Friday, April 15, 2016

AFYA WIKII HII. Je waijua fangasi ya sehemu za siri.

AFYA WIKII HII. Je waijua fangasi ya sehemu za siri.

UGONJWA WA FANGASI
SEHEMU ZA SIRI (VAGINAL
CANDIDIASIS)
Ugonjwa huu husababishwa
na wadudu wanaoitwa
candida na kawaida kila
mwanamke anakuwa na jamii ya fangasi sehemu zake za siri
na wadudu hao huwa
wanamlinda mwanamke ili asishambuliwe na wadudu wengine.
Inapotokea wale wadudu wanaomlinda kuwa wengi sana ukeni badala ya kulinda mwili hugeuka na kuanza kushambulia na mwisho dalili hujitokeza na ndipo hapo tiba huwa inahitajika haraka sana ili kuzuia madhara mengine.
Kuna baadhi ya sababu
zinazosababisha fangasi
kutokea ukeni na sababu hizo ni kama ifuatavyo:
Kutumia dawa za antibayotiki mara kwa mara na kwa muda
mrefu, husababisha fangasi kwani dawa hizo huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha uke ukiwa
hauna kinga. Dawa za antibayotiki ni kama,
Ampicillini, Amoxylline,
Ciproflaxine, Doxylline,
Erythromycine, Gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi,
jamii isitumie ovyo dawa za antibayotiki bila ushauri wa daktari.Sababu nyingine ni unene
kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwa
sababu unene husababisha jasho sehemu za siri na
kuongeza unyevunyevu
sehemu hizo pia michubuko kutokana na kubanwa na nguo ya ndani. Sababu zingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama Prednisoline, Hydrocortisone Dexameltasone na nyingine nyingi.
Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi
kuzaliana kwa wingi.
Pia kuna magonjwa
yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari,
Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza
kinga ya mwili na kusababisha magonjwa nyemelezi.
Kuwepo na joto kupita kiasi
na kuvaa nguo za ndani
ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu
za siri.
Sababu ni nyingi na hatuwezi
kuzitaja zote. Dalili Dalili hutofautiana kutokana
na mtu na mwingine ila dalili
kubwa ni kutokwa na
majimaji meupe wakati
mwingine kama mgando
wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muasho
sehemu za ndani au kwenye
mashavu ya sehemu za nje za
siri.
Nje ya sehemu hizi za siri
hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa
au wakati wa tendo la ndoa.
Pia mgonjwa atajikuta
akikojoa mara kwa mara. Tiba na ushauri Fangasi hutibika vizuri na
kupona ila ni vizuri ukaenda
hospitali na kufanyiwa kipimo
cha mkojo ambapo
chembechembe za yeast
huonwa vizuri kwenye darubini.
Daktari akigundua una
maradhi haya ataweza kukupa
dawa zenye uhakika.
Usinunue dawa hovyo na
kutumia utasababisha usugu wa fangasi, hivyo kutopona.

No comments:

Post a Comment