Sunday, November 6, 2016

Mwanamke aliyemzuia Trump kujenga India

Mwanamke aliyemzuia Trump kujenga India


Smita PanvalkarImage copyrightAFP
Image captionSmita Panvalkar
Miaka mitano iliyopita mwanamke mwenye umri wa zaiid ya miaka 50 aliyekuwa akiishi kwenye jengo moja la miaka 87 mjini Mumbai alipata umaarufu mjini humo kwa kupinga mradi wa tajiri Donald Trump.
Taarifa zilimuelezea Smita Panvalkar ambaye alikuwa akiishi na mmewe , mtoto wake wa kiume na nduguye katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, kama kizuizi kikubwa cha Trump alipokuwa na mpango wa kuanza mradi wake wa kwanza nchini India.
Zaidi ya familia 20 ziliishi kwenye jengo ambalo lingebomolewa kujengwa kwa Trump TowerImage copyrightAFP
Image captionZaidi ya familia 20 ziliishi kwenye jengo ambalo lingebomolewa kujengwa kwa Trump Tower
Mwaka 2011 Trump, mfanyibiashara tajiri aliungana na mfanyibiashara mwingine raia wa India kujenga jumba la ghorofa 65 la Trump Tower lenye vyumba 50 vya kifahari.
Mji wa Mumbai unakumbwa na ubaha mkubwa wa ardhi, na mijengo yoyote mipya hujengwa baada ya majengo ya zamani kubomolewa kwa kuwalipa fidia au kuwapa makao mapya wakaazi wa zamani.
Hatma ya jengo la ghrofa la Pathare Prabhu ambapo Panvalkars alikuwa akiishi tangu mwaka 1990 ilikuwa hatarini.
Aliandikwa kwenye magazeti ya IndiaImage copyrightANUSHREE FADNAVIS/INDUS IMAGES
Image captionAliandikwa kwenye magazeti ya India
" Tuliishi masha ya kawaida hadi mwaka 2011, alisema Prasad Panvalkar ambapo alikuwa akilipa kodi ya dola 2.7.
Haikuchukua muda mrefu kabla ya Trump na mfanyibiasahara wa India kuafikia makubaliano ya kujenga jumba la Kwanza la Trump Tower nchini India.
Hata hivyo Smita Panvalkar alikataa kuondoka kabisa.
Familia hiyo iliendelea kuishi kwenye jengo hilo licha ya umeme kukosa kwa siku 45Image copyrightAFP
Image captionFamilia hiyo iliendelea kuishi kwenye jengo hilo licha ya umeme kukosa kwa siku 45
Matajiri hao walitoa fidia. Lakini Smita akasema kuwa hataondoka kamwe hadi apewe chumba ndani ya jengo jipya.
Kwa miaka sita iliyofuata hadi mwezi Juni mwaka huu, familia ya Panvalkars ilikataa kuondoka na kutatiza jitihada za kubomolewa kwa jengo hilo.
Familia ya Panvalkars iliishi kwenye jengo hilo kwa miaka 27Image copyrightANUSHREE FADNAVIS/INDUS IMAGES
Image captionFamilia ya Panvalkars iliishi kwenye jengo hilo kwa miaka 27
Mradi huo mpya ulikumbwa na changamoto zaidi na hata kushindwa kufuata sheria za ujenzi.
Mwaka 2013 aliachana na mradi huo.

No comments:

Post a Comment