Tuesday, June 16, 2015

MSEVENI WA UGANDA KUCHIMA VIJEMBE

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameijibu video ya waziri mkuu na katibu mkuu wa zamani Amama Mbabazi. Katika tangazo lake, ambalo lilitokeza kwenye mtandao wa YouTube jana alfajiri, Mbabazi anashtumu kuwepo udhaifu katika chama, na utawala wa NRM, na ni kwa sababu hio anataka kuwania uwenyekiti wa chama hicho, na kisha urais katika uchaguzi mkuu mapema 2016. Rais Museveni, katika video yake iliochapishwa jana usiku, amempiga vijembe Mbambazi na kumkosoa kwa kuharakisha kampeni za uchaguzi kabla ya wakati, na kumshauri Mbabazi asipoteze muda wake. Rais Museveni amesema alijuzwa jana, uamuzi wa Mbabazi kujitangaza kuwa mgombea wa uwenyekiti na urais. Hayo alisema ni maamuzi ya Mbabazi, kwani si chama wala tume ya uchaguzi ya taifa, wametangaza tarehe za uchaguzi: '' Sidhani, kwa hiyo, inastahiki kwa Mheshimiwa Mbabazi kupoteza wakati wako na ufanyaji huo wa kampeni njiti''. Museveni alivunja moja, moja, hoja za Mbabazi katika video yake ya jana. Kuanzia kule kumtumikia kila mtu nchini, elimu kwa wote, hoja ya kuifufua NRM, kanuni za demokrasi, na kukariri maendeleo yaliopatikana kwa usalama, na hadhi ya taifa ughaibuni. Ingawaje, Museveni akaongeza, Mbabazi anasema pia, nchi imechoka, kuuguza taifa . Aliyekuwa Waziri mkuu wa Uganda Amama mbabazi ametangaza nia ya kuwania Urais mwakani ''Ni Vyema, Mbabazi yu katikati ya mfumo wetu miaka yote hii.'' ''Alikuwa katika mashirika ya usalama, amekuwa bungeni alikuwa waziri wa usalama kwa muda mrefu, alikuwa katibu mkuu wa chama; na hatimaye alikuwa waziri mkuu.'' ''Sasa huo udhaifu uliopo, ambao ni mimi ambaye daima naukosoa, kwa mfano, ada za shule, licha ya kuwepo kisomo cha bure kwa watoto wote (UPE).'' ''Huu ni uchovu ambao ungesimamiwa na Waziri Mkuu na viongozi wengine, ''Hoja ya kuchoka – baadhi ya sekta ambazo zimechoka''. Hoja ya ufisadi, na nyenginezo ambayo nauelewa vyema na daima kuzizungumzia .'' ''Kuhusu chama cha NRM, Kweli NRM hakijaandaliwa inavyopasa, lakini Mbabazi alikuwa katibu mkuu wetu kwa karibu miaka 10, na ni kwa ajili hio nilitwaa hatua kuirekebisha katiba ya chama na tunaye katibu mkuu wa kudumu.'' ''Museveni alihitimisha kwa kusema hoja zake Mbabazi ni rahisi kujibiwa kwa sababu ikiwa kuna mtu yeyote wa kusailiwa kuhusu uchovu huo Mbabazi ni mmoja wao, hawezi kujiosha mikono nayo.''

No comments:

Post a Comment