Saturday, April 11, 2015

WANAJESHI WA CHADEMA KUFUZU MAFUNZO MWANZA

CHADEMA Red Brigade wala kiapo Mwanza mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe

 Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, al maarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza siku ya Jumamosi Februari 28, 2015. Kiapo hicho kinafuatia kukamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza.Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe (kulia).Picha: K Vis blog
Michuzi
Read more



Habari Zinazoendana

1 month ago

Vijimambo

RED BRIGADE WALA KIAPO CHA UTII MBELE YA MH FREEMAN MBOWE

Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe (kulia)Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza.

DIAMOD KUJITOLEA KUFA

DIAMOND: BORA NIFE KULIKO KUMRUDIA WEMA

Musa mateja
KIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili. Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’. Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini safari hii Diamond amesema…
GPL
Read more



Habari Zinazoendana

(Yesterday)

Vijimambo

ALICHOKISEMA DIAMOND: BORA NIFE KULIKO KUMRUDIA WEMA


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Musa matejaKIAPO! Kuonesha kwamba hana mpango wa kurudi nyuma, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ amefungukia msimamo wake juu ya mwandani wake wa zamani, Wema Sepetu ‘Madam’ kwa kusema kuwa kamwe hawezi kumrudia tena, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.Licha ya Diamond kufunguka hayo, wawili hao wamekuwa na mapenzi ya vipindi, kuna wakati waliwahi kumwagana kisha kurudiana na hakuna aliyewahi kutoa tamko zito lakini...

3 weeks ago

Bongo Movies

Petitman: Bora Ninyang'anywe Mke Kuliko Kuachana na Wema Sepetu

Mfanyakazi wa kampuni ya Endless Fame, Petitman  ambaye mara zote ameonekana kuwa karibu sana na bosi wake , Wema Sepetu  amesema kamwe hawezi kuacha kuwa karibu na Wema eti kwa sababu  Wema  na Diamond wameachana, ukizingatia kuwa Pititman  na Diamond ni mtu na shemeji yake. (Petitman amemuoa dada yake Diamond, Esma)
Kauli hiyo inaashiria kwamba Petitman yupo tayari kunyang'anywa mke endapo uhusiano wake na Wema Sepetu hautaipendeza familia ya Diamond kuliko kuvunja uhusiano na Wema Sepetu...

1 year ago

BBCSwahili

Pellegrini: City ni bora kuliko Man U

Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema kuwa timu yake ni bora kuiliko Manchester United na kwamba itatamba katika CL.

3 months ago

BBCSwahili

Walcott:sisi bora kuliko kina Henry

Winga klabu ya Arsenal Theo Walcott,ameeleza safu yao ushambuliaji ya sasa ni bora Zaidi kuliko ya mwaka 2006.

2 months ago

GPL

BORA USIWE HEWANI KULIKO KUTOPOKEA SIMU!

NIJumanne tena! Kweli siku hazigandi kwani mara nimalizapo kuandika safu hii, kufumba na kufumbua siku ya kuandika tena inafika!Baada ya wiki iliyopita kumalizana na mada ya Mke Kumchuna Mume Ipo Sana! Leo nashuka na mada nyingine. Hii ni kwa wapenzi, wachumba au wanandoa. Kila mtu anajua maisha ya sasa kuhusu mawasiliano ni simu za mikononi. Simu hizi zimekuwa mwiba katika baadhi ya uhusiano kutokana na baadhi yao kuzitumia kwa...

2 months ago

GPL

BORA USIWE HEWANI KULIKO KUTOPOKEA SIMU-2

NI Jumanne nyingine tena ambapo safu hii ya Mapenzi na Maisha inakupa elimu, inakosoa na kurekebisha namna ya kuishi kwa watu waliopo ndani ya uhusiano. Mada hii inaendelea kutokea wiki iliyopita ambapo niliishia pale niliposema kuwa, nilibaini ugomvi wa kutopokea simu wakati inapatikana hewani unatokana na tabia ya mmiliki wa simu.  Nilisema baadhi ya watu wanajulikana kuwa, hawakai mbali na simu hata kwa dakika mbili, sasa...

1 year ago

GPL

Kim: Mbeya City ni bora kuliko Yanga, Simba

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen. Na Nicodemus Jonas
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen, amesifia kiwango cha timu changa kwenye ligi kuu, Mbeya City na kusema kuwa ndiyo timu iliyopo kwenye kiwango cha juu zaidi kwa sasa. Kim amesema katika mechi alizofuatilia, Mbeya City ndiyo imekuwa kwenye kiwango zaidi huku timu nyingine zikitetereka katikati mwa msimu.… ...

8 months ago

Bongo Movies

"Kimenuka kwa Diamond" Mashabiki wa Wema wamtaka aache 'kumtumia' Wema kibiashara.

Kundi la watu wanaojiita mashabiki wa Wema Sepetu, limeanzisha kampeni kwenye mtandao mmoja wa maarufu wa kijamii kampeni iliyopewa jina la #BringBackOurWema likimshinikiza mpenzi wake Diamond Platnumz amrudishe kwenye maisha yake ya zamani na kukuza career yake ya filamu.

Mashabiki hao wanaamini kuwa Diamond anampoteza Wema na amekuwa akitumia umaarufu wake (Wema) kujidhatiti zaidi yeye huku Miss Tanzania huyo wa zamani akiendelea kudidimia.
Hivi ndivyo maelezo...


WAGOMBEA UBUNGE RORYA 2015

ADVERTISEMENT
Wakati vuguvugu la uchaguzi mkuu wa mwaka huu likiendelea nchini, Tasnia ya michezo nayo imeanza kupata msukumo kwa wanamichezo kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kwenye uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Tayari wanafamilia wa michezo wanne, wametangaza nia ya kuhakikisha wanachukua majimbo kwenye uchaguzi huo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Wanamichezo hao ni: Wilhelm Gidabuday (anagombea kupitia Chadema)
Huyu ana kumbukumbu nzuri katika tasnia ya michezo hasa riadha kwani alikuwa mstari wa mbele kukosoa maandalizi waliyopewa wanariadha wa Tanzania walioshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka jana nchini Scotland.
Gidabuday amejitosa kuwania ubunge wa Jimbo la Hanang kwa tiketi ya Chadema, jimbo linaloshikiliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Mary Nagu wa CCM.
“Kwa kuamini kwamba kugombea nafasi yoyote ni haki ya msingi kikatiba, mimi kabla ya kujitathmini mwenyewe nimefanyiwa tathmini na watu wa rika tofauti ndani ya jamii, makundi hayo yakiwakilisha watu wenye busara katika jamii na kuniweka katika orodha ya watu wenye sifa stahiki,” anasema Gidabuday.
Ataitetea michezo bungeni
“Wananchi wa Hanang pia wameridhishwa na harakati zangu za kutetea wanamichezo, hususan riadha kitaifa, Watanzania wengi wananifahamu kwa jina la (mwanaharakati wa michezo Tanzania). Harakati zangu michezoni zimenifanya kuaminiwa na wadau wa michezo kote Tanzania,” anasema Gidabuday.
“Sheria namba 12 ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) ya mwaka 1967 licha ya kukosa meno, lakini pia imedharauliwa na viongozi wa wizara, BMT wenyewe na taasisi zilizokusudiwa kusimamiwa na sheria hiyo, na matokeo ya udhaifu huo umesababisha ufisadi ndani ya vyama vya michezo, ndiyo maana Tanzania tumekuwa watalii katika viwanja vya michezo kimataifa.
 Ili kuondoa hali hiyo nitatoa hoja binafsi sheria hii ibadilike sambamba na kuikumbusha Serikali umuhimu wa kuwa na kijiji cha michezo,” anasema Gidabuday.
Mada Maugo (anagombea kupitia Chadema)
Bondia huyu anajitosa kwa mara ya kwanza kuwania ubunge wa Jimbo la Rorya kwa tiketi ya Chadema, jimbo hilo sasa linaongozwa na Lameck Airo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Sijaingia kugombea ubunge kwa bahati mbaya, nimedhamiria kuwatumikia wananchi wa Rorya ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani na mimi,” anasema Maugo bondia namba tatu kwa ubora nchini kwenye uzani wa super middle.
Ataendelea na ngumi?
ADVERTISEMENT
“Ngumi siwezi kuacha hata kama nitapewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa Rorya, nitakachofanya ni kutenga muda wa kufanya mazoezi na kupunguza idadi ya mapambano kwa mwaka na kutenga muda mwingi wa kuwatumikia wananchi wa Rorya,” anasema Maugo.
Anasema kikubwa atakachokifanya bungeni ni kuwapigania Wanarorya hasa katika huduma muhimu za kijamii kama afya, barabara, maji na kunufaika na rasilimali walizonazo.
“Katika sekta ya michezo, hasa ngumi nitahakikisha unakuwa na usimamizi mzuri ili kuwafanya mabondia wa Tanzania kupiga hatua kimataifa kwani kuna madudu mengi yanafanywa na viongozi wanaosimamia ngumi ambayo yanadidimiza mchezo huu na kuufanya usisonge,”anasema Maugo.
Frederick Mwakalebela (Anagombea kupitia CCM)
Kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, Mwakalebela ambaye hivi sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe amejitosa tena kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwani mwaka 2010 alitoswa kwenye kura za maoni ndani ya CCM hivyo kushindwa kugombea kiti hicho.
Jimbo hilo sasa lionaongozwa na Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema.
Mwakalebela ambaye kabla ya kujiingiza katika siasa, alipata kuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anasema atatumia muda mwingi kuwatumikia Wanairinga katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lao endapo atapata ridhaa hiyo.
“Pamoja na kuwatumikia wananchi wa jimbo langu, sitaipa kisogo michezo, nitahakikisha Iringa haibaki nyuma katika soka la Tanzania na hata michezo mingine, sioni cha kutushinda katika hilo kama nimeweza kuhamasisha vijana kushiriki mashindano mbalimbali ya ndani, hakuna shaka kuwa tutapiga hatua pia kwenye michezo.
Innocent Melleck (Anagombea kupitia CCM)
Melleck anasema ameshawishika kuwania ubunge wa Jimbo la Vunjo ambalo sasa Mbunge wake ni Agustino Mrema wa Chama cha TLP, baada ya kushinikizwa kufanya hivyo na wazee wa jimbo hilo na atagombea kupitia CCM.
Anasema kama atapata ridhaa ya Wanavunjo kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu atatimiza ndoto yake ya siku nyingi ya kuwa mtetezi kwa wananchi wa Vunjo, sambamba na kuipigania sekta ya michezo nchini ambayo tayari ameanzisha mbio za Uhuru marathoni zinazolenga kutangaza amani ya Tanzania na kuwasaidia wanariadha nchini.
Wanamichezo walioonyesha njia
Wakati wanamichezo hao wakitia juhudi kuingia bungeni kwenye uchaguzi wa mwaka huu, tayari wapo wanamichezo bungeni kama Juma Nkamia ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, pia ni Mbunge wa Kondoa Kusini ambaye amewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba.
Pia yupo Mohamed Dewji ambaye ni Mbunge wa Singida Mjini, Joseph Mbilinyi ambaye ni Waziri kivuli wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Mbeya Mjini, yupo Ismail Aden Rage aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye sasa ni Mbunge wa Tabora Mjini.

KIDATO CHA SITA WAJIPANDE AWAMU YA PILI KUPANGWA

AWAMU YA PILI KUCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO

Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili kwa wanafunzi waliobaki kutokana na ufinyu wa nafasi za shule za kidato cha tano, baada ya kubaini uwepo wa nafasi hizo; na baadhi ya wanafunzi wenye sifa watachaguliwa kwenda kusomea ualimu.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa  Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),  Bwana Jumanne Sagini alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari tarehe 22/07/2014  jijini Dar es salaam juu ya wanafunzi waliofaulu masomo ya sayansi.

Serikali kwa kutambua umuhimu wa masomo ya sayansi na mwitikio chanya uliopo sasa kwa wanafunzi kusoma masomo hayo, imeendelea kuimarisha miundombinu ya shule kwa kutoa fedha za ujenzi, ukamilishaji na ukarabati wa majengo ili wanafunzi wengi zaidi waweze kusoma masomo ya sayansi.

Bwana Sagini alisema wanafunzi ambao wamefaulu vizuri masomo ya sayansi na wanapenda kusoma masomo hayo wanayo fursa ya kubadilisha tahasusi (Combination) endapo zinapatikana kwenye shule walizopangwa kupitia kwa wakuu wao wa shule.  Iwapo tahasusi wanazozitaka hazifundishwi kwenye shule hizo wanaweza kuwasilisha maombi yao kwa Maafisa Elimu Mikoa ambayo shule hizo zipo kupitia kwa wakuu wa shule walizopangiwa ili waweze kubadilishiwa tahasusi za sayansi kwenye shule zilizopo kwenye Mikoa husika.

“Jamii inaweza kuwasiliana na watendaji wa wizara na Mikoa kwa simu ambazo zinapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya waziri Mkuu- TAMISEMI. Hivyo, naendelea kuwasisitiza watendaji wote wa Elimu hususani Wakuu wa Shule na Maafisa Elimu Mikoa kusimamia utekelezaji wa suala hili. Lengo la Serikali ni kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi ili kuendana na Malengo ya Milenia na kutekeleza Mpango wa BRN.”alisema Katibu Mkuu.

Serikali inaendelea kusisitiza kila mwanafunzi kwenda kuripoti shule aliyopangiwa kuanzia tarehe 10-30 Julai, 2014, orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha Tano mwaka 2014 inapatikana katika tovuti za www.pmoralg.go.tz na www.moe.go.tz

Serikali inafanya juhudi mbalimbali za kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wataalamu katika fani za sayansi kwa kujiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kila Mwanafunzi aliyefaulu masomo ya sayansi anapangiwa tahasusi ya masomo ya sayansi.

Katika matokeo ya mtihani kwa mwaka 2014, inaonyesha kuwa jumla ya wanafunzi 22,685 kati yao wasichana 7,859 na wavulana 14,826, wamechaguliwa kusoma tahasusi za sayansi ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi 18,746 kati yao wasichana 5,038 na wavulana 13,708 kwa mwaka 2013.

Uchaguzi wa wanafunzi kidato cha tano kwa mwaka 2014, ulifanyika mwezi mei, 2014 na matokeo yake kutangazwa kupitia tovuti ya OWM-TAMISEMI mwezi Juni 2014.Tofauti na miaka mingine iliyopita, Ufaulu wa watahiniwa wa shule kwa mwaka 2013 katika madaraja ya I-III umeongezeka kutoka watahiniwa 35,357 mwaka 2012 hadi 71,527 mwaka huu. Ufaulu huu ni zaidi ya asilimia mia moja ya watahiniwa waliokuwa na sifa za kuendelea na masomo ya kidato cha tano mwaka 2013.


Matokeo haya  yanakaribia sana malengo ambayo Serikali imejiwekea kupitia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (yaani Big Results Now-BRN) ambapo serikali ilijiwekea lengo la kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa asilimia 60 mwaka 2013. Matokeo halisi yanaonyesha kuwa ufaulu umepanda kutoka asilimia 43 mwaka 2012 hadi asilimia 58.25 mwaka 2013.

Yapo manufaa mbalimbali ambayo yatapatikana kutokana na ufaulu huu wa wanafunzi kwa taifa na kwa wanafunzi husika. Kwa taifa ufaulu katika masomo ya sayansi utasaidia kupunguza uhaba wa wataalamu katika fani mbalimbali  za sayansi na pia unarahisisha kazi ya kuwapatia wanafunzi nafasi mbalimbali za kujiendeleza katika masomo ya ngazi ya juu.

AL SHABAB KUVAMIA CHUO KENYA NA KUWAMALIZA WENGI

Matukio 10 makuu baada ya mauaji Garissa

  • 10 Aprili 2015
Polisi wakishika doria katika eneo la tukio Garissa
Familia za wanafunzi 142 kati ya watu 148 waliouawa katika shambulizi la kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa wameruhusiwa kuchukua miili ya wapendwa wao.
Familia zimeanza harakati za safari ya mwisho ya wapendwa wao baada ya serikali ya Kenya kuwaruhusu kuzichukua miili kutoka kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo jijini Nairobi.
Huu hapa mukhtasari wa matukio baada ya shambulizi hilo.
Shambulizi lilipokuwa likiendelea
1.Shambulizi
Takriban wanamgambo 5 wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab washambulia chuo kikuu cha Garissa alfajiri.
Waliwapata wanafunzi wakiwa wamelala.
Waliingia chuoni baada ya kuua walinzi wawili langoni.
Walionusurika wanasema kuwa wavamizi hao waliwabagua wanafunzi waislamu na kuwaua wakristu.
Misa ya wafu huko Garissa
2.Uhuru ahakikisha taifa
Serikali ilitangaza kuwa watu 70 walikuwa wameripotiwa kuuawa na wengine 79 kuripotiwa kujeruhiwa.
Waziri wa usalama wa taifa generali mstaafu Joseph Nkaissery alitangaza idadi ya waliouawa kuwa ni 148 na kusema kuwa operesheni ilikuwa imekamilika
3.Idadi ya waliouawa yatangazwa
Wanafunzi 500 wameokolewa na maafisa wa usalama
Rais Uhuru Kenyatta ahutubia taifa na kutuma risala za rambirambi kwa wale waliouawa.
Serikali ilionyesha hadharani miili ya wanamgambo waliouawa na kuonyesha picha ya raia mmoja kutoka Tanzania aliyekamatwa.
Jamaa ya walioathirika
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa Serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya wakenya wanaolisaidia Al Shabaab.
Serikali yakiri kuwa mmoja kati ya washambuliaji hao alikuwa ni mwanawe Chifu wa kata ya Mandera.
Chifu huyo yamkini alikuwa ameripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwake mwaka uliopita.
4.Maswali yaibuka kuhusu Operesheni
Maswali yaibuka kuhusu hatua zilizochukuliwa na polisi baada ya kuarifiwa kuhusu shambulizi hilo.
Wananchi waizomea serikali kwa kutumia ndege kuwasafirisha waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery na Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett
huku kikosi maalum cha kupambana na magaidi al maarufu (RECCE) kikilazimika kusafiri kwa gari kwa zaidi ya saa saba.
Wanafunzi walionusurika
Kikosi hicho kilitumia chini ya dakika 15 pekee kukamilisha operesheni hiyo.
5.Makurutu 10,000
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa makurutu 10,000 wa polisi waliokuwa wamepigwa marufuku na mahakama kufuatia madai
Waliotekeleza shambulizi la Garissa watajwa
ya rushwa sasa hawatakuwa na budi ila kuingia katika chuo cha mafunzo ya Polisi ilikuimarisha idadi ya polisi na vilevile usalama wa taifa.
Mahakama ilikuwa imeharamisha kusajiliwa kwao kufuatia madai ya rushwa katika usajili.
6.Waliotekeleza Shambulizi watajwa
Raia wa Kenya Mohamed Kuno kwa jina jingine Mohamed Dulyadin,atajwa kuwa ndiye mshukiwa mkuu.
Serikali ya Kenya imetoa ruzuku ya shilingi milioni 20 za Kenya yaani dola $215,000 za kimarekani.
Taifa lahuzunika
Kuno aliwahi kuwa mwalimu katika eneo la Garissa kabla ya kustaafu na kujiunga na kundi hilo.
Mwengine aliyetajwa ni wakili Abdirahim Abdullahi aliyeongoza uvamizi huo.
Wanafunzi walionusurika Rais Uhuru Kenyatta aonya kuwa wale wanaoendeleza sera za Al Shabaab wako miongoni mwa wakenya.
7.Maiti yaletwa Nairobi
Manusura waliopatikana wamelala
Maiti ya wahanga wa mauaji hayo yaletwa mjini Nairobi kwa ndege za kijeshi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi mjini Nairobi.
Kituo cha kuwapokea waathiriwa wa mauaji hayo na jamaa zao kinaundwa katika uwanja wa michezo wa Nyayo mjini Nairobi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi mjini Nairobi
Orodha ya wanafunzi waliouawa na wale waliojeruhiwa inapachikwa katika lango la uwanja wa Nyayo.
8.Serikali yafunga miundo mbinu ya uchumi wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya yatangaza orodha ya mashirika kumi na tatu na akaunti za watu
binafsi wapatao 86 wanaoshukiwa kuhusika na ufadhili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab Garissa.
Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa wakifuatiliwa mienendo yao.
kampuni 13 za ubadilishaji na usafirishaji wa fedha nazo zimefungwa.
Maafisa wa Polisi wakishika doria
Jamii ya wasomali yalalamikia hatua hiyo ikisema ni mtego ambao umenasa waliokuwemo na wasiokuwemo.
9.Utambuaji wa maiti Chiromo
Shughuli ya utambuaji wa maiti yaanza huku familia nyingi zikitatizika kutambua miili ya wapendwa wao kufuatia kuharibiwa kabisa kwa miili.
Miili mingi ilikuwa na majeraha ya risasi kichwani.
Serikali ya Kenya yalazimika kutumia mashine maalum ya kutambua chembechembe za damu za DNA ili kuharakisha utambuzi wa miili.
Dukuduku zaibuka kuhusiana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wazazi ambao wamekosa miili ya wapendwa wao.
Muungano wa walimu na wafanyikazi wa vyuo vikuu (UASU) yadai kuwa takriban wanafunzi 166 hawajulikani waliko.
10.Uhuru aomboleza
Rais Uhuru Kenyatta aliwaandikia familia ya wahadhirika wote barua ya kuomboleza
Rais Uhuru Kenyatta jana aliwaandikia barua kila familia iliyopoteza mpendwa wao.
Wote walioathirika walipewa shilingi laki moja za Kenya,Jeneza na gari la kusafirishia maiti hadi makwao.
Makumi ya raia wa kigeni wakamatwa kote nchini kufuatia msako mkali unaoendelea.