Sunday, May 22, 2016

PICHA ZA MAKONGORO OGING.


Makongoro Oging’ enzi za uhai wake.
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi
Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya
Ocean Road jijini Dar. WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa
magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi,
wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa
Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging’ aliyefariki leo
jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu aliugua kwa kipindi kifupi na alikuwa akiendelea kwa matibabu
akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti
yamemfika.
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho
Marando (kushoto). Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri
taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata jijini Dar es
Salaam.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.
Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa
kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang’ ombe, jijini Dar es Salaam
walikuwa katika mgomo.