Wednesday, February 24, 2016

Mwana wa Sokwe azaliwa kwa upasuaji

Image copyrightBristol Zoo
Image captionMadaktari wakimzalisha sokwe kwa njia ya upasuaji
Mwana wa Sokwe anaendelea vyema baada ya kuzaliwa kupitia upasuaji katika hali isiyo ya kawaida.
Sokwe huyo anayetoka upande wa magharibi alizaliwa kupitia upasuaji usio wa kawaida baada ya mamaake kuonyesha ishara za ugonjwa hatari wa shinikizo la damu.
Alihitaji msaada wa kupumua,lakini sasa madaktari wanasema hali ya mama na mtoto iko shwari.
Image copyrightBristol Zoo
Image captionMwana sokwe
Kumekuwa na sokwe wachache waliofanyiwa upasuaji wakati wa kujifungua duniani,kisa cha hivi majuzi kikiwa kile cha San Diego Safari Park mwaka 2014.
Sokwe huyo aliye na siku 11 alizalishwa na Professa David Cahill ambaye amewazalisha wanawake wengi kupitia upasuaji ,lakini ilikuwa mara yake ya kwanza kumzalisha sokwe.
''Mbali na kuwa na watoto wangu,huu ni ufanisi mkubwa kwangu,kitu ambacho sitoweza kusahau tena,''alisema.
Image captionMwanasokwe
Aliulizwa maoni yake baada ya mamaake sokwe huyo kwa jina Kera kuugua ugonjwa wakati ambapo alikuwa karibu kujifungua.

No comments:

Post a Comment