Chelsea wapewa Everton, Watford waingoja Arsenal FA
- roryamaendeleo
Chelsea watacheza dhidi ya wapinzani wao katika Ligi ya Premia Everton kwenye robofainali Kombe la FA.
Mshindi kati ya Manchester United na klabu ya Shrewsbury inayocheza ligi ya daraja la tatu Jumatatu atacheza nyumbani dhidi ya West Ham.
Droo hiyo ya robofainali ilifanywa uwanjani Stamford Bridge Jumapili.
Kwingineko Reading, wanaocheza ligi ya daraja la pili, watacheza dhidi ya Crystal Palace nyumbani, nao Watford wawe wageni wa mshindi kati ya Arsenal na Hull mechi ya marudiano.
Arsenal na Hull walikosa kufungana mechi ya raundi ya tano iliyochezwa Jumamosi.
Mechi za nusufainali zitachezwa wikendi ya 11-14 Machi.
Chelsea walilaza Everton katika fainali ya Kombe la FA mwaka 2009 meneja wa sasa wa Chelsea Guus Hiddink alipokuwa kwenye muhula wake wa kwanza kwenye usukali Stamford Bridge.
"Ni zamani sana. Najua wanataka sana kulipiza kisasi. Tunatumai tutaendeleza ufanisi ambao tumekuwa nao Kombe la FA,” alisema Mholanzi huyo baada ya timu yake kulaza Manchester City 5-1 mechi ya raundi ya tano Jumapili.
Matokeo ya mechi za raundi hiyo ambazo tayari zimechezwa ni kama ifuatavyo:
- Arsenal 0-0 Hull
- Reading 3-1 West Brom
- Watford 1-0 Leeds
- Bournemouth 0-2 Everton
- Blackburn 1-5 West Ham
- Tottenham 0-1 Crystal Palace
- Chelsea 5-1 Manchester City
No comments:
Post a Comment