SERIKALI YAJADILI RASIMU YA KISWAHILI YA MPANGO WA KUKABILIANA NA MAAFA
Ofisi
ya Waziri Mkuu imejadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango
wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wilayani Kilosa
Mei 30, 2016.
Rasimu
hiyo imejikita katika kutoa miongozo ya uratibu
katika kukabili dharura za aina zote za majanga yanapotokea
katika ngazi zote za Kitaifa.
Akizungumza
na wajumbe wa Kamati ya Maafa Wilayani Kilosa Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango
Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Naima Mrisho
alieleza kuwa muongozo huo ni sehemu ya kuisaidia
jamii katika kupata mbinu bora za kujiandaa, kukabili, na
kurejesha hali pindi maafa yanapotokea ili kuzisaidia jamii zetu.
“Ni
muhimu kuwa na mpango huo kwa kuzisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na
maafa yanayotukabili,”alisema Bi. Naima
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele alibainisha umuhimu wa
Mpango huo ikiwa ni sehemu ya kuanzia na inayotoa muongozo mzuri unaosaidia
katika Halmashauri yake katika kukabiliana na Maafa.
“Tangu mpango
kuanza kutumika Desemba 2013 Wilaya ya Kilosa imeweza kuwa na mbinu za
kuyakabili maafa yanapotokea hususani yale ya mafuriko” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Bw. Idd Mshili aliipongeza Ofisi ya Waziri
Mkuu kwa kuona umuhimu wa kuitembelea Halmashauri yao kwa kuupitia Mpango na
kuuboresha ili kusaidia kurahisisha uelewa kwa kua lugha ya Kiswahili
inaeleweka kwa urahisi hususani ngazi ya chini na kwa wanavijiji wanaokumbana
na maafa pindi yanapotokea.
“Nichukue
fursa hii kuwapongeza Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuona umuhimu wa kuubadili
mpango kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kufikia
makundi yote ya jamii kwa urahisi.”
AWALI: Mpango wa
Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa ulianza kutumika mwaka 2013
ikiwa na lengo la kuziwezesha Halmashauri kujiandaa na kuyakabili maafa
yanapotokea, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya Tathimini kwa Halmashauri
za baadhi ya Mikoa kwa kuangalia ubora wa mpango tangu uanze kutumika katika
Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Singida na Shinyanga kuanzia
Mei 23 hadi 30, 2016.
No comments:
Post a Comment