Katibu mkuu mambo ya ndani ya nchi atunuku vyeo kwa maafisa 327 wa jeshi la magereza, chuo cha magereza kiwira, mkoani Mbeya
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira
akiwa katika Jukwaa akipokea Salaam ya heshima kutoka kwa Gwaride Maalum
lililoandaliwa na Wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili katika
sherehe za kufunga Mafunzo hayo ya Maofisa wa Jeshi la Magereza, Chuo
cha Magereza Kiwira kilichopo, Rungwe Mbeya(kushoto) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Rwegasira akikagua
moja ya Gadi ya Wanaume inayoundwa Gwaride rasmi la sherehe hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Rwegasira
akimvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza mmoja wa Wanafunzi
Wahitimu kwa niaba ya Wahitimu wote wa Mafunzo ya Uongozi Daraja la
Pili. Mwanafunzi huyo amefanya vizuri katika Mafunzo hayo.
Onesho Maalum la kujihami kutoka kwa Askari wa Jeshi la Magereza katika
namna ya kupambana na adui yeyote wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto)
akifurahia jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
nchi(katikati). Kulia ni Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, SACP.
Stanford Ntirundura.
Askari Wanafunzi ambao wanaendelea na Mafunzo yao ya Awali wakifuatilia
sherehe hizo za kufunga Mafunzo ya Uongozi Daraja la Pili.
Maafisa Wandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza wakiteta jambo mara baada ya kufungwa rasmi kwa Mafunzo ya
Uongozi Daraja la Pili(kulia) ni ACP. Solomon Urio(katikati) ni ACP.
Lazaro nyanga(kushoto) ni ACP. Ismail Mlawa.
(Picha zote na Lucas Mboje).
Na; Lucas Mboje, Rungwe
JUMLA ya Askari 327 wa Jeshi la Magereza, kati yao wanaume 257 na
wanawake 81 wametunukiwa cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza baada ya
kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Pili kozi namba 1 katika Chuo cha
Magereza Kiwira, Wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya.
Cheo hicho wametunukiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi,
Meja Jenerali Projest Rwegasira katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo
hayo zilizofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho leo Mei 20, 2016.
Akizungumza katika sherehe hizo Meja Jenerali Rwegasira amesema Askari
na Maafisa wa Jeshi la Magereza nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa
kuzingatia Haki za Binadamu na Utawala Bora kila wakati wanapotekeleza
majukumu yao ya kazi.
Jenerali Rwegasira amesema Maafisa hao wahitimu wakazingatie elimu
waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe mfano kipindi cha utendaji kazi
wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwaongoza wenzao ambao
hawakupatiwa elimu kama yao.
Aidha, amewaasa kutowatesa Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia
kwa kuzingatia kanuni na taratibu za uendeshaji wa magereza kwani
Wafungwa ni Binadamu kama watu wengine ispokuwa tu wameikosea jamii.
"Tuzingatie falsafa ya kwamba mfungwa yupo gerezani kwa ajili ya
kutumikia adhabu na si kwa kuongezewa adhani. Kwa kufanya hivyo,
Serikali yetu itakuwa inazingatia Utawala wa Sheria na hivyo kuwa Taifa
linalozingatia na kuheshimu Haki za Binadamu na Utawala Bora".
Alisisitiza Jenerali Rwegasira.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, John Casmir Minja amesema kuwa changamoto nyingi ambazo
kwa kiasi fulani zimeathili utekelezaji wa majukumu ya Jeshi hilo ni
pamoja na ufinyu wa bajeti, makazi duni ya maafisa na askari, uhaba wa
vitendea kazi na uchakavu wa vyombo vya usafiri.
Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa tayari Jeshi hilo limechukua
hatua mbalimbali za kufanya maboresho kwa lengo la kufanya Jeshi la
Magereza kuwa la kisasa katika kutekeleza majukumu yake kisayansi na kwa
ufanisi unaotarajiwa.
No comments:
Post a Comment