Saturday, July 11, 2015

Sifa za Magufuli, Migiro na Amina

Magufuli, Balozi Amina, Migiro wapenya
tatu bora
Details
Published on Sunday, 12 July 2015 00:30
Written by roryamaendeleo , Dodoma
Hits: 1162
WAJUMBE
wa
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya CCM waliokutana
jana mjini hapa, walipigia kura majina matano ya
wawania urais kupitia chama hicho, ambapo Dk John
Magufuli, aliongoza na kufuatiwa na Balozi Amina Salum
Ali na Dk Asha-Rose Migiro.
Kwa matokeo hayo, viongozi hao walipelekwa katika
Mkutano Mkuu wa CCM kupigiwa kura na wajumbe wa
mkutano huo, ili kumpata mgombea urais wa chama
hicho katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC,
Nape Nnauye, wagombea wengine walioshindwa katika
kura hizo, January Makamba na Bernard Membe,
waliridhia matokeo hayo.
Dk John Magufuli
Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 Chato (sasa Mkoa
wa Geita). Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 –
2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994 alisoma Shahada ya Uzamili
(Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),
na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988 alisoma Shahada ya Kwanza ya
Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua
masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982: alisoma diploma Chuo cha
Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981 alipata elimu ya juu ya sekondari
katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978 alisoma elimu ya sekondari katika
Shule ya Sekondari Lake, Mwanza. Mwaka 1975 – 1977
alisema Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani
Kagera. Mwaka 1967 – 1974 alisoma Shule ya Msingi,
Chato.
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni,
Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora,
Dodoma. Uzoefu wa kazi, siasa Mwaka 2010 – hadi
sasa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato. Mwaka
2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Samaki; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo
Mashariki (Chato). Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa
Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na
Mbunge wa Biharamulo Mashariki. Mwaka 1989 – 1995:
Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative
Union (Ltd.) Mwanza.
Dk Asha-Rose Migiro
Dk Asha Rose Migiro alizaliwa Julai 9, 1956 katika
Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Migiro alianza
masomo katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Dar es
Salaam mwaka 1963 hadi mwaka 1966.Akahamia shule
ya Msingi Korogwe, Tanga na kuendelea na elimu ya
msingi mwaka 1967–1969.
Baadaye akajiunga kidato cha kwanza mpaka cha nne
katika Shule ya Sekondari Weruweru mkoani Kilimanjaro
mwaka 1970 mpaka 1973 na kidato cha tano na sita
katika Shule ya Sekondari Korogwe mwaka 1974 -1975.
Migiro alikuwa mmoja wa wasichana waliofaulu vizuri
Korogwe Sekondari na alipojiunga Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) mwaka 1977, alichukua Shahada ya
Kwanza ya Sheria (LLB) mwaka 1980.
Baada ya kukamilisha Shahada ya Kwanza, aliajiriwa
UDSM kusaidia kufundisha masomo ya sheria katika
nafasi ya Mhadhiri Msaidizi. Alifanya kazi hiyo kwa miaka
miwili, kabla ya kuendelea tena na masomo ya juu ya
sheria mwaka 1982–1984, alipohitimu Shahada ya
Uzamili ya Sheria (LLM).
Kati ya mwaka 1985–1988, aliendelea kufundisha
UDSM, ambapo mwaka 1988, alikwenda Chuo Kikuu cha
Konstanz, Ujerumani kusoma Shahada ya Uzamivu
(PHD) katika masuala ya sheria na kuhitimu mwaka
1992.
Dk Migiro alirejea Tanzania akiwa Mhadhiri Mwandamizi
na aliendelea kufundisha katika Kitivo cha Sheria cha
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambapo kati ya mwaka
1992 – 1994, alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba
na Utawala na kati ya mwaka 1994 – 1997 aliongoza
Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai. Mwaka 2000, Dk
Migiro aliingia rasmi katika siasa.
Anaongea vizuri lugha nne za kimataifa, ikiwemo
Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani na ni mke
wa Profesa Cleophas Migiro na wana watoto wawili wa
kike.
Ubunge, Uwaziri
Tofauti na wanasiasa wengi ambao hufikia ngazi za juu
za uongozi wa nchi kuanzia siasa katika nyadhifa za
vyama vyao, Dk Migiro amekuwa na historia tofauti
kidogo.
Yeye ameanza siasa za kujijenga akitokea katika
taaluma, akitazamwa na watu wengine kuwa ana uwezo
wa kulisaidia Taifa.
Mwaka 2000 aliteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kuwa
Mbunge na baadaye akateuliwa kuwa Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Watoto.
Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani mwaka 2005,
alimteua Dk Migiro kuwa Mbunge tena na Waziri wa
Mambo ya Nje, Januari 2006 na kuwa mwanamke wa
kwanza kuwahi kushikilia wadhifa huo.
Naibu Katibu Mkuu UN
Ilipotimu Januari 5, 2007, aliweka rekodi nyingine kubwa
kimataifa; alipoteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa (UN), Ban Ki-moon, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa
UN, akiwa mwanamke wa pili kushika wadhifa huo,
baada ya Louise Fréchette, Mwanadiplomasia wa
Canada.
Balozi Amina Salum
Ali Mwanadiplomasia Amina Salum Ali, alihitimu Chuo
Kikuu cha New Delhi , India - Shahada ya Uchumi (B.A),
mwaka 1979, pia alisomea masuala ya utawala wa fedha
na utafiti wa uendeshaji kwenye Taasisi ya Uongozi
(Institute of Management) Pune, India mwaka 1980.
Mwaka 1981 alihitimu Shahada ya Uzamili ya Masoko
katika Chuo Kikuu cha Pune, India - (Symbiosis College
of Management) na mwaka 1983 alijiunga na Chuo
Kikuu cha Helsinki, Finland, Kuchukua Diploma ya Utafiti
wa Masoko na Uuzaji wa Bidhaa za Nje.
Nyadhifa alizoshika Mwaka 1981 hadi 1982, Mchumi
Mwandamizi -Tume ya Mipango Zanzibar, mwaka 1982
hadi 1983, Mkurugenzi Biashara za Nje - Wizara ya
Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na mwaka
1983 hadi 984, Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar- Wizara
ya Biashara Zanzibar.
Nafasi nyingine ni, mwaka 1984 hadi 1985, Mchumi
Mwandamizi - Tume ya Mipango, Wizara ya Nchi Ofisi ya
Rais Zanzibar, mwaka 1985 hadi 1990- Mbunge Bunge
la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, mwaka 1985 hadi
1986- Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1986 hadi
1989- Waziri wa Nchi ,Wizara ya Mambo ya Nje.
Pia, mwaka 1989 hadi 1990- Waziri wa Fedha, Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1990
hadi 2000 – Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano Tanzania, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar, mwaka 2001 hadi 2005.
Amewahi pia kuwa Waziri wa Fedha, Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar , Mjumbe wa Tume ya Mipango,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mwaka 2005 hadi 2006-
Mjumbe Baraza la Wawakilishi. Nyingine ni, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Kiongozi Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, mwaka 2006 - Mwakilishi wa Kudumu wa AU
kwenye Umoja wa Mataifa.

Wafuasi wa lowassa walia na kamati Kuu.

Wafuasi wa Lowassa walia na uamuzi wa
Kamati Kuu
Details
Published on Sunday, 12 July 2015 00:08
Written by roryamaendeleo, Dodoma
WAFUASIwa
aliyekuwa
akiwania
uteuzi wa
CCM kuwa
mgombea
urais,
Edward
Lowassa,
ambaye
hakupata
nafasi ya
kuwa
miongoni
mwa
wagombea
bora
watano,
wamepaza
sauti zao wakionesha kutoridhishwa kwa jina la
mgombea huyo kuchujwa katika vikao vya uamuzi.
Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu
usiku wa kuamkia jana, wajumbe watatu wa kikao hicho
walilalamikia maamuzi hayo.
Mbunge wa Songea Mjini na Waziri wa zamani wa
Awamu ya Nne, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa,
walieleza kutoridhika na uamuzi huo.
Dk Nchimbi alisema hawajaridhika na uamuzi huo kwa
kuwa Lowassa aliondolewa katika hatua za awali na
Kamati ya Maadili aliyodai haina mamlaka kwa mujibu
wa Katiba ya CCM, kufanya hivyo.
Alisema Kamati Kuu ndiyo inayopaswa kufanya uteuzi
huo, na kuongeza kuwa Lowassa pia ana sifa ya
kukubalika ndani na nje ya chama, mojawapo ya vigezo
vilivyowekwa na chama hicho.
Aidha, jana asubuhi, mmoja wa wajumbe wa NEC, Dk
Raphael Chegeni alipokuwa akiingia ukumbini, alipaza
sauti akisema CCM ni chama chao na kuwa
wanakwenda kufanya uamuzi mgumu.
“CCM is our party (CCM ni chama chetu)… tunakwenda
kufanya uamuzi mgumu,” alisema Dk Chegeni na
kuongeza kuwa Lowassa anakubalika kwa wana CCM na
wananchi. Ndani ya Ukumbi wa NEC, wakati wajumbe
wakiwapokea viongozi wakuu wa chama hicho saa 5.50
asubuhi kuanza kikao, waliimba kwa sauti wakitaja jina
la Lowassa. “Tuna imani na Lowassa, oya oya oya…
Lowassa kweli…kweli…kweli…kweli kweli kweli Lowassa,”
waliimba takriban nusu ya wajumbe wakati viongozi hao
wakuu wa CCM walipoingia ukumbini akiwamo
Mwenyekiti wao, Rais Jakaya Kikwete.
Mara baada ya kukaa, Rais Kikwete alisema, “Haijapata
kutokea.” Lakini Lowassa mwenyewe aliwaambia
wanahabari jana asubuhi wakati anaingia katika kikao
cha NEC kuwa hajapata taarifa rasmi za kutopitishwa na
CC na akipata ataongea na wanahabari.
Tangu jina la Lowassa lichujwe na Kamati Kuu,
kumekuwa na hisia kali kutoka kwa wafuasi wake
wakitaka arejeshwe katika mchakato, ili apigiwe kura na
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).
Akifungua kikao hicho cha NEC jana, Rais Kikwete
aliwataka wajumbe kuwa watulivu, kupunguza jazba
akisema ukikasirika, jambo unalotaka kulisema halitatoki
vizuri.
Kikao hicho kilichokuwa na wajumbe 325 kati ya 374
kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana, kilikuwa na ajenda tatu ikiwamo ya kufanya
uteuzi wa wagombea urais wa Zanzibar na wa Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania.
Ilitarajiwa kufanya uteuzi huo kwa kupitisha majina
matatu kati ya matano yaliyowasilishwa kwao na Kamati
Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Hao ni mawaziri Bernard Membe (Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa), Dk John Magufuli (Ujenzi), Dk
Asha-Rose Migiro (Katiba na Sheria) na Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
Mwingine ni Balozi wa Umoja wa Afrika katika Marekani,
Amina Salum Ali. Majina matatu yatakayobaki
yalitarajiwa kupigiwa kura jana jioni katika Mkutano
Mkuu wa CCM kupata mgombea wao wa urais katika
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Dr Slaa kuteuliwa na Ukawa.


HABARI KUU LEO
POPULAR ON YOUTUBE
Dr Slaa athibitisha kuteuliwa na
UKAWA
Habari Zinazoendana
Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa
likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa
nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wa @twitter wa Dr
Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.

ACT wazalendo kupigwa marufuku na baraza la kilimo tz.

HABARI.BARAZA LA KILIMO
LAPINGA ACT KUTUMIKA KAMA
JINA LA CHAMA Baraza la Kilimo
Tanzania (ACT) limekitaka chama
cha siasa cha ACT – Tanzania
kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari
baraza hilo limekwsha sajili jina la
ACT kama kifupi cha jina la Baraza
hilo. Akizungumza leo katika kipindi
cha Hotmix cha EATV kinachoruka
kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00
hadi saa 2:00 jioni, Mwenyekiti wa
Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare
amesema kuwa jina ACT
linatambulika kama kifupi cha
Agricultural Council of Tanzania na
kwa mujibu wa taratibu za hati miliki,
jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na
watu wengine hata kama
litaambatanishwa na maneno
mengine. “Hata kama wakiongeza
maneno, bado kuna ACT, hiyo ni
nembo yetu, tumekwisha andika
barua kwenda kwa msajili wa vyama
vya siasa, pia tumeandika barua
kwenda katika chama hicho lakini
bado hatujapata majibu, nimekwisha
ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na
kumweleza kuwa wanatakiwa
kurekebisha kabla hatujaenda hatua
za juu zaidi(Mahakamani) ambazo ni
ghali.” Amesema Dkt Sinare.
#HOTMIX
#HABARI BARAZA LA KILIMO
LAPINGA ACT KUTUMIKA KAMA
JINA LA CHAMA Baraza la Kilimo
Tanzania (ACT) limekitaka chama
cha siasa cha ACT – Tanzania
kutotumia jina hilo kwa kuwa tayari baraza hilo limekwsha
sajili jina la ACT kama kifupi cha jina la Baraza hilo.
Akizungumza leo katika kipindi cha Hotmix cha EATV
kinachoruka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 12:00 hadi saa
2:00 jioni, Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Sinare Yusuf Sinare
amesema kuwa jina ACT linatambulika kama kifupi cha
Agricultural Council of Tanzania na kwa mujibu wa taratibu
za hati miliki, jina hilo (ACT) halitakiwi kutumika na watu
wengine hata kama litaambatanishwa na maneno mengine.
“Hata kama wakiongeza maneno, bado kuna ACT, hiyo ni
nembo yetu, tumekwisha andika barua kwenda kwa msajili
wa vyama vya siasa, pia tumeandika barua kwenda katika
chama hicho lakini bado hatujapata majibu, nimekwisha
ongea na Zitto Kabwe kuhusu hilo na kumweleza kuwa
wanatakiwa kurekebisha kabla hatujaenda hatua za juu zaidi
(Mahakamani) ambazo ni ghali.” Amesema Dkt Sinare.
#HOTMIX

CV YA MAGUFULI HAPA SOMA.

Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ametangaza
rasmi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Amesema kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kimetangaza rasmi kwa wanachama wake
wenye sifa kujitokeza kuwania nafasi hiyo kubwa
ya uongozi nchini, ameona hana budi kutangaza
rasmi azma yake.
Dk. Magufuli, amekuwa mbunge tangu mwaka
1995. Baada ya kushinda ubunge mwaka huo,
alichaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi; Wizara
iliyokuwa ikiongozwa na Anna Abdallah.
Anajulikana kama kipenzi cha aliyekuwa Rais wa
Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa, ambaye mara
kadhaa hakusita kumsifu hadharani, akimtaja
kama mmoja wa ‘askari wa miavuli’ katika baraza
lake la mawaziri.
Aidha, uhusiano wake na Mkapa umejidhihirisha
hadi kwenye masuala ya kifamilia, ambako mara
kadhaa rais huyo mstaafu ameweza kuhudhuria
hafla na misiba mbalimbali nyumbani kwa Dk.
Magufuli.
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk.
Magufuli alipewa fursa kwenye Mkutano Mkuu wa
CCM kusoma mafanikio ya chama hicho kwenye
utekelezaji wa ilani yake upande wa barabara.
Uwezo wake wa kukariri takwimu mbalimbali,
ulikuwa kivutio kwenye mkutano huo na sehemu
nyingine kama bungeni ambako hutakiwa kueleza
mafanikio ya wizara yake.
Hivi karibuni, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Ali
Hassan Mwinyi, alimsifu kwa kumtaja kama
‘simba wa kazi’ kutokana na uchapaji kazi wake
katika wizara mbalimbali ambazo ameziongoza.
Kwa upande wa wananchi, wengi wanamuona Dk.
Magufuli kama mmoja wa mawaziri wachapakazi
waliowahi kutokea katika historia ya taifa hili.
Hata hivyo, waziri huyo amekuwa akikosolewa
kwa uamuzi wake wa uuzaji nyumba za Serikali
kwa watumishi na hata wasio watumishi wa
umma.
Pamoja na dosari hiyo, watetezi wake wanaamini
kilichofanywa wakati huo wa utawala wa awamu
ya tatu kilikuwa ni matokeo ya uamuzi wa Baraza
la Mawaziri, na si uamuzi wa Dk. Magufuli
mwenyewe.
CV yake
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa
Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo
ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009)
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili
(Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na
baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza
ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika
Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia
na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya
sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa,
Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari
katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi
Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi,
Chato.
Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani
Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT
Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT
Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na
Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya
Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo
Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo
Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na
Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na
Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika
cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari
Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na
Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani
na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa
na kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa
na ana watoto kadhaa.

Magufuli juu ccm 2015

Magufuli kujinadi mbeli ya kamati kuu ya ccm usiku huu na kujipatia asilimia nyingi za kushinda katka 3 bora za ccm. Piya magufuli bila kusahau kazi yake kataja tu kwa kifupi sifa zake na kazi ndani ya wizara yake.

Picha za 3 bora ccm

Pata Top three hapa

NEWSSSSS. Watatu kupatikana tayari

Magufuli, Migiro na Anna kusonga melee

Pata picha ya uzinduzi wa kwaya kuu Iringa univesity

Kwaya kuu kuimarisha urafki wake na tucasa Leo kwenye uzinduzi wake

Pata picha mbalimbali za uzinduzi wa tucasa Iringa hapa.

Picha mbalmbali toka kwa watu makini katka kwaya makini ya chuo kikuu cha iringa Maarufu Kama Tucasa chini ya malezi mazuri ya kanisa la Ngome sda church. Pata kopi yako ya DVD kwa mamba 0768441610.

NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI TAR 30 JULAI 2015

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe anatangaza nafasi ishirini na tatu(23) za
kazi . maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo
yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili
Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo
1. MTUNZA KUMBUKUMBU MSAIDIZI DARAJA LA
II: (NAFASI 3)
Majukumu.
i.    Kutafuta kumbukumbujmajalada yanayohitajiwa
na wasomaji wanaohusika.
ii. Kuweka majalada katika makundi.
iii. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka, n.k)
katika majalada. .
iv. Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa
kumbukumbu/ nyaraka.
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
i.    Awe amehitimu Elirnu ya Kidato Nne (IV) au Sita
(VI)
ii. Awe amehitimu rnafunzo ya Utunzaji, wa
Kumbukumbu angalau katika ngazi ya Cheti
katika mojawapo ya fani ya Masjala.
Ngazi ya Mshahara: TGS B
Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
i.    Mwombaji awe raia wa Tanzania
ii. Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua
miaka 18.
iii. Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti
cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nsie]
sita, Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na
anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na
majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa
kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi
karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)
iv. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/ Sita
ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili
anayetambulika na Serikali. Aidha atakayewasilisha
taarifa na sifa za kugushi atachukuliwa hatua za
Kisheria na mamlaka zinazohusika.
v. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia
mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu,
maombi yake hayatashughu1ikiwa.
vi. Watumishi ambao wa1ikwisha kuajiriwa hapo
awali Serikalini na kupangiwa vituo vya kazi maeneo
mengine wasiombe nafasi hizi za kazi kwa kuwa
hawataweza kuingia kwenye Payroll ya Serikali.
vii.    Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti
cha kuzaliwa.
viii. Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya
Kiswahili.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi
yatakayowasilishwakwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi:
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani
ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
S.L.P. 01
MASUMBWE
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015,
Saa 9:30 Alasir.
Abdallah l. Mfaume
Mkurugeozi Mtendaji (W)
MBOGWE
SOURCE; MWANANCHI 09TH JULY 2015
============
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe anatangaza nafasi ishirini na tatu(23) za
kazi . maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo
yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili
Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo
2. Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III: (NAFASI 8)
Majukumu:
i.    Mtendaji Mkuu wa Serikali ya kijiji
ii. Kusimamia U1inzi na Usalama wa raia na mali
zao, kuwa M1inzi wa Amani na Msimamizi wa
Utawala Bora katika kijiji.
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa
uteke1ezajiwa Mipango ya maende1eo ya kijiji
iv. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
v. Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
vi. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi
kumbukumbu zote za Nyaraka za kijiji.
Mwombaji awe na Sifa zifuatazo:-
i.    Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI)
ii. Aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti
katika moja ya fani zifuatazo:• Utawala,
Sheria, Elirnu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha,
Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa
kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma
au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Ngazi ya Mshahara: TGS B
Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
ix. Mwombaji awe raia wa Tanzania
x. Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua
miaka 18.
xi. Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya cheti
cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha nsie]
sita, Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na
anuani, namba za simu za kuaminika pamoja na
majina ya wadhamini (Referees) watatu (3) wa
kuaminika na picha mbili (passport size) za hivi
karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)
xii.    Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/
Sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili
anayetambulika na Serikali. Aidha atakayewasilisha
taarifa na sifa za kugushi atachukuliwa hatua za
Kisheria na mamlaka zinazohusika.
xiii. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia
mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu,
maombi yake hayatashughu1ikiwa.
xiv. Watumishi ambao wa1ikwisha kuajiriwa hapo
awali Serikalini na kupangiwa vituo vya kazi maeneo
mengine wasiombe nafasi hizi za kazi kwa kuwa
hawataweza kuingia kwenye Payroll ya Serikali.
xv.    Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti
cha kuzaliwa.
xvi. Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya
Kiswahili.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi
yatakayowasilishwakwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi:
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani
ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
S.L.P. 01
MASUMBWE
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015,
Saa 9:30 Alasir.
Abdallah l. Mfaume
Mkurugeozi Mtendaji (W)
MBOGWE
SOURCE; MWANANCHI 09TH JULY 2015
============
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe anatangaza nafasi ishirini na tatu(23) za
kazi . maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo
yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili
Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo
3. KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III : (NAFASI 3)
Majukumu:
i.    Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za akwaida.
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasai1i shida
zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza
kushughu1ikiwa.
iii. Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za
matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari na
Mkuu wake na ratiba zingine za kazi zingine
zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia
kazi, na kumarifu Mkuu wake kwa wakati
unaohitajika.
iv. Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa
kazi kwa wasaidizi na kumuarifu kuhusus taarifa
zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao
v. Kutekeleza kazizozote atakazopangiwa na
Msimamizi wake wa kazi.
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:-
i.    Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita(VI)
ii. Awe amahitimu mafunzo ya Uhazili kutoka Chuo
cha Utumishi wa Umma au Chuo chochote
kinachojarnbuliwa na Serikali.
iii. Awe amefaulu somo la Hati Mkato na mwenye
uwezo wa kuchapa maneno themanini kwa dakika
moja na
iv. Awe amesoma masomo ya computer,
Ngazi ya Mshahara: TGS B
Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
xvii. Mwombaji awe raia wa Tanzania
xviii. Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua
miaka 18.
xix. Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya
cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha
nsie] sita, Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV)
ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
(3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za
hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)
xx.    Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/
Sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili
anayetambulika na Serikali. Aidha atakayewasilisha
taarifa na sifa za kugushi atachukuliwa hatua za
Kisheria na mamlaka zinazohusika.
xxi. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia
mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu,
maombi yake hayatashughu1ikiwa.
xxii. Watumishi ambao wa1ikwisha kuajiriwa hapo
awali Serikalini na kupangiwa vituo vya kazi maeneo
mengine wasiombe nafasi hizi za kazi kwa kuwa
hawataweza kuingia kwenye Payroll ya Serikali.
xxiii. Waombaji wote waambatanishe nakala ya
cheti cha kuzaliwa.
xxiv. Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya
Kiswahili.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi
yatakayowasilishwakwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi:
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani
ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
S.L.P. 01
MASUMBWE
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015,
Saa 9:30 Alasir.
Abdallah l. Mfaume
Mkurugeozi Mtendaji (W)
MBOGWE
SOURCE; MWANANCHI 09TH JULY 2015
============
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBOGWE
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mbogwe anatangaza nafasi ishirini na tatu(23) za
kazi . maombi ya kujaza nafasi yoyote kati ya hizo
yanakaribishwa kutoka kwa mtanzania yeyote
mwenye sifa hizo zilizotajwa katika tangazo hili
Nafasi zilizotangazwa ni kama ifuatavyo
4. DEREVA DARAJA LA II NAFASI: 06
MAJUKUMU
i.    Kuendesha magari madogo na malori
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali
nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari
kabla na baada ya safari
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari kwa safari
zote
Mwombaji awe na sifa zifuatazo:
i.    Awe amehitimu kidato cha Nne (IV)
ii. Awe amehitimu mafunzo ya udereva
iii. Awe na leseni daraja la “C” ya uendeshaji
Ngazi ya Mshahara: TGOS B
Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Waombaji:
xxv. Mwombaji awe raia wa Tanzania
xxvi. Awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua
miaka 18.
xxvii.    Maombi yote yaambatanishwe na nakala ya
cheti cha Taaluma, nakala ya cheti cha Kidato cha
nsie] sita, Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV)
ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika
pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu
(3) wa kuaminika na picha mbili (passport size) za
hivi karibuni (ziandikwe jina kwa nyuma)
xxviii. Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha Nne/
Sita ni lazima vithibitishwe na Hakimu au wakili
anayetambulika na Serikali. Aidha atakayewasilisha
taarifa na sifa za kugushi atachukuliwa hatua za
Kisheria na mamlaka zinazohusika.
xxix. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia
mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo juu,
maombi yake hayatashughu1ikiwa.
xxx. Watumishi ambao wa1ikwisha kuajiriwa hapo
awali Serikalini na kupangiwa vituo vya kazi maeneo
mengine wasiombe nafasi hizi za kazi kwa kuwa
hawataweza kuingia kwenye Payroll ya Serikali.
xxxi. Waombaji wote waambatanishe nakala ya
cheti cha kuzaliwa.
xxxii.    Maombi yote yaandikwe kwa lugha ya
Kiswahili.
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta, maombi
yatakayowasilishwakwa mkono au barua pepe
hayatafanyiwa kazi:
Barua zote zitumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani
ifuatayo:-
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe
S.L.P. 01
MASUMBWE
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 31/07/2015,
Saa 9:30 Alasir.
Abdallah l. Mfaume
Mkurugeozi Mtendaji (W)
MBOGWE
SOURCE; MWANANCHI 09TH JULY 2015

TANGAZO LA KAZI YA MUDA (BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA) MWISHO WA KUTUMA MAOMBI TAR 31/07/2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA
UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA KAZI YA MUDA
WAKUSANYA TAARIFA ZA TATHMINI YA KAZI –
(NAFASI 50)
Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa
Umma ambayo imeanzishwa kwa Hati Maalum
iliyotolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 162 la tarehe
3 Juni, 2011. Majukumu ya Bodi ni kufanya mapitio
ya mara kwa mara ya viwango vya mishahara, posho
na mafao mengine na kumshauri Rais juu ya misingi
ya miundo ya mishahara katika utumishi wa umma.
Katika mwaka wa fedha 2015/16, Bodi inatarajia
kufanya Tathmini ya Kazi katika Utumishi wa Umma
kwa lengo la kuoanisha na kuwianisha mishahara.
Bodi inahitaji watumishi 50 watakaomsaidia Mtaalam
Mwelekezi kukusanya taarifa za awali:
a) Sifa za mwombaji
i) Mtumishi wa Umma;
ii) Elimu ni kuanzia shahada ya kwanza au
stashahada ya juu na kuendelea;
iii) Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha kwa Kiswahili na
Kiingereza;
iv) Mwenye maadili, uwezo wa kufanya kazi
inayozingatia matokeo, kujituma na kukamilisha
malengo kwa wakati; na
v) Uelewa wa kutumia kompyuta.
b) Kazi za kufanya
i) Kuwahoji watumishi wa Umma na kujaza dodoso
la kukusanyia taarifa;
ii) Kuingiza taarifa za madodoso kwenye mfumo wa
kompyuta; na
iii) Kazi nyingine zinazohusiana na Tathmini ya Kazi
kwa maelekezo ya msimamizi.
c) Mshahara
Waombaji watakaofanikiwa, kwa kuwa ni watumishi
wa umma, wataendelea kulipwa mishahara yao kama
ilivyo sasa. Aidha, Bodi itagharamia mafunzo na
posho za safari za kikazi kwa viwango vya Serikali.
d) Muda wa Kazi
Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa jumla ya miezi 15.
Hata hivyo, kazi ya mtumishi mmoja mmoja haitazidi
siku 100.
e) Namna ya kuwasilisha maombi.
i) Maombi yote yaambatanishwe na Maelezo binafsi
(CV), nakala za vyeti vya elimu ya juu na mafunzo ya
kompyuta;
ii) Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao
kwa kupitia anwani ya: es@psrb.go.tz ; na
iii) Maombi yote yapitishwe na waajiri wenyewe.
f) Mwisho wa kupokea maombi
Zoezi la kupokea maombi litafungwa tarehe
31/07/2015.
Tanbihi: Watumishi wanaofanyakazi katika Mamlaka
za Serikali za Mtaa wanahimizwa kuleta maombi yao.
IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA
UTUMISHI WA
UMMA

MWANAMKE ALIYEJIBADILI JINSIA YAKE YA KIUME HUKO KENYA ASHINDA KESI

Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume
na kuwa mwanamke na kutaka jina lake
kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani
ameshinda kesi yake dhidi ya baraza la
kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa
Adrey Mbugua cheti kipya kinachoonyesha
hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa
anapokea matibabu ya kufanikisha jinsia
yake kubadilika kabisa.Bi Mbugua alilishitaki
baraza la kitaifa la mitihani nchini humo kwa
kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia
yake kwenye cheti hicho kutoka kwa
Mwanamme na kumtambua kama mwanamke
licha ya amri iliyotolewa katika gazeti rasmi
la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku
45 kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho
kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na utambulisho wa
mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la
'Audrey Mbugua' bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti
hicho haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake
wala alama alizopata Audrey na kuondolewa kwake
vile vile hakuna athari yoyote. SOMA ZAIDI>>

MKE WA JANUARY MAKAMBA ALIA MACHOZI.

IMANI YA JANUARY YA MPONYA.
January Makamba juzi usiku aliongea kwa imani
kubwa na kujiamini akiamini viongozi wa chama
chake watafata taratibu na sheria.Amewashukuru
wote wenye mapenzi naye toka mchakato unaanza
hadi leo utakapofikia kikomo.
at Saturday, July 11, 2015

Kilio kutanda baada ya watu kukatwa Dodoma

LE MBEBEZ AHANGUA KILIO CLUB
YA USIKU BAADA YA MGOMBEA
KUKATWA.

ZOEZI LA ''AMEKATWA'' LAHAMIA BONGO STAR SEARCH ARUSHA.

Majaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba
limeamia mjini Arusha ambapo mchujo na ukataji
majina la endelea kwa kasi ili kupata washiriki
wachache kuelekea jijini Dar es Salaam.

Nafasi za kazi crdb bank Leo

CRDB Bank PLC is urgently looking for
suitable person to fill a vacant position of
Bank Officer Trainee
The ideal candidate will be candidate with
Bachelors degree in business or related
discipline from any recognized University.
How To Apply:
Interested candidates Apply through CRDB
online Recruitment Portal -
Recruitment.crdbbank.com
Or should submit an Application Letter
accompanied with copies of academic
transcript, certificates and with a detailed up
to date CV with two work related referees
addressed to;
Director of Human Resources
CRDB Bank PLc
P.O.Box 268,
DAR ES SALAAAM
Closing Date: 01-Aug-2015

KAULI NZITO ALIYO IANDIKA EDWARD LOWASA MTANDAONI KWAKE

Waziri mkuu mstafu Edward Lowassa
Ametoa kauli kuelekea kwenye  Vikao vya
Juu vya CCM vyakupitisha Jina la Mgombea
Urais ..

BREAKING NEWZZZ....TOKA KAMBI YA LOWASA JUU YA ACT.

Habari Toka katika kambi ya Lowasa
wakishirikiana  kwa pamoja wanamshawishi
ndugu Edward Lowasa kuhamia ACT na
kundi lake na kugombea urais kupitia
chama hicho.
wanaamini kuwa anawafuasi wengi na akikosa
mwaka huu hatopata nafasi nyingine tena
maiashani mwake kwa ushawishi alionao ndani ya
jamii

Zitto Kabwe auanika wazi Ufisadi wa Freeman Mbowe.

Zitto Kabwe auanika Ufisadi wa
Freeman Mbowe... Adai Tundu
Lissu ni kifaranga, hivyo anamtaka
mama kifaranga....Amegusia pia
kifo cha Chacha Wangwe
Akizungumza katika press conference ya CHADEMA
na waandishi wa habari iliyofanyika leo,
Mwanasheria mkuu wa Chadema, Mh.Tundu Lisu
alisema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni
wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa
kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009
alipokuwa akiwasiliana na akina Denis Msack wa
Mwananchi.
Lissu alisema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka
mashtaka ya Ugaidi ambapo katika mahojiano yake
ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba Zitto
hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa
Chadema imtose Wilfred Lwakatare
Lissu aliongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari
mawili ya Nimrod Mkono na Mkono mwenyewe
ndiye amewaambia taarifa hizo. Mkono
amewaambia kuwa amempa Zitto hela nyingi sana
na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia
mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod
Mkono .
====Huu ni ujumbe wa Zitto Kabwe kujibu
mapigo ya Tundu Lissu===
**
Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee
Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini
Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa
Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe
asifanye kampeni Musoma vijijini.
Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya
orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono
alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime
na Freeman akasema kwenye chama ametoa
mkopo na akalipwa.
Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010
Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya
Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam
Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu
anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima
limeanzishwa na fedha za chama kutoka
Conservative party?
Nimefanya internship yangu kwa Mkono and
Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba.
Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya
kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli
wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi
namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze
aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka
2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba
kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo
Club Bilicanas.
They must know I am not a push over. Chacha
died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake
aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole
kuhusu maadili.

Baadhi ya kazi za zitto Bunge.

Baadhi ya kazi za Zitto Bungeni
Kwa uzito na mahala unapofanyika mkutano huu, naomba
niwaletee kwa muhtasari kabisa baadhi ya kazi ambazo
Ndugu Zitto Kabwe amezifanya katika kusukuma mbele
guruduma la maendeleo katika nchi yetu.
1. MABADILIKO SEKTA YA MADINI
Zitto alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa mbunge
mwaka 2005 akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini
ambalo halina mgodi hata mmoja wa madini ukiachana na
wachimbaji wadogo wa udongo wa Pemba ambao una
soko kubwa hapa Kariakoo jijini Dar es Salaam. Hata hivyo
ajenda inayomtambulisha Zitto Kabwe kwa Taifa ni ajenda
ya mabadiliko makubwa aliyoanzisha katika sekta ya
Madini nyakati ambayo hakuna mwanasiasa aliyethubutu
kukosoa sera za uwekezaji kwa namna aliyofanya. Baada
ya kudokezwa kuwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini
Bwana Nazir Karamagi amesaini mkataba mpya wa Madini
akiwa hotelini nchini Uingereza, Zitto alimtaka Waziri
kujieleza ndani ya Bunge kuhusu mkataba huo na masharti
yake ya kikodi. Waziri huyo aliposhindwa Zitto aliwasilisha
Hoja Binafsi Bungeni (akiwa mbunge wa kwanza kufanya
hivyo katika Bunge la Tisa na la Nane kwa pamoja). Hoja
ya Buzwagi ilisababisha Zitto kusimamishwa ubunge kwa
miezi 4. Hata hivyo mnamo Septemba 10, 2007 alitangaza
Azimio la Songea lililomshinikiza Rais Jakaya Kikwete
kuunda Kamati ya Bomani ili kupitia mikataba yote ya
Madini nchini.
Kutokana na kazi yake hiyo leo Tanzania ina Sera mpya ya
Madini na Sheria mpya ya Madini ambayo imeboresha
nafasi ya Tanzania kufaidika na Madini, imeruhusu kisheria
Serikali kuwa na hisa kwenye migodi ( na hivi
tunavyoongea, kwa mfano, sasa Serikali inamiliki 50% ya
Mgodi wa TanzaniteOne). Makampuni ya Madini ambayo
yalikuwa yanatangaza hasara kila mwaka leo yanalipa kodi
ya Mapato na Halmashauri zenye migodi zinalipwa ushuru
wa huduma wa mabilioni ya fedha. Huyu ndiyo Kiongozi
wetu wa ACT Wazalendo. Hawa ndio Viongozi Taifa hili
linawataka. Viongozi wanaotenda na kutoa majawabu ya
changamoto za nchi. Sio Viongozi wanaolaumu tu eti
wakisubiri kushika dola ndio watende. Nani anayebisha
rekodi hii?
2. KUZUIA UBINAFSISHAJI WA SHIRIKA LA BIMA LA
TAIFA (NIC)
Zitto Kabwe alikuwa Waziri Kivuli wa Mipango na Uchumi
mwaka 2006 wakati Shirika la Bima la Taifa likiwa kwenye
mchakato wa Ubinafsishaji. Wafanyakazi wa TUICO Tawi
la Bima walimfuata wakielezea kwa ushahidi namna mali
za Shirika zilivyopangwa kuuzwa na wajanja wachache
kutaka kujiuzia Shirika na Mali zake hasa jengo la kitega
uchumi kwa bei ya kutupwa. Zitto aliwakilisha hoja hiyo
kwenye Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi chini ya
Mwenyekiti wake Ndugu Abdallah Kigoda na kuishawishi
Kamati kukataa ubinafsishaji wa NIC na badala yake
kuunda kikosi kazi cha kurekebisha Shirika na liendelee
kuwa Mali ya Umma.
Mwezi Novemba Mwaka 2006 Baraza la Mawaziri
lilikubaliana na hoja za Zitto alizotoa kwenye Kamati ya
Bunge na ndani ya Bunge na kuamua kuliondoa Shirika
kwenye mchakato wa ubinafsishaji na leo hii Shirika
limebaki kuwa la Umma na limeanza kurudi kwenye hali
yake. Aliendelea kulisaidia Shirika la Bima kwa kuagiza
(akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali ) kuwa Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma
yaweke Bima kupitia Shirika la Bima la Taifa na agizo hilo
kutekelezwa na Mashirika mengi ikiwemo Benki Kuu ya
Tanzania.
Sio Bima tu, Zitto akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Mashirika ya Umma aliagiza kuondolewa
katika orodha ya ubinafsishaji Shirika la STAMICO ili liweze
kushiriki kikamilifu katika sekta ya Madini na liliondolewa.
Huo ndio Ujamaa wa kidemokrasia ambao Chama chetu
cha ACT-Wazalendo kinautangaza, na huyo ndio Kiongozi
wetu ambaye ana uzalendo wa dhati kwa mali za
Watanzania. Nani anayebisha rekodi hii?
3. SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Mwaka 2008/2009 Zitto Kabwe aliweka rekodi nyingine ya
kuwa Mbunge wa kwanza kuzungumzia mabadiliko ya
sheria ya viongozi wa umma ili kuipa meno secretariat ya
maadili ya viongozi na kutengenisha biashara na siasa.
Alipeleka Bungeni Muswada Binafsi wa Sheria ili kufanya
mabadiliko makubwa ya Sheria Maadili. Hata hivyo
muswada ule ulizuiwa na Serikali kuingia Bungeni licha ya
kukamilisha kila hatua iliyopaswa.
Leo hii Chama chetu kinazungumzia kurejesha Miiko ya
Viongozi kuna watu wanadhani Zitto kaanza haya hivi
sasa, la hasha. Huu ni mwendelezo wa yale aliyokuwa
anaamini miaka kadhaa iliyopita na kwa kuwa yeye
anapenda kutembea anayoyasema alitushawishi wenzake
kufanya Miiko ya Viongozi kuwa sehemu ya Katiba ya
Chama chetu. Yeye ni Kiongozi wa kwanza wa kisiasa
kuweka hadharani Mali na Madeni yake hapa nchini. ACT
Wazalendo ni chama pekee cha siasa hapa nchini
ambacho Viongozi wake wanatakiwa kikatiba kutangaza
Mali zao, Madeni yao na Maslahi yao ya kibishara. Nani
anabisha rekodi hii?
4. UKAGUZI WA MAHESABU WA VYAMA VYA SIASA
Katika kuhakikisha kuwa kila senti ya fedha ya umma
inakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya
Serikali, Ndugu Zitto Kabwe aliwasilisha Bungeni
mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa, Sheria namba 5
ya Mwaka 1992 na kuwezesha CAG kukagua fedha za
vyama ambazo zinatoka Serikalini kama ruzuku. Sheria ya
Vyama vya siasa inataka kila Mwaka Serikali kutenga
kiwango kisichozidi asilimia mbili (2%) ya Bajeti ya Serikali
kama ruzuku kwa vyama vya siasa. Vyama hupewa
wastani wa Shilingi bilioni 20 kila mwaka na kugawana
miongoni mwao lakini fedha hizi zilikuwa hazikaguliwi
kinyume na Sheria za Fedha.
Baada ya Sheria hiyo kupitishwa na Bunge mwaka 2009,
Zitto alisimama kidete kuhakikisha inatekelezwa jambo
ambalo lilimletea uhasama mkubwa sana na viongozi
wenzake katika chama chake cha zamani akiwa Naibu
Katibu Mkuu. Zitto alipigana kwa kushirikiana na
Wazalendo wenzake katika Kamati ya Bunge ya PAC na
kufanikiwa na hivi sasa vyama vyote vinakaguliwa na
kuweka rekodi nyingine katika nchi nyingi za Afrika. Kwa
kazi hii iliyotukuka Zitto Kabwe amedhibiti fedha za umma
kwa vyama vya siasa na hivi sasa taarifa za mahesabu ya
vyama ipo wazi, na tumeona vyama vyote vikiwa na hati
chafu, vikiwemo vyama vya upinzani vya zamani. Ni wajibu
wa wanachama wa vyama hivyo kuwawajibisha viongozi
wao wanaogeuza fedha za ruzuku kuwa ni fedha zao
binafsi. Nani anabishia rekodi hiyo ya Kiongozi wetu?
5. KUFUFUA ZAO LA MKONGE
Mwaka 2012 Zitto Kabwe aliweka rekodi nyingine tena
akiwa mbunge wa kwanza katika Bunge la 10 kuwasilisha
Hoja Binafsi. Aliwasilisha Hoja Binafsini Bungeni akitaka
Serikali kufufua Kilimo cha Mkonge kwa kuwanyanganya
wawekezaji wakubwa mashamba waliyobinafsishiwa na
kuyaacha bila kulimwa na badala yake mashamba yale
wapewe wakulima wadogo. Zitto alitaka kubadilisha
mfumo wa kulima Mkonge kutoka mashamba makubwa
yanayomilikiwa na tajiri mmoja na kulimwa na manamba
mamia na kwenda kwenye mfumo ambao wakulima
wadogo wadogo wanalima Mkonge na hivyo kushirikisha
wananchi wengi zaidi kwenye uchumi wao.
Hoja hiyo ilipingwa na Wabunge kutoka Tanga lakini
iliungwa mkono sana na wananchi wa mkoa huo na hivyo
kumwona Zitto kama mwakilishi wao licha ya kwamba
alikuwa akiwakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini.
Katika Chama chetu ajenda ya kumilikisha Ardhi wananchi
ni ajenda kubwa na ACT Wazalendo kimekua chama cha
kwanza nchini kutangaza kinagaubaga kuwa kitazuia
uporaji wa Ardhi na kumilikisha wananchi ardhi yao
wenyewe. Nani anabishia rekodi hiyo?
6. KURASMISHA KAZI ZA SANAA NA BURUDANI
NCHINI
Kwa muda mrefu sana wadau wa tasnia ya sanaa na
burudani nchini walikuwa wanalalamika kazi zao kutokuwa
rasmi na hivyo kuibiwa na mchango wao katika uchumi
kutotambuliwa. Mwaka 2012 Zitto Kabwe akiwa Waziri
Kivuli wa Fedha alifanya kampeni maalumu ya kuhakikisha
kuwa wasanii hawanyonywi na kazi zao kutambuliwa
rasmi. Aliwasilisha Bungeni mabadiliko ya Sheria ya
Ushuru bidhaa ili kutambua rasmi kazi za sanaa na
burudani na kuhakikisha kuwa wasanii wanalipwa
wanavyostahili katika biashara ya miito ya simu.
Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge na Mamlaka ya Mapato
Tanzania ikaanza kutoa stempu rasmi katika CDs za kazi
za sanaa ili kudhibiti wazalishaji kuwanyonya wasanii.
Katika Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya mwaka 2015
tasnia ya Sanaa na Burudani imekuwa sekta rasmi ya
Uchumi na imeripotiwa kuwa sasa ina thamani ya shilingi
270 bilioni kama mchango wake katika Pato la Taifa. Hivi
sasa Wasanii wanafaidika maradufu kwa kazi zao kuuzwa
kama miito ya simu na wengine wanapata mamilioni ya
shilingi na kuboresha maisha yao kwa jasho lao. Nani
anabisha rekodi hii?
7. KUDHIBITI UKWEPAJI KODI NA MISAMAHA YA
KODI
Wawekezaji kutoka nje wamekuwa wakiibia nchi yetu kwa
kubadilisha badilisha majina ya makampuni yao na kubadili
wamiliki bila ya kulipa kodi hapa nchini. Watanzania
mnakumbuka jinsi majina ya mahoteli makubwa
yalivyokuwa yakibadilishwa. Kwa mfano kutoka Sheraton
kwenda Moevenpick na kwenda Serena sasa. Makampuni
ya Simu yalivyokuwa yakibadilishwa. Kwa mfano kutoka
Mobitel kwenda Buzz kwenda Tigo.
Vile vile kutoka Celtel kwenda Zain na kwenda Airtel. Haya
yamekuwa yakitokea kwenye maeneo mengi zaidi ya haya.
Yote haya yalitokea bila ya Serikali kupata kodi yeyote.
Kwenye mauzo ya Zain kwenda Airtel Serikali ilipoteza dola
za Kimarekani 312 milioni ( zaidi ya shilingi bilioni 600 kwa
bei za sasa za dola ). Kwa uchungu kwa nchi yake Zitto
Kabwe aliwasilisha Bungeni muswada wa sheria wa
kurekebisha sheria ya kodi ya Mapato na kuanzisha tena
kodi ya ongezeko la mtaji ( Capital Gains Tax ).
Marekebisho hayo yalipitishwa na Bunge kupitia Sheria ya
Fedha ya mwaka 2012 na mwaka huo huo Tanzania ilipata
mapato ya shilingi bilioni 50 kwa mauzo ya Kampuni ya BP
kwenda PUMA. Mwaka 2014 Tanzania ilipata dola za
kimarekani 222 milioni ( zaidi ya tshs 450 bilioni )kwa
mauzo ya sehemu ya vitalu vya gesi asilia vya kampuni ya
Ophir kwenda kampuni ya Pavilion ya Singapore.
Zaidi ya hapo Zitto na wazalendo wenzake katika Kamati
ya PAC walitoa maagizo ya kuhakikisha kuwa Misamaha ya
kodi yote inakaguliwa na ukaguzi wake kuwekwa wazi ili
kudhibiti mianya ya matumizi mabaya ya misamaha hiyo.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania CAG
anakagua misahamaha ya kodi na PAC iliweka wazi taarifa
ya kwanza ya ukaguzi wa misamaha ya kodi. Nani
anabishia rekodi hizi?
8. MABILIONI YA USWISS
Mwaka 2012 mwezi Novemba Zitto Kabwe aliwasilisha
Bungeni Hoja Binafsi kuhusu mabilioni ya Uswisi ikiwa na
lengo la kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu Watanzania
wanaoficha fedha nje ya nchi kinyume cha sheria. Bunge
lilipitisha hoja hii binafsi na kuitaka Serikali kufanya
uchunguzi kuhusu Watanzania wanaotorosha fedha
kwenda nje na kuchukua hatua stahiki za kisheria.
Tanzania iliingia katika rekodi ya kuwa nchi ya kwanza
katika nchi za Jumuiya ya SADC kupitisha Azimio la Bunge
kuhusu suala la utoroshaji wa fedha. Licha ya kwamba
Serikali haijatoa taarifa yake miaka miwili sasa toka Azimio
la Bunge namba 9 la mwaka 2012, na baada ya danadana
ya muda mrefu kutoka vyombo vinavyohusika Kiongozi
wetu Zitto Kabwe ameamua leo kupasua jipu la hoja hiyo
kwa kuweka wazi orodha ya kwanza ya Watanzania 99
wenye akaunti katika Benki ya HSBC ya Uswiss. Uongozi ni
umakini, na sio kukurupuka na kujitafutia sifa za
harakaharaka. Ilikuwa ni muhimu Ndugu Kabwe kufuata
taratibu zote kabla ya kuanika majina hayo hadharani. Sasa
leo baada ya kujiridhisha pasipo shaka atayaanika majina
hayo hadharani na wale waliokuwa wanambeza kwamba
kashindwa wanyamaze milele! Huyo ndio Zitto, mwenye
uvumilivu na ujasiri usio kifani. Anatenda anayosema. Nani
anabisha rekodi hii?
9. KUWAJIBISHA MAWAZIRI
Katika historia ya Tanzania ni Wabunge wawili tu
walioweza kutoa hoja zilizopelekea Mawaziri wengi
kuondolewa madarakani kwa mpigo. Ni Zitto Kabwe na
Dkt. Harrison Mwakyembe ambaye aliongoza kamati teule
ya Bunge iliyochunguza Mkataba wa kampuni feki ya kufua
umeme ya Richmond. Hoja hii ilipelekea Waziri Mkuu
kuwajibika kwa kujiuzulu na hivyo kumlazimisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano kuunda upya Serikali kwa kuteua
Waziri Mkuu mwingine.
Zitto ana rekodi ya kipekee. Kwanza mwaka 2012 baada ya
Taarifa ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya
fedha za umma, Zitto alikusanya sahihi za wabunge 75 na
kuandika hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Shinikizo hili lilipelekea Rais kufukuza kazi mawaziri 8
ambao Wizara zao zilitajwa kuwa na mahesabu machafu.
Pili mwaka 2013 baada ya Kamati ya Mali Asili na
Mazingira kutoa taarifa yake Bungeni kuhusu Operesheni
Tokomeza, Zitto alisimama ndani ya Bunge na kubadilisha
mjadala kwa kutaka Mawaziri wote ambao watendaji wao
walitesa wananchi kuwajibika. Mawaziri 4 waliwajibika.
Tatu, mwaka 2014 katika Taarifa Maalumu ya Kamati ya
PAC kuhusu uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Escrow
ya Benki ya Tanzania, Zitto na wazalendo wenzake wa
kamati hiyo walipelekea Mawaziri wawili maarufu kama
mawaziri wa Escrow na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kuwajibika. Uwajibikaji umekuwa ni ajenda kubwa ya
Kiongozi wetu na amekuwa hana aibu hata kwa watu
anaowaheshimu na rafiki zake. Alitaka wawajibike huku
akiwatazama usoni. Ni Viongozi wachache sana wenye
ujasiri wa aina hii. Huyu ndio Kiongozi wa chama chetu
cha ACT Wazalendo. Nani anabisha rekodi hii?
10. KUKATAA POSHO ZA KUKAA
Mwaka 2010 chama chake cha zamani waliweka katika
Ilani yao ya Uchaguzi kupinga posho kama hatua ya
kubana matumizi ya Serikali. Wakakubaliana kuwa
wabunge wa chama chao hawatapokea posho ya kukaa
(sitting allowance). Hata hivyo, ilipokuja katika utekelezaji
wenzake wote wakagwaya na Ndugu Zitto Kabwe ni
mbunge pekee aliyepinga posho za vikao na kuzikataa kata
kata kwa miaka mitano (5) mfululizo, ambazo ni takribani
shilingi milioni 21 kila mwaka. Katika kipindi hicho cha
miaka mitano Zitto alikaa kuchukua jumla ya Shilingi
Milioni Mia Moja na Tano (105,000,000)!! Kukataa pesa
yote hii kwa sababu ya ‘principle’ tu ni jambo nadra sana
kutokea katika mazingira yetu. Zitto anatembea maneno
yake. Zitto anatenda anayonena. Sasa kwa yote hata kwa
nini wasimchukie wenye roho zao za kwa nini?
Ndugu Wananchi,
Huyu ndio Kiongozi wa Chama chetu. Tunachoomba
Watanzania mumhukumu Zitto kwa rekodi zake na si kwa
propaganda za mahasimu wake.

Greece debt crisis. Eurozone ministers to decided on bailout

Greece debt crisis: Eurozone ministers to
decide on bailout
11 July 2015 Europe
The new proposals faced opposition from some in the Greek
parliament
Eurozone finance chiefs are gathering in Brussels for a
meeting that could decide whether new Greek proposals are
sufficient to secure a third bailout and prevent a possible
eurozone exit.
Greece's parliament overnight backed PM Alexis Tsipras's
new package.
But he faced anger from some in his own party for proposing
measures that were rejected in a referendum last Sunday.
Some creditors gave an initially positive reaction to the plans
but a bailout agreement is far from certain.
Follow the latest updates here
The creditors - the European Commission, European Central
Bank and International Monetary Fund - have sent a first joint
assessment to the eurozone ministers.
"Under certain conditions, they jointly see the proposals as a
basis for negotiation," an EU official told Reuters.
Greece is asking creditors for €53.5bn ($59.47bn; £38.4bn)
to cover Greece's debts until 2018, but the amount of the
new bailout could reach €74bn, as Greece is seeking a
restructuring of its massive debt, which it says is
unsustainable.
At the scene: Jasmine Coleman, BBC News, Athens
Punters are watching for their numbers on TV screens
outside a betting cafe in central Athens. Next to broadcasts
of motorbike racing, lottery draws and athletics, TV
commentators give the latest on the debt crisis.
But George Vassis, 45, is not betting on the politics. "Who
knows what will happen?" he asks. Like many here, he is
weary after months of talks and economic decline.
He runs a business information company and wants an end
to the current deadlock. "Something must be done. The
measures the government is offering are bad, but it's the
only way to go forward."
Mr Tsipras has faced backlash to his proposals, but for
George much of the damage has already been done. His
company will have to make redundancies either way - he is
just waiting to find out how many.
Will a deal be reached?
Did Greeks really fail to pay 89.5% of taxes?
Of the €74bn, €58bn could come from the EU's bailout fund,
the European Stability Mechanism , with €16bn from the
IMF, sources said.
Greece's creditors have already provided more than €200bn
in two bailouts over the past five years. The second expired
on 30 June, when Greece fell into arrears on an IMF loan.
A euro working group began a technical revue of the new
proposals in Brussels on Saturday morning.
The 19 eurozone finance ministers will review the proposals
afterwards and decide whether they form the basis for a new
loan deal, and whether to supply Greece with interim
funding.
There will then be a meeting of Eurogroup leaders in
Brussels on Sunday afternoon, followed two hours later by a
full meeting of EU leaders.
Although the new package has drawn support from the likes
of France and Italy, the reaction from Germany, which is
more exposed to Greek debt, has been more subdued.
One EU source told Agence France-Presse the new Greek
plan stood only a "50-50" chance of approval on Saturday.
Crisis countdown
11 July: Eurozone finance ministers discuss plans
(Brussels 13:00 GMT)
12 July: Eurogroup leaders meet (14:00 GMT) followed
by summit of all 28 members of the European Union
(16:00 GMT). Both Brussels
20 July: €3bn payment due from Greece to the European
Central Bank
Will EU leaders choose Grexit?
How has austerity affected the eurozone?
Ripple effect of crisis reaches Georgia
Without a deal, Greece risks crashing out of the euro.
Banks have been closed for two weeks now and a €60 (£43;
$66) daily limit on cash machine withdrawals, imposed on
28 June, remains in force for Greek citizens. Many people
say they have only been able to withdraw €50, as there are
no smaller denomination notes.
The measures submitted in the new Greek document
include:
tax rise on shipping companies
unifying VAT rates at standard 23%, including
restaurants and catering
phasing out solidarity grant for pensioners by 2019
€300m ($332m; £216m) defence spending cuts by 2016
privatisation of ports and sell-off of remaining shares in
telecoms giant OTE
scrapping 30% tax break for wealthiest islands.
Many of the ideas had previously been opposed by Mr
Tsipras - and when put to the Greeks in a referendum last
Sunday were soundly rejected.
The prime minister admitted that the package "entails many
proposals that are far from our pledges, from what we feel
is right for the recovery of the economy" and were only
"marginally better" than proposals put forward by the
creditors last month.

Simba kutaja mashine mpya matano

Mzungu Simba ataja mashine mpya
tano
KOCHA Mzungu wa Simba, Dylan Kerr, amesema amefanya
tathmini ya kina ya kikosi chake na kubaini
Kocha wa Simba, Dyan Kerr akifanya mazoezi wa wachezaji
wake.
ADVERTISEMENT
KOCHA Mzungu wa Simba, Dylan Kerr,
amesema amefanya tathmini ya kina ya kikosi
chake na kubaini kuwa anahitaji nyota watano
wapya kabla ya kuuanza msimu mpya na
amewahakikishia mashabiki wa Simba kwamba
mambo yatakuwa mazuri watulize presha.
Bosi huyo amewaambia mashabiki kwamba
anahitaji kipa mmoja, beki mmoja, kiungo
mmoja na mastraika wawili ili kumpatia wigo
mpana wa kuchagua kikosi cha kwanza.
Kerr alisema kipa wao namba moja kwa sasa,
Ivo Mapunda ni majeruhi na hafahamiki
atarejea uwanjani lini, hivyo ni vizuri timu hiyo
ikasajili kipa mwingine wa kiwango cha juu.
“Nilifanya tathmini ya wachezaji waliopo kwa
kuangalia historia tu na nafasi walizokuwa
wakicheza, sijatazama uwezo wao uwanjani.
Kwa haraka nimebaini kuwa tunahitaji nyota
watano wapya, kipa, beki, kiungo na straika
wawili, nataka kuwa na kikosi bora,” alisema
Kerr.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya
Vietnam, alisema bado hajaanza kufanya
mazoezi ya mbinu kutokana na baadhi ya
wachezaji waliokuwa na timu zao za Taifa
kushindwa kujiunga na klabu mpaka sasa.
Nyota ambao hawajajiunga na timu ni nahodha,
Hassan Isihaka, Mohammed Hussein
‘Tshabalala’, Abdi Banda, Laudit Mavugo na
Jonas Mkude aliyerejea nchini mwishoni mwa
wiki iliyopita akitokea Afrika Kusini
alikokwenda kufanya majaribio ya soka la
kulipwa.
“Hatuwezi kufanya mazoezi ya mbinu wakati
wengine hawajajiunga na sisi, tunafanya
mazoezi ya viungo hapa na ufundi kidogo,
mbinu na namna ya kushinda mechi ni baadae
tukikamilika wote,” alisema Kerr.

Mbinu za kurejesha penzi lililokufa?

UNATAKA KUREJESHA PENZI LILILOKUFA ?
by roryamaendeleo
20 minutes ago
ASALAMALEIKUM ndugu zangu Waislamu ambao mpo
ndani ya mfungu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan . Bila
shaka shaka swaumu inapanda na ishallah Mungu
atawafanyia wepesi mtaumaliza mwezi huu salama .
Nikirudi katika mada yangu ya leo, nazungumza zaidi na
wale ambao walikuwa wapenzi lakini kutokana na
sababu mbalimbali walifikia hatua ya kutofautiana . Penzi
lao likaota mbawa .
Wameona sera zao haziendani , wakaamua kuachana .
Kila mmoja anaanza kutafuta pumziko lingine kwa muda
wake .
Lakini wakati hayo yakiendelea , kuna mmoja kati ya
wawili hao anakuwa ameguswa na ugomvi wao .
Anataka kurejesha penzi , hajui ataanzia wapi. Huyo ndiye
ninayezungumza naye leo hapa.
Vipo vitu vya msingi vya kutafakari kabla hujaamua
kufufua penzi lililokufa , ni vyema ukajifunza :
JITATHMINI
Kabla hujaamua kufufua penzi lililokufa kwanza
unapaswa kujitathmini juu ya penzi lako la awali na
sababu ya kuachana kwenu . Jiulize ni nini kilisababisha
hadi mkafikia hatua ya kuachana ?
Pima uzito wa sababu hizo za kuachana kabla ya kuamua
kuomba nafasi upya . Sababu hiyo inaweza kubadilika au
haiwezekani ? Usije ukawa sababu ya kuachana kwenu ni
mwenzako kukwambia anaolewa na mtu mwingine
halafu wewe ukaendelea kulazimisha kuomba nafasi.
Sababu ya kuachana kwenu ikiwa ni ya yeye kupata
bwana wa kumuoa na mipango tayari imeshafika
patamu, huna haja ya kuendelea kurejesha penzi hilo
maana tayari linakuwa limeshafika hatua ambayo huwezi
kulizuia .
Jiulize nani alikuwa chanzo cha mgogoro ? Chanzo chake
ni nini ? Ukishagundua chanzo chake na nani alikuwa
anasababisha, anza kutafuta suluhu kwanza moyoni
mwako .
Jitathmini kama chanzo kilikuwa ni tabia yako wewe
labda mfano hasira , jiulize unaweza kubadilika ? Ufanyeje
ili uweze kubadilika ? Ukishabadilika, hauwezi kurudia
tena tabia hiyo?
Hakikisha kwanza unajishughulikia matatizo yako . Katika
maeneo yote ambayo wewe ulihusika, hakikisha
unajisahihisha mwenyewe ndipo baadaye utamshirikisha
mwenzako pindi utakapokuwa umekutana naye kwa ajili
ya mazungumzo.
TAZAMA VIKWAZO
Wakati unatafuta muda wa kukutana na mwenzi wako ,
jiulize kwa wakati huo ana kikwazo gani ? Yawezekana
wakati mnaachana hakuwa na kikwazo lakini wakati
unataka kurejesha penzi , unakuta mwenzako ana
kikwazo.
Hawezi kurudiana na wewe wakati huo tayari yupo katika
mikakati ya kufunga ndoa na mtu. Au yupo na mtu
ambaye tayari wameendana , wameshatambulishana kwa
wazazi na kuweka mikakati ya ndoa .
ANDAA SULUHU
Ukishabaini chanzo , sababu na kujiridhisha kwamba
umeshafanyia kazi upungufu wako , omba nafasi ya
kukutana na mwenzi wako. Ikiwezekana watumie hata
watu wake wa karibu ili wakusaidie kukukutanisha naye .
Muombe radhi. Mueleze kwamba umeshayafanyia kazi
matatizo yako . Umebaini tatizo na uko tayari kwa suluhu.
Hata katika maeneo ambayo yeye alikuwa akikosea,
tumia lugha nzuri kumueleza namna ambavyo anapaswa
na yeye kubadilika ili msijikute mnaingia tena kwenye
migogoro.
Usimlamu. Onesha dhamira ya dhati ya kutaka kuishi
kama zamani . Mpe nafasi pia akueleze vitu ambavyo
pengine ulikuwa unamkwaza . Vikubali na ahidi kuvifanyia
kazi .
Akikuelewa , ongeza upendo maradufu. Ishi kwa
kujikumbusha kila siku maeneo ambayo ulikuwa
unayakosea . Usirudie makosa . Hakika mtaheshimiana na
mtafurahia penzi lenu na kila mmoja akihofia kumuudhi
mwenzake .
Mara nyingi penzi lililokufa likifufuka huwa linakuwa
tamu , linakuwa na matokeo mazuri zaidi ya lile la awali .
Ni matumaini yangu mtakuwa mmenielewa , tukutane
wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri .

Mkwere kupata mtoto wa kike

MKWERE APATA MTOTO WA KIKE
by roryamaendeleo
9 minutes ago
Mtoto wa Komediani maarufu nchini, Hemedi Maliyaga
‘ Mkwere ’ aliyepewa jina la Shamsa Hemedi Maliyaga .
Chande abdallah
MSANII wa komedi anayeuza sura kupitia Kipindi cha
Mizengwe kinachorushwa katika Kituo cha Televisheni
cha ITV , Hemedi Maliyaga ‘ Mkwere ’ amefunguka kuwa
anajivunia kupata mtoto wa kike baada ya mkewe
kujifungua hivi karibuni.
Mke wa Mkwere na watoto wake , Shamsa na Kamira
mwenye hijabu, aliyevaa tisheti ni mtoto wa mpiga
picha wa ITV .
Akipiga stori na mwandishi wetu , Mkwere alisema mtoto
huyo aliyempa jina la Nurat ni wa pili baada ya wa kiume
na kuongeza kuwa amefurahi zaidi kumpata mtoto wa
kike kwani alikuwa akitamani kwa muda mrefu .
“Mwanangu anaitwa Nurat , kweli nimefurahi sana
nilikuwa na hamu sana ya kumpata mtoto wa kike sasa
furaha yangu imezidi baada ya kumuona , ” alisema
Mkwere .
Wanafamilia wa Maliyaga wakimbeba mtoto huyo .
Mkwere akimbeba mwanaye Shamsa .
Mkwere akiwa na familia yake na Mama Mkwe.

Banza atoka hospitali

MUNGU MKUBWA, BANZA ATOKA
HOSPITALI
by Global Publishers Ltd
16 minutes ago
Gladness mallya
BAADA ya mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan
Masanja ‘ Banza Stone ’ kulazwa katika Hospitali ya
Mwananyamala , Dar kwa siku saba , hatimaye
ameruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mwanamuziki wa Dansi nchini, Ramadhan Masanja
‘Banza Stone.
Banza aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo , Jumatano
iliyopita ambapo kwa mujibu wa kaka yake ana nafuu
japokuwa bado hali si shwari kwani daktari aliyekuwa
anamtibu aliwaeleza kwamba ndugu yao huyo ana tatizo
la upungufu wa damu.
“Tunamshukuru Mungu mgonjwa wetu ameruhusiwa
japo bado hali yake haijatengamaa kwani tofauti na
matatizo ya awali ya fangasi za kichwani , anakabiliwa na
upungufu wa damu hivyo tumeshauriwa tumpe vyakula
vya kuongeza damu, ” alisema Hamis .

Friday, July 10, 2015

Mkutano mkuu wa ccm kuonyeshwa mtandaoni

MKUTANO MKUU WA CCM
KUONYESHWA MTANDAONI

Chadema kutimu wengine Jana.

Waliotuhumiwa Mamluki Chadema
Wavuliwa Uongozi.
Na Bryceson Mathias, Kilosa.
NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Kata ya Ruaha, Jimbo la
Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua
Uongozi waliokuwa Viongozi wao na kuweka
Kamati ya Muda (Task Force), kwa madai ya kuwa
Mamluki ndani ya Chama chao.
Waliovuliwa Uongozi na kubaki na Uanachama ni
pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George
Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi,
William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na
Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.
Katika Kikao cha ndani cha Julai 2 (Ukumbi wa
Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa
Uchaguzi na Mafunzo wa Chadema Taifa, Benson
Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi
hao, aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo
wote walipaza Sauti; Wavuliwe Uongozi na kubaki
Wanachama!.
Aidha Tuhuma zilizoelekezwa kwa Viongozi hao, ni
Kuwafukuza Viongozi wenzao Watatu wa Chadema,
kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba
ya Chadema, ilihali wakijua ni kukinyang’anya
Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha
Chama Mapinduzi(CCM).
Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha Vikao vya
Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi ya
Chadema Kata, kwa Miezi zaidi ya Minne
walihamishia Vikao na Ofisi kwenye Mgahawa wa
mmoja wa Viongozi hao kinyume cha Katiba.
Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa
Mwenyekiti wa Muda kati ya Viongozi
waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara
tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti,
ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua
UKatibu aliovuliwa, Mponda.
Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka
kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu
za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa
Uongozi na kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu,
Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa
ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema
Hata hivyo, Longa alikiri kupokea Fomu za Viongozi
watatu waliovuliwa Uongozi na kubaki Wanachama
wa Chadema, Banda, Mponda na Mnunga, ambao
wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.
Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari,
kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea Udiwani
wa Kata hiyo wakiwemo Viongozi wenzake
waliovulia Madaraka, jambo ambalo limeendelea
kuwawatia Shaka Wana Chadema kuwa, huenda
kulikuwa na kitu nyuma ya Pazia