Friday, April 15, 2016

UHURU WA KUABUDU

UHURU WA KUABUDU

UHURU WA IBADA/ IMANI/ DINI NA KUABUDU KWA VIJANA WA TAASISI ZA ELIMU NA RAIA KAMA ULIVYOBAINISHWA KATIKA KATIBA MAMA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Ambassador’s Congress 25th Dec 2010- Y.I. Juma

KUSUDI LA SOMO:

    Kusaidia vijana wetu wa kanisa kujenga uimara wa imani yao kwa Mungu, Ujasiri wa mahusiano yao na Mungu katika hali zote za maisha, kazini, Biashara, Taasisi za elimu na mtandao mzima wa shughuli za maisha zinazoweza kuathiri mahusiano yao ya ki-imani na kuwalazimisha kufanya kazi/ Kusoma/ kufanya biashara au burudani na michezo isiyo na maadili siku ya sabato au kinyume cha imani yao kwa ujuzi wa kuielewa sheria ya nchi na sauti ya Mungu Math 22:21-22, Warumi 13:1-8, 1Petro 2:13-17
    Kuwasaidia vijana wa kanisa kusimama imara katika imani kwa zamu yao bila tegemezi la mtu yoyote, awe mchungaji , mzazi au kanisa. Imani aliyoielewa aisimamie kwa dhati hata katikati ya moto. Daniel 3:16-18

UJUZI WA KISHERIA NA WA-KIIMANI KATIKA KULINDA IMANI YA VIJANA WA KANISA

1. Ni heri kumtii Mungu kuliko Mwanadamu- Matendo 5: 29

2. Jua haki ya Kikatiba na Sheria ya nchi ya kila raia katika swala zima la kuabudu na kushiriki shughuli za Ki-imani.

3. Jua wajibu wako katika kujihusisha na mambo ya imani na ibada

4. Jua nini cha kufanya haki yako ya ibada/imani inapokiukwa makusudi na mamlaka iliyo chini yako.

5. Jua hatua za kisheria na za-kinidhamu zitakazochukuliwa dhidi yako kwa kukiuka wajibu wako katika maswala ya imani.

DONDOO NA NUKUU ZA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA MASWALA YA IMANI NA IBADA

    ‘Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchunguzi katika mambo ya dini’ Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6[1]
    Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi; na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za Mamlaka ya nchi. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6
    Kila palipotajwa neno “ dini” katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6
    Kila raia anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomhusu yeye, maisha yake au yanayohusu Taifa. Uhuru wa Kushiriki shughuli za umma: sheria ya 1984 Number 15, ib. 6

VIJANA WA KANISA NA TAASISI ZA ELIMU NA WAJIBU WAO KATIKA KUTII SHERIA ZA NCHI

Wajibu huu ni kwa mujibu wa katiba kipengele cha “ Wajibu wa kutii Sheria za nchi:

Sheria ya 1984 Na. 15, ib. 6

    Ni wajibu wa kisheria na agizo la Mungu vijana kufanya kazi halali za mapato au za jamii bila kuvunja sheria ya nchi na Sheria ya Mungu.
    Ni wajibu wa Kisheria na agizo la Mungu kutii sheria halali za nchi bila kumkosea Mungu.
    Ni wajibu wa Kisheria kulinda mali za umma na kuepuka hali zote za machafuko na kualifu amani ya jamii kwa nia ya kuhujumu mali za umma unazozitumia.
    Ni wajibu wa Kisheria kulinda na kusimamia ulinzi na usalama wa raia katika mambo yote, likiwapo swala la ibada.

No comments:

Post a Comment