Tuesday, April 19, 2016

Mwigulu Nchemba amaliza Ziara Mkoa wa Mara kwa Mkutano Mkubwa wa Hadhara

Mwigulu Nchemba amaliza Ziara Mkoa wa Mara kwa Mkutano Mkubwa wa Hadhara

Mwigulu Nchemba ahitimisha ziara yake mkoa wa Mara kwa mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika uwanja serengeti.

Katika mkutano huo ambao Mwigulu aliambatana na Mbunge wa Tarime kwa tiketi ya CHADEMA  Mh.Easter Matiko ambaye kwa nafasi yake aliwaambia wananchi serikali ya magufuli na mawaziri wake wanaonesha mfano wa kufanya kazi bila kunagua vyama,Kitendo cha waziri kufika katika jimbo hili na kuzungumza na wananchi ni dhahiri umoja unakwenda kutamalaki.

Akizungumza na wananchi wa Tarime mjini,Mwigulu chemba amewaambia wanatarime kuwa,mnada wa ng'ombe Magena unafanyiwa upembuzi ili serikali ijiridhishe na ama uendelee kufanya kazi au uhamie Kirumi.

Mbali na mnada huo,Mwigulu amewaeleza wanatarime kuwa wizara yake imejipanga kuboresha mfumo wa usambazaji wa pembejeo kwa wakulima,mfumo ambao utahakikisha wakulima kwa silimia kubwa kama sio wote wanapata fursa ya kunufaika pembejeo zenye ruzuku ya serikali.

Kwa upande wa ufugaji,Nchemba anasema,"huu ni muda muafaka kwa wafugaji kuachana na kufuga mifugo mingi isiyo na tija kubwa,nimeongozana na wataalamu ambao wanaandaa utaratibu wa kuwapatia wafugaji elimu na maeneo ya kufuga kwa kisasa "mifugo michache,tija kubwa".

Pamoja na hayo yote,wakulima na wafanyabiashara wa tarime wameaswa kuachana na "LUMBESA" wakati wa kuuza mazao yao.Lumbesa inamnyonya mkulima na ni lazima tuipige vita kuanzia kwetu sisi wakulima kabla mazao yetu hayajafika sokoni.

No comments:

Post a Comment