Saturday, April 9, 2016

Mahakama yatengua ushindi wa Chadema

wananchi
Mahakama yatengua ushindi wa Chadema

Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetengua rasmi matokeo ya udiwani, Kata ya Boma Mbuzi wilayani

Moshi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi imetengua rasmi matokeo ya udiwani, Kata ya Boma Mbuzi wilayani hapa yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema, Yudosi Tarimo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

Hukumu hiyo imetokana na kesi ya kupinga ushindi iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia CCM, Juma Raibu.

Hukumu hiyo iliyotolewa leo na Hakimu Mkazi, Pamela Meena ilisomwa na Hakimu Julieth Maole baada ya kusikiliza pande zote mbili na kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji.

Hakimu Maole alisema katika uchaguzi huo Tarimo alipata kura nyingi dhidi ya Raibu kwa tofauti ya kura moja.

Alisema katika vituo vinane vya kupigia kura vilivyokuwa katika kata hiyo, vilikuwa na tofauti ya matokeo ya udiwani wakati wa kuhesabiwa ikilinganishwa na idadi ya watu waliopiga kura.

ìKwa utofauti huo ulikuwapo ni wazi kwamba katika majumuisho ya kura yaliyompa ushindi mgombea wa Chadema haukuwa wake kutokana na mgombea wa CCM kuweza kuithibitishia Mahakama,î alisema hakimu huyo.

Raibu alifungua kesi ya kupinga matokeo ya udiwani yaliyompa ushindi Tarimo wa kura 3,512 dhidi ya kura 3,511 alizopata yeye.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo kusomwa, Tarimo alisema hajaridhika na atawasiliana na wanasheria wake ili waweze kukata rufaa kwa madai kuwa, katika uamuzi wake hakimu hakuzingatia ushahidi muhimu aliouwasilisha.

Baada ya hukumu kutolewa mamia ya wafuasi wa CCM waliokuwa wamefurika nje ya Mahakama hiyo walishangilia ushindi wa mgombea wao.

No comments:

Post a Comment