Sunday, February 21, 2016

HUYU NDIE MAMA ANGELINA MABULA, MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA.

 0
roryamaendeleo
Mama Angelina Mabula ni Miongoni mwa waliojitokeza kugombea Ubunge katika Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, akisifika kwa sifa kedekede kutokana na uchapaKAZI wake hali ambayo inatarajia kuleta mchuano mkali wa kumtafuta mgombea katika Jimbo hilo Agost Mosi mwaka huu ndani ya chama hicho.

Kama ulikuwa humfahamu Mama Mabula, basi tambua ya kwamba ni mwana mama shupavu na msomi ambae safari yake ilianza kupamba moto kuanzia mwaka 1981 baada ya Kuhitimu elimu ya Sekondari katika shule ya Lake iliyopo Jijini Mwanza ambapo mwaka 1983 alitunukiwa cheti cha Uhasibu kutoka Chuo cha Uhasibu Kurasini Jijini Dar es salaam.

Mwaka 1984 Mama Mabula alipata Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa katika Kambi ya Oljoro JKT na kuhitimisha safari ya Mafunzo hayo katika Kambi ya JKT, Kitengo cha Operation nguvu ya Kazi.

Safari yake ilizidi kupamba moto ambapo mwaka 1990 alitunukiwa Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka Chuo cha IFM kilichopo Jijini Dar es salaam na Mwaka 1991 Stashahada ya Uzamili kutoka Chuo cha IFM Dar es salaam.

Aliendelea kupiga kitabu zaidi ambapo Mwaka 2000 alitunukiwa Shahada ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Mwaka 2007 alihitimu Stashahada ya Maendeleo na Uongozi kutoka Taasisi ya Coady International ya nchini Canada huku Mwaka 2014 akihitimu Shahada ya Uzamili katika Maendeleo ya Jamii na Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Open University of Tanzania.

Mchango wa Mama Mabula umeonekana katika maeneo mbalimbali aliyowahi kuyatumikia na anayoyatumikia hadi sasa, ikizingatiwa kwamba alikuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT ambayo ni Jumuiya ya Wanawake CCCM, Mkuu wa Wilaya ya Mleba Mkoani Kagera, Mkuu wa Wilaya wa Kwanza katika Wilaya ya Butiamba Mkoani Mara na sasa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.
BONYEZA HAPA KUPATA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU
Mama Angelina Mabula

No comments:

Post a Comment