Tuesday, June 21, 2016

Sherehe ya kula nyama ya mbwa yaanza China

Sherehe ya kula nyama ya mbwa yaanza China


Image copyrightREUTERS
Image captionRaia wanaofurahia mlo wa nyama ya mbwa nchini China
Sherehe ya kila mwaka ya kula mbwa imeanza kusini mwa taifa la China licha ya pingamizi kutoka katika taifa hilo na ugenini
Takriban mbwa 10,000 na paka wanatarajiwa kuuawa na kuliwa wakati wa sherehe hiyo ya siku kumi inayofanyika Yulin.
Wanaharakati wanasema kuwa hafla hiyo ina ukatili huku wale wanaotaka sherehe hiyo kupigwa marufuku wakiandikisha saini milioni 11.
Image copyrightAP
Image captionMbwa
Mamlaka ya eneo hilo inasema kuwa sherehe hiyo haiungwi mkono moja kwa moja na serikali lakini hufanywa na wafanyibiashara wa kibinafsi.
Je,sherehe hiyo inahusu nini?
Sherehe hiyo ya mlo wa nyama ya mbwa huwaleta pamoja watu wengi katika eneo la Yulin ili kujichagulia nyama ya mbwa, matunda na vinywaji.
Image copyrightREUTERS
Image captionSherehe ya nyama ya mbwa Yulin
Utamaduni wa kula nyama ya mbwa ulianza miaka 500 iliopita nchini China,Korea Kusini pamoja na mataifa mengine ambapo wengi wanaamini mlo huo huondoa joto mwilini wakati wa majira ya kiangazi.

No comments:

Post a Comment