BIBLIA NA MIFANO YA WATU WALIOSIMAMIA IMARA IMANI ZAO BILA KUVUNJA SHeRIA YA NCHI WALA SHERIA YA MUNGU
YUSUFU- Mzo 39:9-11 “ Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe” Sheria ya Misri ya Mahusiano ya ndoa na sheria ya Mungu Kutoka 20:14 ‘Nifanyeje ubaya nimkose Mungu’
ESTER- Esta 4:16 “ Nitaingia kwa mfalme, Kinyume cha Sheria; nami nikiangamia, na niangamie” Sheria ya Wa-Amedi na Waajemi isiyobadilika”
Daniel- Dan 6:4-5, 8, 10, 16 : Sasa ee mfalme piga marufuku, ukatie sahihi maandiko haya, yasibadilike, kama ilivyo sheria ya Waamedi na Waajemi. Daniel akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.
Shadraka, meshaki abednego- Dan 3:16, Dan 3:18 “ Bali kama si hivyo, ujue Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Paul: Matendo 22:25- Je ni halali ninyi kumpiga mtu aliye mrumi naye hajahukumiwa bado? Sheria za Rumi
Yesu: Mathayo 10:17-20 “ Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka mabarazani, na katika masinagogi yao watawapiga. Nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa, Msifikiri-fikiri jinsi ya kusema, mtapewa saa ile ile mtakavyosema kwa kuwa Roho atawaongoza kunena
No comments:
Post a Comment