Wednesday, February 8, 2017

Freeman Mbowe, gwajima na wengine 63 watajwa kwenye list ya wauza madawa ya kulevya.

MAJINA YA WATU 65 NDIYO ANAYATAJA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, PAUL MAKONDA AKIWATAKA WAFIKE KITUO CHA KATI DAR ES SALAAMU KWA MAHOJIANO

Mmiliki wa Slipway, Mmiliki wa Yatch Club, Mwinyi Machapta, Salehe wa MMI, Rose yupo China, Kiboko wa Mbezi, Hafidh wa Mbezi .....Idd Azzan atakiwa kufika Central Polisi Ijumaa saa Tano Asubuhi!! ...

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye atakiwa kufika Central Polisi Siku Ijumaa Saa Tano Asubuhi

Makonda pia amtaja Askofu wa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka naye afike kwa ajili ya mahojiano. Source  mwananchi .....leo

Tuesday, February 7, 2017

ibada za mashetani zashamiri mashuleni


Na Mchambuzi wetu toka roryamaendeleo

WAKATI wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Loleza iliyoko mkoani Mbeya hivi majuzi waliamua kumtimua shetani shuleni kwao kwa kumcharaza viboko nchi ya jirani ya Kenya mambo ni tofauti ambapo shetani amefanikiwa kuwaingia wanafunzi mioyoni na kuishi ndani yao.

kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Raisi Daniel Arap Moi Toroitich iliyo kuwa ikizunguka mikoa yote ya Kenya kuchunguza ibada za shetani, kama ufa hautazibwa sasa kudhibiti kasi ya wanafunzi wa Kenya kujihusisha na shughuli za Kishetani basi ukuta utajengwa.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa wakala kadhaa wa shetani hivi sasa wanazunguka katika mashule na vyuo vya elimu ya juu nchini Kenya wakidai kuwa wao ni maafisa wa Jumuiya ya Kikristo ya Wanafunzi "Kenya Students Christian Fellowship" lakini kinyume na hayo wakiwasajili wanafunzi kuwa watenda kazi wa shetani.

Ripoti hiyo imewashutumu walimu wa Kenya kwa kutokuwa waangalifu kiasi cha kuruhusu wageni kuingia hovyo kwenye mipaka ya shule ambapo imebainika kuwa baadhi ya wageni hao huwaletea wanafunzi madawa ya kulevya na zawadi ghali za kuwashauri wajiunge na ibada na kazi za shetani.

Ripoti ya Tume ya Rais Moi imetoa wito na tahadhari ikijulikana wazi kuwa vijana ndio tegemeo la Taifa kwa kusukuma gurudumu la maendeleo na kwamba upo umuhimu wa serikali kuchukua tahadhari kupambana na shetani kabla hajaipokonya vijana wake wanaopotoka kwa kasi.

Akielezea jinsi alivyoponea chupuchupu kuopolewa na shetani mwanafunzi mmoja wa kidato cha pili nchini Kenya ambaye sasa ameacha shule ameeleza kuwa aliingizwa kwenye ibada za shetani kwa mara ya kwanza katika maisha yake baada ya mama wa kambo, kumpa fedha nyingi sana kiasi cha kumpelekea ajihoji ni nini maana yake.

Mwanafunzi huyo ameieleza Tume ya Rais Moi ya kuchunguza ibada za shetani kuwa mama yake huyo pia alimpa saa ya mkononi ya thamani ambayo kila alipokuwa akiivaa ilikuwa ikimnyonya sana damu yake.

Katika tukio la kushangaza mwanafunzi huyo ameeleza kuwa siku moja akitoka shuleni alikutana na mwanamke mmoja mrembo sana akiwa na mwanaume ndani ya gari jeusi aina ya "mercedes Benz." Walipomkaribia walifunga breki na kumuita, watu hao wawili mwanamke na mwanaume walijitambulisha kwake ndipo walipomwomba aongozane nao mpaka kwenya hoteli moja ya kifahari ya jijini Nairobi.

Walipofika hotelini kwa mujibu wa ripoti ya tume hiyo watu hao waliagiza vyakula na vinywaji kisha wote watatu wakuendelea kisha wakamshawishi kwa lugha laini wakimbembeleza ajiunge na ibada za shetani.

Watu hao hawakuishia hapo tu bali walimwambia mwanafunzi huyo baba yake mzazi aliyefariki kwenye ajali ya gari mnamo mwaka 1992 alitolewa kafara kwa shetani na mamaye wa kambo yule aliyemuingiza kwenye ibada za shetani.

Baada ya watu wale kumshawishi kwa bidii alikubali kujiunga nao ambapo ana elezea kuwa wakimpa nguvu za kishetani za kuweza kubadili umbo lake la kibinadamu kuwa nyoka aina ya Cobra ,

Pia kwa nguvu za roho chafu za shetani aliweza kusafiri kimiujiza mpaka nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani na Ulaya pia walimpa nguvu za kuweza kupelekea ajali barabarani.

Mwanafunzi huyo anaelezea kuwa aliamua kubwaga manyanga na kuacha dini ya shetani siku alipopokea barua iliyoandikwa kwa kutumia damu tupu ikimtaka awatoe kafara kaka yake na dada yake ambao ni mapacha .

Anasema haikuwa lelemama kuhama kutoka kwa shetani kurejea maisha ya kawaida. Ilibidi Chama cha Wanafunzi Wakristo shuleni kwake wamfanyie maombi ya pekee ambapo baadaye walimu "alikata shauri kumuachisha masomo akapumzike nyumbani mpaka atakapoachana na shetani kabisa.

Naye mwanafunzi mmoja wa kike toka kidato cha kwanza katika shule moja ya sekondari mkoani Rift Valley huko Kenya ameelezea kuwa yeye aliingizwa kwenye ibada za shetani kwa kupewa zawadi kidogo kidogo na wasichana wenzake wa kidato cha nne waliokuwa ni wakala awa shetani shuleni hapo.

Amesema kuwa vitu alivyokuwa akipewa na wasichana hao ni pamoja na juisi za matunda na vinywaji vinginevyo, mkate, nyanya za kupona vyakula vingine vilivyosindikwa Wasichana hao pia kila mara walikuwa na mazoea ya kumpa fedha za matumizi kiasi cha shilingi 5000/- za Kenya

Lakini msichana huyo alishikwa na butwaa siku wasichana hao walipomfuata na kumtaka ajiunge na dhehebu lao la shetani kama hatua ya kulipia vitu ambavyo wamekuwa wakimpatia lijaribu kila awezavyo kuwaeleza kuwa kanisa lake linapinga ibada za shetani, hivyo alikuwa tayari kuwalipa zawadi zao lakini asijiunge nao.

Wasichana wale walikataa kata kata kurejeshewa zawadi zao. Ndipo msichana yule anaelezea kuwa kimiujiza alikuta tayari yeye ni mmoja wa waabudu shetani wazuri.

Toka Tume ya Rais Moi ilipotoa ripoti yake baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kwamba yale yaliyosimuliwa na viongozi wa tume hiyo siyo ya kweli.

Akithibithisha kiasi gani mambo hayo yana ukweli Mwenyekiti wa tume hiyo Rev, Bernard Muindi aliiambia gazeti la "Daily Nation kuwa

"people questining the report on devil worship have no basisi to do so , the report is reality , we have live evidence in our report, such as in "shimo la Tewa and Maragua,where we witnessed young men strip naked before getting down to worship" yaani Mombasa.

"Watu wanahoji kuhusu ukweli wa ripoti ya tume ya kuchunguza ibada za shetani, wanapaswa kuacha kufanya hivyo. Ripoti hii ni kweli na mengine hatujaelezwa bali tumeshuhudia kwa macho yetu huko "Shimo la Tewa Mombasa na Margua vijana wakijipanga kwenye mstari wakiwa uchi kama walivyozaliwa na kumuabudu shetani". Akielezea kuhusu matukio hayo Rev Muindi amesema kuwa huko Maragua walimbamba mwanafunzi mmoja mnamo majira ya saa 9 mchana akiabudu uchi wakati ambapo katika shule ya sekondari ya shimo la Tewa huko Mombasa walishuhudiwa na wanafunzi wakiwachinja kuku na kunywa damu zao.

Naye kiongozi wa chama cha kisiasa cha NDP Bw Raila Odinga ameitaka serikali ya Kenya kutopuuza taarifa za ripoti ya Tume ya Rais Moi sababu watakaoathirika na ibada za kishetani ni wananchi.

Mwenyeketi wa Baraza la Maimamu wa Kiislamu nchini Kenya Bw Juma Ngao amesema kuwa serikali ya nchi hiyo ni lazima ihakikishe inafanyia kazi, maoni yote yaliyotolewa na wananchi kwenye ripoti hiyo.

Naye kiongozi mmoja wa kanisa la Wasabato nchini Kenya Bw. Alex Ayub amesema kwa muda mrefu waabudu shetani wamekuwa wakiiba vitu kanisani mwao na kuvitumia kutengenezea alama zao.

Alama hizo za waabudu shetani zimetajwa kuwa ni pamoja na misalaba yenye nyoka , nyota yenye pembe saluti yeye pembe na namba 666

Maajenti (mawakala) wa shetani waliotajwa kuwa wamekuwa wakishawishi wanafunzi kujiunga na madhehebu ya shetani ni pamoja na wanafunzi wanaosoma vidato vya juu kuanzia kidato cha tatu mpaka cha nne hasa wanafunzi toka familia zenye uwezo mkubwa kifedha.

Wengine ni wasichana warembo sana vijana wa kiume wenye sura za kuvutia wafanyakazi wa "Matatu"hususani toka Nairobi ambao hutumia pesa na muziki uliofunguliwa kwa sauti kuvutia wanafunzi.

Matajiri kadhaa wanaoabudu shetani wamekuwa wakigawa zawadi kwa wanafunzi wanao kubali kujiunga na ibada zao na wengine ni wahubiri wa kujitegemea wanaoendesha mikutano ya Injili iliyojaa miujiza