Huku akinukuu Kanuni za Usalama na Maadili, toleo la mwaka 2012, Msekwa alisema ilitumika ili kupambana na siasa zinazoendeshwa kwa nguvu ya fedha na kuwachuja wagombea ili kupata walio waadilifu.
Kauli ya Msekwa ni mwendelezo wa madai ya Kingunge aliyeitupia lawama CCM kuwa haikutenda haki katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM.
Katika mchakato huo, Dk John Magufuli alichaguliwa kuwa mgombea urais akiwashinda Asha-Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali.
Kingunge aliyejitoa kindakindaki kumpigania Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo na zaidi akisema haukutenda haki.
Amekuwa akikaririwa akisema wagombea wote 38 waliojitokeza walitakiwa kuhojiwa na Kamati Kuu, kisha wachujwe na kubaki watano na kupinga kitendo cha Kamati ya Usalama na Maadili kufanya kazi ya kuwachuja wagombea.
Msekwa ni mmoja wa viongozi wa zamani waliotoa mapendekezo yaliyokuwa msingi wa CCM kupata mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu
Msekwa alinukuu vifungu vinavyoeleza majukumu ya Kamati ya Usalama na Maadili na chama hicho, kusisitiza kuwa wanaolalamikia mchakato huo, ama hawajazipitia kanuni hizo au hawazijui.
“Mzee Ngombale amezua madai kwamba eti mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ulikuwa ni batili, kwa sababu eti ulikiuka kanuni za chama. Madai hayo yamepotosha kabisa ukweli wa jambo hilo. Kwani ukweli wenyewe ni kwamba kanuni za CCM zinazohusika zilifuatwa kwa ukamilifu. Kanuni hizo zilizotumika zinaitwa Kanuni za Usalama na Maadili, toleo la mwaka 2012. Pengine tatizo la mzee huyo ni kwamba hajazipata vizuri.”
Alisema: “Kwa mujibu wa Kanuni namba 3(3)(vii); Kamati ya Usalama na Maadili itachambua kwa makini ubora wa wanachama wanaoomba uongozi, kabla vikao vinavyohusika havijatoa idhini ya kuwaruhusu wateuliwe kugombea uongozi wanaouomba.”
“Kanuni hii ndiyo inaipatia uwezo Kamati ya Usalama na Maadili kufanya uchambuzi wa maadili ya wagombea wote kabla majina yao hayajapelekwa kwenye vikao ninavyofuata vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa.”
Alisema utaratibu uliowekwa na kanuni hiyo ulifuatwa kwa ukamilifu, kusisitiza kuwa haukuwa batili kama inavyodaiwa.
Akizungumzia lengo la kutoa kipaumbele cha kwanza kwa suala la maadili ya viongozi alisema: “Ni vyema ieleweke kwamba kanuni hii ilikusudiwa kupambana na ukosefu wa maadili ya viongozi ambao ni wanachama wa CCM na hususan kupambana na tatizo kubwa la ujio wa money-driven politics (siasa zinazoendeshwa kwa nguvu ya fedha).”
Alisema tatizo la siasa zinazoendeshwa kwa fedha lilijitokeza kwa nguvu wakati wa mchakato wa kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka huu.
MTANZANIA
Vituko vimeanza katika kampeni za kuwania kuteuliwa na CCM kugombea nafasi za Ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.
Moja ya vituko hivyo ni kile kilichotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini anayemaliza muda wake Dk.David Mallole ambaye jana wakati akijinadi kwa wanachamawa chama hicho, aliwaomba wamteuwe kwa mara nyingine kwa sababu amesoma darasa moja na mgombea Urais John Magufuli.
Wakati hayo yakijiri Dodoma, Jimbo la Kinondoni msanii Steve Nyerere aliomba achaguliwe kwani ana uwezo wa kupita katika ofisi za mabalozi wa nje waliopo jijini Dar es salaam kuomba misaada.
Kampeni hizo zilianza jana wakati Dar wakati wagombea wakijinadi mbele ya wajumbe kabla ya kupiga kura ya maoni Agosti mosi mwaka huu.
“Wilaya ya Kinondoni ndio inayoongoza kwa kuwa na ofisi nyingi za mabalozi, mkinichagua nitahakikisha nakwenda wenye Ubalozi wa Marekani kuomba misaada kwa ajili ya kuwawezesha vijana…Nitakwenda Ubalozi wa China kuomba atusaidie kuondoa mafuriko yanayolijumba jimbo hili “Steve Nyerere.
Katibu wa CCM,Kinindoni alisema katika Wilaya yake kuna wagombea 60 ambao kati yao wanawake wanne wanawania majimbo ya Kinondoni,Kawe, Ubungo na Kibamba.
NIPASHE
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Dodoma, Mariam Mfaki, alifariki dunia jana katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mtoto wa marehemu, Mohamed Mfaki, alisema mama yake alifariki majira ya saa sita mchana.
Alisema mama yake mpaka kufikwa na mauti hayo alikuwa anasumbuliwa na saratani ya utumbo.
“Alianza kuugua tangu mwaka 2012 vidonda vya tumbo, baadaye utumbo ulipata tatizo lililosababisha saratani ya mapafu na utumbo, baada ya kuendelea na matibabu hayo akapata pia ugonjwa wa moyo,” alisema.
Mohamed alisema marehemu alianza kutibiwa katika Hospitali ya Apollo nchini India mwaka 2012 mpaka mwaka 2014 huku akiwa anaendelea na shughuli zake ikiwamo kuhudhuria vikao vya Bunge.
“Marehemu alizidiwa usiku wa Julai 19 mwaka huu na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu, ilipofika jana majira ya saa tano asubuhi hali ilibadilika hatimaye saa sita mchana akaaga dunia,” alisema.
Alisema taratibu za mazishi zinaendelea na kwamba wao kama familia wamepanga mazishi yafanyike leo saa 10 jioni shambani kwake maeneo ya Miyuji, Manispaa ya Dodoma.
Alipoulizwa kama ofisi ya Bunge ina taarifa za msiba huo, alisema taarifa wanazo na tayari baadhi ya maofisa walifika nyumbani kwa marehemu Area E.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ezekiel Mpuya, alithibitisha kutokea kifo hicho na kwamba kilitokea majira ya saa tano asubuhi.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashillilah, alipotafutwa kwa njia ya simu kuelezea kifo hicho cha Mbunge, simu yake haikupokelewa.
Marehemu alikuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 hadi Bunge lilipovunjwa Julai 9, mwaka huu.
Kabla ya kuwa mbunge, alikuwa Afisa Tarafa kwa zaidi ya miaka 20 katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Dodoma. Ameacha mume, watoto sita na wajukuu 10.
NIPASHE
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), leo inatarajia kuanza uandikishaji wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa Teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) katika Jiji la  Dar es Salaam, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu idadi ya mashine zitakazotumika kwa kila kituo.
Hadi jana majira ya mchana, baadhi ya ofisi za kata za Manispaa za Temeke, Ilala za jiji hilo zilikuwa bado hazijapelekewa mashine hizo, isipokuwa Ubungo, katika Manispaa ya Kinondoni ilikuwa na  takriban BVR 14.
Manispaa  ilieleza kuwa  kila kituo kitakuwa na BVR moja, tofauti na maelezo ya awali yaliyotolewa na Nec, kwamba kila kimoja kingekuwa na mashine  mbili.
Katika Ofisi za Manispaa ya Kinondoni, pilikapilika za watu, wakiwamo maofisa watendaji wa Kata, waliofika katika ofisi hizo kufuata mashine hizo.
Ofisa Uchaguzi wa Manispaa hiyo, Valence Urassa, alisema mashine 706 zilikuwa zimepokelewa katika ofisi hizo hadi majira ya jioni.
Kwa mujibu wa Valence, manispaa hiyo ina vituo vya kuandikishia wananchi 706 na kila kituo kimoja kitakuwa na BVR moja.
Ofisa Mwandikishaji Msaidizi wa Manispaa ya Temeke, Waziri Kombo, alisema BVR zote 572 zilikuwa zimepokelewa kwa ajili ya kusambazwa leo asubuhi kwenye vituo 572  na kwamba kila kituo kitakabidhiwa mashine moja.
Ofisa Uchaguzi wa Manispaa ya Ilala,  Baina Hilary, alisema mashine zilizopelekwa katika ofisi yao  zilikuwa 396 ambazo ni sawa na idadi ya vituo vya kuandikishia wananchi katika daftari hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Nec, Julius Malaba, alisema mashine zilizoagizwa kwa ajili ya uandikishaji nchi nzima zipo 8, 000 na zinazotarajiwa kutumiwa kwa Dar es Salaam ni zaidi ya 3,000.
“Hakuna utakakokwenda utakuta BVR mbili… hiyo ni minimum. Eneo linaweza kuwa na vituo zaidi na idadi ya BVR inaweza kuwa vinne, 13 kulingana na eneo.  Siyo kwamba foleni hazitakuwapo lakini tumejiandaa na tutaendelea kuongeza BVR katika eneo lenye tatizo,” alisisitiza.
NIPASHE
Mchakato wa uteuzi wa wagombea ubunge kupitia viti maalum katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) unadaiwa kutawaliwa na hongo.
Habari kutoka vyanzo vyetu mbalimbali ndani ya CCM na Jumuiya zake zinaeleza kuwa kuna baadhi ya vigogo wakiwamo wabunge wanaoshikilia nafasi hizo ambao wanamwaga kiasi kikubwa cha fedha kuwahonga wajumbe wa vikao mbalimbali kuanzia kata, wilaya na mikoa watakaopiga kura.
Mbali na kumwaga kiasi kikubwa cha fedha kwa wajumbe, pia wanadaiwa kuwahonga watendaji ambao wanawatumia kuwaandalia mikutano isiyo rasmi kwa ajili ya kukutana na wapigakura.
Malalamiko mengi ya kumwagwa hongo kwa ajili ya kupata viti maalum yanauhusu Mkoa wa Dar es Salaam ambao vigogo kadhaa wamejitosa kwa ajili ya kusaka nafasi hizo.
Vigogo watatu wanaowania nafasi hizo ndio wanaolalamikiwa zaidi kwa kufuru ya hongo.
Chanzo kimoja kimeeleza kuwa kuna kigogo mmoja mwenye ukwasi mkubwa ambaye anakata dau kubwa kuwashawishi wapigakura na kwamba kwa sasa anatoa hadi Sh. 200,000 kwa kila mjumbe.
Yaani nakwambia sasa hivi napiga raundi ya tatu mkoani. Kuna wajumbe kama 300 hivi, kila mmoja mara ya kwanza aliwapoa Sh. 150,000, lakini juzi hapa baada ya Bunge kuvunjwa ameibuka na anatembeza Sh. 200,000,
Mwanachama huyo aliyeomba kutokutajwa jina lake kwa sababu za kiusalama, alisema kuwa kwa mwelekeo wa sasa ndani ya CCM ni miujiza kama mtu hana fedha za hongo, kuchaguliwa.
Yaani ukifika kwenye ofisa za kata kama hujatoa fedha, hakuna anayekusikiliza. Akija aliyetoa fedha utashangaa anavyoshangiliwa. Jamani CCM imefika hapa kweli,” alilalamika.
JAMBOLEO
Mbunge wa Kasulu Mjini ,Moses Machali amekihama rasmi chama hicho na kujiunga na ACT – Wazalendo huku akiwaeleza wananchi waliofika kumsikiliza katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kiganamo mjini hapa kuwa hatasita kuachana na chama chake kipya endapo kitaonekana kinatetea mafisadi na viongozi wanaokandamiza demokrasia.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi na kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu huyo wa NCCR – Mageuzi alisema amejiunga baada ya viongozi wa chama hicho kumhujumu katika harakati zake za kutetea masilahi ya Halmashauri ya Wilaya Kasulu.
“Nilijiunga na NCCR-Mageuzi nikitokea Chadema mwaka 2010 na wananchi mkanichagua kuwa mbunge wa Kasulu Mjini ili tushirikiane kupigania haki na maendeleo ya Kasulu, lakini kwa muda mrefu nimekuwa nazushiwa maneno kwamba mimi ni mkorofi na ndiyo maana sielewani na wataalamu pale halmashauri, lakini vita yangu ilichochewa na kuchukia kwangu rushwa na ufisadi, mambo ambayo kuna wenzetu kule NCCR wanashiriki kuyafanya,” alisema.
Alisema: “Nilifukuzwa bungeni pamoja na wabunge wengine watano wa upinzani kwa vile tulikuwa tunapinga kitendo cha Serikali kuleta miswada muhimu kwa hati ya dharura. Kama Spika, Anne Makinda mwenyewe alikuwa anaogopa muziki wangu, hawa watendaji wa Halmashauri wataniweza? Alitamba Machali.
Mbunge huyo alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kueleza namna baadhi ya viongozi wa NCCR walivyokuwa wakitumika kuhujumu miradi ya maendeleo, akimtaja mmoja wa madiwani wa Kasulu kama chanzo cha matatizo ndani ya chama hicho.
Zitto licha ya kuwataka wananchi wa Kasulu kujiunga na chama hicho, alisema Machali alishajiunga nao muda mrefu na kwamba alichokuwa anasubiri ni kukabidhiwa kadi. “Tulisema lazima tupate baadhi ya wabunge na viongozi maarufu kutoka vyama vingine, sasa tumeanza na Machali na wengine watafuata,” Zitto.
Viongozi wengine waliojiunga na chama hicho jana ni pamoja na kada wa CCM, Emmanuel Mbwiliza aliyewahi kuwa Diwani wa Kata ya Nyumbigwa hadi mwaka 2010 pia akiwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kuanzia 2007 hadi 2012.
Katika mkutano huo pia viongozi wengine wa NCCR kutoka Kasulu Mjini na Kasulu Vijijini walijiunga na ACT huku wakiahidi kupambana kuhakikisha wanashinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Azam FC imekamilisha usajili kwa Wachezaji wa Kigeni kwa kumsajili huyu.. (Picha)

Azam FC imekamilisha usajili kwa Wachezaji wa Kigeni kwa kumsajili huyu.. (Picha)


wanga sign
Klabu ya Azam FC imekamilisha nafasi zake saba za kusajili raia wa kigeni kufuatia sheria iliyowekwa na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) ambalo linaruhusu kusajili wachezaji wasiozidi saba raia wa kigeni.
Usajili huo unakuwa pigo kwa golikipa Nelson Lukong raia wa Cameroon na Ryan Burge raia wa Uingereza ambao wote walikuja kufanya majaribio na Azam FC.

Azam FC imetangaza kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Allan Wanga aliyekuwa anakipiga katika klabu ya Al Merrikh ya Sudan.. Allan Wanga amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Azam FC.
AFC-Allan-Wanga-2-300
Stori za mwanzo ilikuwa Allan Wanga na Nelson Lukong Bongaman golikipa kutokea Cameroon aliyekuwa anakipiga katika klabu ya AS Vita Club ya Congo kushindwa kufikia makubaliano na Azam FC baada ya kugoma kufanya majaribio ili kocha Stewart Hall aangalie viwango vyao kabla ya kuwasajili.
AFC-Allan-Wanga-300
Kufuatia usajili wa Allan Wanga Azam FC imemaliza nafasi zote saba za kuwasaji wachezaji wa kigeni, hadi sasa Azama FC imewasajili Serge Pascal Wawa, Kipre Tchetche, Kipre Michael Balou kutokea Ivory Coast na Jean Baptiste Mugiraneza kutokea APR ya Rwanda, Didier Kavumbagu kutoka Burundi, Brian Majwega kutokea Uganda na Allan Wanga aliyekamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni.

Mastaa 10 wa Nigeria na magari yao >>>Wizkid, Davido, Kcee nao wamo… (Pichaz)

Mastaa 10 wa Nigeria na magari yao >>>Wizkid, Davido, Kcee nao wamo… (Pichaz)


KCEE COLLECTN
Nigeria ni moja ya nchi za Afrika ambazo zinaongoza kwa kuwa na mastaa wengi wanaofahamika zaidi kuanzia kwenye filamu na muziki.
Kitu kingine kilichowasaidia kufika mbali ni ukongwe wa mastaa hao kuingia kwenye industry ya burudani..lakini ukongwe huo una mafanikio pia nyuma yake.
Wengi wao wamekua wakimiliki majumba ya kifahari na hata kuwa na magari ya thamani kutokana na kazi yao wanayoifanya.
Hapa kuna magari 10 ya mastaa mbalimbali wa Nigeria wanayomiki:-
PSUARE CARS
Magari ya Psquare
WIZKID CAR
Gari la Wizkid aina ya BMW X6
IYANYA
Gari la Iyanya aina ya Range Rover Sport
DBANJ
Gari ya D’Banj aina ya Aston martin Vantage
ICE PRINCE
Gari la Ice Prince aina ya Lamborghini Gallardo LP570 Superleggera
KCEE COLLECTN
Magari ya Kcee G-Wagon, Range, Audi
DON
Gari la Don Jazzy aina ya Porsche Carrera Gts
YEMI
Gari la Yemi Alade aina ya Mercedes Benz G-Wagon
SAVAGE
Gari la Tiwa Savage aina ya Volkswagen EOS
JMARTINS
Gari la J Martins aina ya Rolls royce phantom, G-wagon 550

Collabo ya Diamond na D’Banj? Vanessa kazungumzia tuzo za MTV, ‘Dear God’ ya Kala imevuka lengo?..(255 Audio)

Collabo ya Diamond na D’Banj? Vanessa kazungumzia tuzo za MTV, ‘Dear God’ ya Kala imevuka lengo?..(255 Audio)


onair
Diamond kambania collabo D’Banj? DBanj amesema aliwahi kukutana na Diamond na kutaka kufanya naye collabo lakini haikuwezekana.. sasa hivi wamepanga kufanya hivyo kabla ya mwaka kumalizika lakini hawajaweka wazi ni lini.
Diamond amesema walitakiwa kufanya wimbo wa pamoja lakini aliogopa kufanya kazi na msanii mkubwa kama huyo alafu ikatokea akashuka, inakuwa si kitu kizuri, alitaka kufanya kazi ngazi kwa ngazi ili kufika mbali.
dia
Diamond akiwa na D’Banj
Pamoja na kwamba Vanessa hakufanikiwa kurudi na tuzo ya MTV, Vanessa kikubwa anachojivunia ni kuweza kupata connections na wasanii wakubwa..amefanikiwa kurekodi wimbo na Patoranking, Sayi shay…pia wamerekodi wimbo wa miaka 10 ya muziki wa MTV akiwa na wasanii mbalimbali wakubwa.
VANEE
Vanessa Mdee aka Vee Money
Kala Jeremiah amesema mapokezi ya ngoma yake ya ‘Dear God’ umepokelewa na mashabiki wengi kuliko nyimbo zake nyingine..anaamini ulikua ni zaidi ya wimbo na anatarajia kufanya ngoma nyingine kali zaidi ya hiyo ili kutimiza malengo yake.
KALA
Kala Jeremiah
Wamesikika hapa wakihojiwa kwenye kipindi cha XXL CloudsFm…

Haya ndio maamuzi ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi kwa vile Obama hatowatembelea?


Haya ndio maamuzi ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi kwa vile Obama hatowatembelea?


DCF 1.0
Babu Owino ni Kiongozi wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Nairobi, aliwasilisha barua yake kwa Balozi wa Marekani ambaye yuko Kenya, ndani ya barua kulikuwa na Ujumbe wa Wanafunzi wa Chuo hicho kwamba wanahitaji Rais Obama akitua Kenya apitie na Chuoni hapo kwa ajili ya kuongea nao !!
sonu
Babu Owino.
Ratiba ikaonesha kwamba Rais Obama hatofika hapo… hawakupenda kwa sababu mwaka 2006 Rais Obama akiwa Senator wa Illinois alitembelea Chuoni kwao na akapanda mti wa kumbukumbu.
Obama-iyo-Wangari-Maathai-oo-geed-ku-beeray-Nairobi-University-2006-kii
Hii ilikuwa mwaka 2006, Rais Obama akipanda mti Chuo Kikuu Nairobi pamoja na Marehemu Mama Wangari Maathai.
Kwenye barua ya wanafunzi hao ilionesha  kwamba wapo ambao wako tayari kujiua, wengine watajipanga kuukojolea mti aliopanda mwaka 2006… Babu Owino alikutana na Rais Kenyatta na wakaongea kidogo tu kwamba hiyo haikuwa kitu kizuri kufanya kwenye ugeni mkubwa kama huu.
Capture-3
Picha iliyonaswa Rais Kenyatta akiongea na Babu Owino siku chache zilizopita.
Mengine ni haya na yameshateka mitandao ya Kenya tayari, wanafunzi wa Chuo Kikuu Nairobi wameuchoma moto mti huo uliopandwa na Rais Obama, kuna mengine yatafuatia? Niko karibu na updates za Nairobi kila wakati likinifikia jipya utalipata hapahapa mtu wa nguvu.

Hii ndio hukumu iliyotolewa kwa mashabiki waliomsukuma mtu mweusi nje ya treni Ufaransa..

Hii ndio hukumu iliyotolewa kwa mashabiki waliomsukuma mtu mweusi nje ya treni Ufaransa..


chelsea fannnn
Unawakumbuka wale mashabiki wa Chelsea waliomshusha shabiki mwenzao kwenye treni  ya Paris Metro kisa ana asili ya Afrika?
Mahakana ya Stratford imewapiga marufuku kuhudhuria mechi zote za soka kwa miaka mitano ndani ya Ufaransa.
Richard Barklie, kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, Joshua Parsons pamoja na William Simpson wote kutoka Surrey wamepigwa marufuku kuhudhuria mechi baada ya mahakama kuridhika na adhabu hiyo.
hawa
Jaji Gareth Branston alisema kwamba chuki ya kibaguzi iliyooneshwa na mashabiki wa Chelsea katika treni hiyo ya Paris na kiliharibu sifa  soka ya Uingereza.
Ishu hiyo ilitokea wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa katika mji wa Ufaransa wakishabikia mechi ya klabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Paris Saint Germain July 17 2015.
Baadae ilisambaa video iliyomwonesha raia mmoja wa Ufaransa Souleymane Sylla akisukumwa nje ya treni na mashabiki hao.
NYOBAKI SIKU YA MWISHO HAPA DUNIANI

Tuesday, July 21, 2015

Bado siku tatu Obama kutua kenya pata yanayojiri......


CHECK NA MIMI KWENYE TWITTER
#TZA Siku tatu kabla ya Obama kutua haya
yameendelea kushuhudiwa Nairobi leo, ingia hapa
uione stori yote na... fb.me/3BT8qx4zN
millard ayo
@millardayo
Show Summary
23m
Tweet to @millardayo
#TAGS
MAGAZETI MAGAZETI PB DUNIANI HEKAHEKA
255 DIAMOND PLATNUMZ U HEARD
BONGOFLEVA AYOTV KENYA AJALI
STORI KUBWA MAGAZETI TOPNEWS
BONGOMOVIE VIDEO MPYA ZARI ALI KIBA
STORI PEKEE WEMA SEPETU
HOME NIFAHAMU WASILIANA NAMI
MATANGAZO TEAM
KWANINI SHEDDY CLEVER KAMBLOCK RICH MAVOKO
INSTAGRAM?
MANENO YA ABDU KIBA KUHUSU ALI KIBA NA DIAMOND
PLATNUMZ
ZILIZOSOMWA SANA
MGAWANYO WA STORI
RELATED ITEMS KENYA
Ijumaa July 24 2015 Kenya itashuhudia kutua kwa Rais
Obama kwa mara ya kwanza tangu awe Rais wa Marekani…
Wamarekani wanajali sana kuhusu Usalama wa Rais wao,
tulisikia ishu ya kutua kwa wanausalama wa kutosha pamoja
na magari ambayo yalianza kushushwa zaidi ya mwezi
mmoja kabla ya siku ya Obama kutua.
Bado leo Viwanja vya Michezo vya Chuo Kikuu cha Kenya
zimeshuhudiwa Helicopter kadhaa za wanausalama zikitua
na kuruka kuzunguka anga la Nairobi… waliobebwa humo ni
makomandoo ambao nao wameshushwa kuhakikisha
hakiharibiki kitu kwenye ishu ya Usalama wa Rais wao.

Mkulima wa mfano mkoani Mara.

Mkulima wa mfano mkoani Mara.
  
Mkulima wa  matikiti maji aweza kubadilisha maisha yake. Akikagua shamba la mkulima huyo wa kijiji cha MARASIBORA kata ya KISUMWA mkoa MARA KAIMU AFISA MANUNUZI WA WILAYA YA TARIME. BW. BONIPHACE YOHONA.Alisema, pamoja mkulima huyo bwana OSUNGA YOHANA mwenye matatizo ya mkono mmoja ni mkulima wa kuigwa katika kijiji hicho.


CCM KUWAWEKA WATANGAZANIA WA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI KIKAANGONI,,,,,,,,,.....

CCM KUWAWEKA WATANGAZANIA WA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI KIKAANGONI,,,,,,,,,.....
MWENYEKITI WA CCM KATA YA KIHESA aka JEMBE LAO HAKIWANADI WAGOMBEA WA UBUNGE .








MWIMBAJI WA NYIMBO ZA IJILI KATKA DIMBA

DR.WA HOSPITALI YA MKOA WA IRIONGA HAKITOA SERA ZAKE MBELE ZA WATU




Picha za wagombea ubunge jimbo la iringa leo wakiwa semtema.