Magereza na mafunzo ya ujasiliamali kwa wafungwa
JESHI LA MAGEREZA NCHINI LASAINI MKATABA WA UFUNDISHAJI ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAFUNGWA LEO 18.05.2016-DAR ES SALAAM
Jeshi la Magereza limesaini Mkataba (MoU) na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Technoserve
– Tanzania kushirikiana katika ufundishaji wa wafungwa mafunzo ya
Ujasiriamali wakiwa wanakaribia kumaliza vifungo vyao magerezani ili
stadi hizo ziwasaidie kumudu maisha mapya baada ya kutumikia adhabu
zao.
Programu
hii itaendeshwa katika Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Mfuko wa
“Master Card” kwa vijana wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 18
hadi 30 hivyo wafungwa walioko katika Magereza yaliyomo Mkoani humo na
wengine wenye sifa toka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ili kupata mafunzo
kupitia progamu ya uimarishaji wa maendeleo ya vijana vijijini kupitia
biashara “STRYDE” inayoendeshwa na Taasisi hiyo.
Takwimu
za sasa zinaonesha kwamba kati ya asilimia 30 na 35 ya wafungwa
wanaomaliza vifungo vyao hurejea magerezani.Hivyo, mafunzo haya
yatalenga kuwafanya wanapomaliza vifungo vyao waweze kupata maarifa ya
kuanzisha shughuli zao wenyewe za kujipatia kipato halali na kuacha
vitendo vya uhalifu katika jamii wanamoishi vinavyowafanya kurejea
magerezani.
Aidha,
mafunzo haya ya Ujasiriamali yatajikita katika kuwafundisha kilimo
biashara, matumizi mazuri ya fedha binafsi, uwezo wa kutumia ujuzi,
ubunifu na tafakari ya kina katika kufanya maamuzi, mpango biashara,
mawazo ya biashara na uwezo wa kuandaa mpango biashara n.k.
Ushirikiano
huu ni mkakati endelevu wa Jeshi la Magereza katika kuboresha Programu
za Urekebishaji wa wafungwa magerezani ili wawe raia wema na wenye tija
katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Program za Ujasiriamali kwa wafungwa zinaendeshwa pia katika baadhi ya Magereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Dorcas International na New Life in Christ
katika Gereza la Karanga – ushonaji viatu, ufumaji na uokaji mikate,
Gereza Arusha – uokaji mikate, ufundi seremala na ufumaji.
Jeshi
la Magereza linawakaribisha wadau wa ndani na nje kushirikiana katika
urekebishaji wa tabia za wafungwa ili wawe na michango chanya katika
jamii na Taifa kwa ujumla.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO
MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment