Friday, April 15, 2016

JE, UNAFAHAMU MTU WA KWANZA KUGUNDUA "GYM" ALIKUWA MUADVENTISTA MSABATO?

 Ni daktari Mmarekani na muadventista msabato John Harvey Kellogg aliyezaliwa tarehe 26/02/1852 huko Tyrone Michigan na alifariki tarehe 14/12/1943 akiwa na umri wa miaka 91 huko Battle Creek, Michigan. Alipata elimu yake katika chuo kikuu cha New York katika hospitali ya Bellevue.
Alioa mwaka 1879 mwanamke aitwae Ella Ervilla Eaton (1853–1920) na kwa pamoja hawakubahatika kupata mtoto wa kuzaa ila kwa pamoja walifanikiwa kulea watoto 42 na kati yao waliwalea watoto 8 kisheria kama watoto wao wa kuzaa kabla Ella hajafariki mwaka 1920.
Dkt. John aliamini tiba ya mwanadamu kupitia vyakula asili, mbogamboga na mazoezi huku akipinga vikali matumizi ya pombe na tumbaku.
Dkt. John Harvey Kellogg

Baadhi ya maelezo katika nyumba yake ya makumbusho

Baadhi ya vifaa vya mazoezi alivyogundua kwa ajili ya afya ya mwanadamu

Maelezo yakionesha idadi ya huduma alizawahi kutoa enzi za uhai wake duniani kote

Kifaa cha mazoezi alichogundua dkt. John

Moja ya maelezo kumuhusu yaliyopo katika nyumba ya makumbusho

Picha ikionesha vifaa vyake vya mazoezi

Maelezo ya matumizi ya kifaa cha mazoezi

Maelezo kuhusu nyuma yake ya mazoezi na aina ya tiba yake. Taarifa kwa msaada wa http://en.wikipedia.org/wiki/File:John_Harvey_Kellogg. na Amusir Solutins

No comments:

Post a Comment