Kunguni sasa ni sugu kwa dawa
- Saa moja iliyopita
Huenda kunguni wakawa sugu kwa dawa, hali ambayo itasababisha wadudu hao kuwa na uwezo kuhimili makali ya dawa ya kuua wadudu.
Idadi ya watu inayozidi kuongezeka na safari za kimataifa zimesadia mdudu huyo kuwa kero kwenye mahoteli kote duniani.Dawa za kuua wadudu ndizo hutumiwa kwa wingi kuua kunguni lakini kwa haraka waduduhao wamekuwa sugu kwa dawa.
Kumuua kunguni sugu inaweza kuhitaji dawa yenye makali mara elfu moja zaidi ya ile inayohitajika kuua wadudu wasio sugu.
Wadudu hao wamesambaa kwenda manyumbani na ofisini na hii imekuwa vigumu kuwaangamiza mara wanapoingia.
Wanaweza kuishi hadi mwaka mmoja bila kula, na yai moja la kunguni linaweza kuzaa kunguni wengi mno.
Kama wadudu wengine kunguni wamefunikwa na ngozi inayojuliana kama cuticle.
David Lilly kutoka chuo cha Sydeny na wanzake walilinganisha unene wa ngozi kutoka kwa kunguni walio sugu kwa dawa na ngozi ya wale wadudu wanaokufa kwa haraka kutokana na dawa.
Matokeo yalionyesha kuwa ikiwa ngozi ni nene kunguni anaweza kuwa sugu kwa dawa.
No comments:
Post a Comment