Friday, January 29, 2016

Uvamizi wa arthi yaendelea marasibora.

Wavamia arthi watua marasibora kwa kasi ambapo wamevamia arthi ndani ya kijiji hicho kilichopo Kata Kisumwa wilayani Rorya Mkoa Mara.tulipo fika kijijini hapo na kuongea na Mzee mmoja kwa jina Jackson Yohana aliyedai ni kijana mkumbwa wa familia ya mzee Yohana alisema haya toka mwaka 1987 kikao cha ukoo wa kasemo kilipo kaa baada ya Baba yangu kufariki na kunipa kusimamia Mali za Mzee Yohana ndipo nipoanza kazi hiyo na mpaka Leo naendelea kuvigawa kwa wajukuu na kwa wadogo zangu. Katika eneo la nyasuna katika kitongoji cha karama kuna MTU kajitokeza na kusema eneo nilake wakati mpaka Leo hii tunailima na maindi yangu yapo shambani mpaka Leo. Kijana huyu anasema kwamba eneo nilake na mpaka sasa kesi kapereka mahakama ya mwanzo na nilipo uliza mahakama kwanini kesi ya arthi isikilizwe hapa walijibu kwamba Mimi ni mvamizi wa eneo hili na kupelekea kesi kunishinda na nilipo Kata rufaa mpaka mahakama ya tarime na ukumu ukatoka kwamba nimeshinda nilipo omba nakala ya hukumu nikajulishwa kwamba nita pewa ilifika wiki mbili majibu nikakuta hukumu umebadilishwa na kuonyesha nimeshindwa naomba serekali ya Mzee j p magufuli kunisaidia kwani kijana huyu Marwa maguchi anapewa Pesa na Mjomba wake kijana wa Nyanguru ili kuonga na kuonyesha nimeshindwa kesi.

Kutana na samata hapa.

MARASIBORA MAJI NI HISTORIA NDEFU......

Maji bado ni story ndani ya Kata Kisumwa wilayani Rorya Mkoa Mara .ndani ya Kata hiki cha Kisumwa kulikua na mradi wa maji safi na salama toka kipindi cha baba wa taifa mwl.jk nyerere.na ilipo fika mwaka wa 1987 mradi huu ukapata kusimama kutokana na machine kuchoka kitu kilichopelekea Kata zima kukosa maji na kufanya wana Kisumwa kuishi kwa shida.ilipofka mwaka 2006 halmashauri ya wilaya Rorya chini ya mbunge lameck pamoja na Diwani malaki walileta wakandarasi na kuanza kazi ya kujenga mabomba mapya toka kijiji cha marasibora na nyanchabakenye ila ilipofika kuleta machine ya kusukuma maji toka sibora mpaka kwenye tank kubwa kilichojengwa kobwasa na kwa Mzee zephania nyanchabakenye kilikua chakavi kitu kilicho pelekea mwenyekiti wa kijiji cha marasibora wa kipindi hicho john akuti kigoma kusaini kupokea machine icho.ilipofika mwaka 2010 wakaja tena wengina na walichokifanya ni kuongeza tu mabomba ya kupamp maji toka chini ya arthi na wakaondoka pia mwaka 2013 walipo kuja wengine walichokifanya ni kuongeza ukubwa wa jengo la machine tu nakuondoka mpaka Leo nipesa nyingi zimetumika bila mafanikio kumbuka kwamba mpaka sasa wana marasibora na nyancha wana tumia maji yasiyo sala katika maisha yao yote.haya yalibainishwa na wana kijiji hicho walipo hongea na blog hii hapa kijijini kwao.
 
kumbuka ni kijana mwenye chini ya miaka kumi na leo hii amelazimika kutokwenda shule kutokakana na shuguli ya kutafuta maji.

mwenyekiti wa kitongoji cha karama bw.APIYO  katika picha iliyo pigwa karibu na mashine ya kupampia maji toka arthini katka mto Dago.
mkee wa NYAMBOCK katika shuguli ya kuchota maji karibu na jengo hilo maharufu kama dago.
picha ya mashine inayodaiwa kwamba inafanya kazi wakati toka kipindi cha mwl.j k mpaka leo akija badilishwa.
umeme nao mpaka leo ni historia kwani toka luku ya hofa toka tanesko ya unit 50 kwisha mpaka leo ni 0 kh.
Mzee jeckson yohana maharufu kama mkongwe wa kijiji.