Sunday, May 3, 2015

NJIA ZA KUMPATA MWEZI TOKA KWA MUNGU.

NJIA ZA KUMPATA MWEZI TOKA KWA  MUNGU. 
    Mtumishi wa Bwana. BARAKA J. OTIENO
Maandiko: Mwanzo 2: 7, 15, 18- 23; 29: 1-30 

Yaliyomo: 
01. Utangulizi

02. Chanzo cha ndoa

03. Kusudi la ndoa

04. Njia za kupata mume au mke sahihi ( chaguo lako )

05. Utajuaje huyu ni chaguo lako?

06. Mambo yanayovunja uhusiano

07. Mambo ya kuzingatia ili kumaliza safari ya mahusiano salama kwa ushindi 

01. UTANGULIZI 
Je, unazijua njia sahihi za kumpata mke au mume toka kwa Mungu?
Je, umewahi kupenda au kupendwa?

Basi fuatana nami katika mfululizo wa somo hili ili tujifunze kwa pamoja katika somo hili la mahusiano.
 02. CHANZO CHA NDOA ( MAHUSIANO KATI YA MUME NA MKE) 
Mwasisi wa ndoa ni Mungu mwenyewe. Tazama akawaambia, zaeni mkaongezeke, mkaijaze nchi na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Tazama Mwanzo 1:28, 2:18.
Kumbuka: Mke mwema hutoka kwa BWANA, Mithali 19: 14. 

03. KUSUDI LA NDOA 
Kusudi pekee la ndoa ni kuendeleza uumbaji (uzao). Tazama Mwanzo 1:26- 28, pamoja na ushirika na kusaidiana, Mwanzo 2: 18 – 25. Hivyo kusudi la ndoa ni uzao, ushirika na kusaidiana. 

04. NJIA ZA KUMPATA MKE AU MUME TOKA KWA BWANA. 
Njia ni mwongozo au dira inayomwongoza mtu kufika au kumaliza mwendo au safari yake. Kumbuka: 
Kila njia lazima iwe na masharti yake hivyo yakupasa kuifuata vizuri. 
Njia pekee ya kanisa au mwongozo wetu ni NENO la Mungu pekee ndio lenye mwongozo au njia ya kupata mke au mume toka kwa BWANA. 
Zifuatazo ni baadhi tu ya njia hizo: 

(i) Jipate kwanza wewe mwenyewe vizuri 
Hivyo kabla ya mwenzi wako anza kwanza kujipata wewe mwenyewe. Luka 1:80, 2:52. Kumbuka: 
Usiingie kwenye mahusiano kwa dhana ya kujaribu(test). Ndoa hatujaribu bali tunatenda. 
Tatizo lao wengi ni kimo au kiwango (ufahamu) sahihi wa taasisi ya ndoa. 
Uanaume ni kupenda. Mwanaume wa ukweli haishii pale wanapoishia wengi (wengine) – Be a man. Jambo jingine la msingi hapa ni kujitambua wewe ni nani. 

Angalizo: Wanaume (vijana) wote waone wazuri, pia wanawake (mabinti) wote waone wazuri, lakini usiwabinafsishe wote. Elewa kuwa; 
Wanaume wote ni waume, lakini siyo wote ni waume zako.
Wanawake wote ni wake, lakini siyo wote ni wake zako. 
Tembea ukijua kuwa wewe ni JIBU la mtu, hivyo tembea ukijua wewe ni mke au mume wa mtu. 

(ii) Usitafute mke au mume. 
Mwanzo 2:7, 15, 18-23, 1Petro 5:7 
Usijitaabishe/ usijihangaishe ni wapi utampatamke au mume, Mwachie Mungu akupe mke au mume kwani yeye ndiye mwasisi wa ndoa hivyo anajua ni yupi atakufaa katika maisha yako. Rejea kwa mzazi wetu wa kwanza Adamu; hakuhangaika kutafuta bali yelye alijikita kuilima na kuitunza bustani ya Edeni. Ndipo Mungu alipoona kuwa Adamu ana uwezo wa kuhimili ndoa, akampa Hawa kuwa mkewe. 

(iii) Maombi na shukrani 
Filipi 4:4-7 
Hupaswi kufanya mahusiano kabla ya kufanya maombi ili uone. 
Ukishamwona mwenzi wako hauhitaji kuomba wala kwenda kwa Mungu bali kwenda kwa Mchungaji ili kuendelea na mchakato wa kufikia hatma njema, Rum 8 24-25. 
Angalizo:
Kuna mambo ya kuomba na yapo mambo ya kutenda (wajibu).
( Prayer is not a substitute to your responsibilities) Maombi ni ishara ya kuhitaji msaada na imani ni kupokea kwa shukrani ulivyoomba. 
Kumbuka:
Mwenzi wako lazima maisha yake yakuguse, bila kujali hali, mazingira, elimu n.k. 

Mambo ya kuelewa katika mahusiano:

(a) - Ukimtamani mtu lazima utaanguka naye (kutenda dhambi)

- Ukimpenda mtu lazima utamjali 
(b) - Ukiwa mtu wa kuangalia au kuchunguza sana, lazima utabagua ( selective)

- Ukiwa mtu wa kutazama, lazima utapenda kwa kujali. 
Kumbuka:
Mahusiano yanaanza kwa kuta za mana, Mawnzo 2:18-23
Hakuna kupenda bila gharama, Mwanzo 29:1-30. 
Tujenge mahusiano ili tupate akili ya kujuana vizuri.
Lazima umjue mtu unaefanya naye mahusiano. 
Kuna msemo usemao: Ukishindwa kumpata umpendae, basi jitahidi kumpenda utakayempata. Jambo la msingi katika mahusiano ni kuweka mipaka

Usiwe na mazoea na maongezi au mazungumzo yasiyompa Mungu utukufu. 
(iv) Jitoe vema (kikamilifu) kwa ajili ya utumishi

Mwanzo 2:8, 15, 29:1-30
Endelea kuwa mwaminifu katika ibada na huduma na Mungu ajuaye haja za mioyo atakutendea mema.

Kumbuka:
Kijana au binti ukikataliwa usimchukie mwenzako na kumwona amepoa kiroho, bali mshukuru Mungu maana amekuponya na matatizo, janga au msiba. 
Zaidi, nenda kaongeze kimo/kiwango chako cha ibada na utumishi. Angalizo:
Kijana usijaribu kutongoza- yaani kumshawishi binti akubaliane na jambo asilolitaka, bali eleza ukweli wa maisha yako halisi.

Wapagani ndio wanaotongoza (danganya) kwa kujivika nafasi, vyeo na majina makubwa ya uongo ili wakubalike. 
Angalizo:
Usimwoe binti wala usiolewe kwa kigezo/msingi wa kumwonea huruma (kumhurumia) mtu; kwa madai ya kumpunguzia matatizo au kuondoa kero za kukufuatilia kila siku.

Hatuoi kwa kuhurumiana, bali kwa msingi wa kupendana na mapenzi ya Mungu.

Ni vyema kuweka vigezo, lakini uwe tayari kuyaruhusu mapenzi ya Mungu kuchukua nafasi ya kwanza, kwani ndiye anayemjua vizuri huyo mwenzi wako. Math 26:36-44. 
05. UTAJUAJE HUYU NDIYE CHAGUO LAKO.
Kitu pekee kitakachojulisha na kuamua kuwa huyu ndiye mwenzi na chaguo lako maishani ni ile Amani ya Mungu (Kristo) itaamua ndani yako.

Amani ya Kristo ni sauti ya Roho Mtakatifu kuthibitisha kuwa upo mahali sahihi, Filipi 4:7 
Kumbuka:
Mke hatuonyeshwi, bali tunaona waziwazi, kama ilivyokuwa kwa Adamu, Mwanzo 2:19-25

Japo wakati mwingine Mungu anaweza kukuonyesha au kusema nawe; ila uwe makini sana hapa kwani zipo sauti kama tatu ma ukishindwa kupambanua utaumia mbele za safari.

Sauti hizi ni:
Sauti ya Mungu
Sauti ya dhamiri (mimi)
Sauti ya shetani 
Angalizo/Onyo:
Usionjeshe/usifungulie chemchem.

Usianze mahusiano ya kimapenzi (sexual intercourse) kabla ya au nje ya ndoa. Hii itakuwa ni ishara ya kuwa msingi wa mahusiano au ndoa yenu siyo upendo bali tamaa tu.

Biblia inatutahadharisha kutoyachochea wala kuyaamsha mapenzi hata yatakapoona vema yenyewe, Wimbo 4:12, 2;7, 3;5

Hapa mapenzi yanafananishwa na chemichemi iliyofungwa, siku itakapofunguliwa itaendelea kutamani kufunguliwa kila siku hata utakapokuwa ndani ya ndoa, utasumbua sana.

Ukishaonja utaendelea kuonja na kuonjesha na hapo ndipo mwisho wa uthamani wako na heshima yako. Tafadhali jitunze, ili uimailize safari yako salama na kwa ushindi. 

06. MAMBO YANAYOVUNJA UHUSIANO.
Yapo mambo mengi, lakini haya baadhi yana mchango mkubwa:
(i) Maneno unayoyaongea/ yanayosemwa na watu wengine dhidi ya mwenzi wako.

(ii) Mwonekano wako:
Ni vizuri kijana ukawa msafi (smart) na siyo kuwa ovyo ovyo (rough)
Jifunze kuoga, kufua nguo zako, kujipaka mafuta, marashi n.k. 
(iii) Tabia ( haiba) ya asili ya mtu
Mithali 30:11-14.
Ni jambo jema hizi tabia za asili zikashughulikiwa mapema kabla ya ndoa, maana zinaweza kuleta shida ndani ya ndoa.

07. MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUMALIZA SAFARI YA MAHUSIANO HATA NDOA KWA USHINDI.
Mwenzi anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo ili kumaliza safari au mwendo wake salama:

(i) Uwe na kiasi (self control) yaani kuweka mipaka katika:

- Mazungumzo, 1 Kor 15:33

- Mazoea ya kijana na binti kuwa peke yao mafichoni.

- Usijirahisi eti kuonyesha unampenda mtu. ( uwe rahisi kuingilika na siyo kujirahisi). ( You can be simple, but don’t be cheap) 
(ii) Uwe na maono
Mithali 29:18
Mtu mwenye maono ana malengo, mipango na mikakati. Katika mambo yake hajiendeiendei ovyo.

Panga unataka kuishi maisha ya namna gani. 
(iii) Jaa Neno na Roho Mtakatifu
Luka 4:1-15

Hii itakusaidia kuzipinga hila za mwovu ( shetani) 
(iv) Kimbia/Ondoka maovuni
Mwanzo 39:5-23
Habari za Yusufu akikimbia pale alipotaka kubakwa na mke wa Potifa.
Usijifanye wa kiroho sana na kujiamini kupita Neno la Mungu (Biblia) 
Angalizo:
Wakati unapofanya jambo lisilo la kiroho kuwa la kiroho, utakuwa unasema uongo wa kiroho na kuzuia isionekane ile maana halisi ya Neno la Mungu. 
(v) Fanya maombi ya kufunga
Dawa ya mwili ni kuunyima chakula, Galatia 5:16-21, Luka 18:1-7.
Tiba ya magonjwa hayo ni kufunga ( kutoupa mwili chakula) 

UISHI MILELE 

2KOR 13:14 

No comments:

Post a Comment