Tuesday, June 16, 2015

ZITTO KUZUNGUMZIA TAARIFA YA CAG

Tamko la Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndg.
Zitto Kabwe kuhusu Ripoti ya CAG mwaka 2013/2014
1) Taarifa nyingine ya CAG imetoka, kwa mujibu wa Katiba
ya JMT na kwa mujibu wa sheria za nchi. Taarifa hii
imechelewa kutolewa kulingana na mabadiliko ya Ratiba za
Bunge ambapo hapo awali taarifa ilikuwa ikitoka mwezi
Aprili na kuwezesha kuchangia katika mchakato wa Bajeti
ya nchi. Taarifa ya mwaka huu na ile ya mwaka Jana
imetoka wakati wa Bunge la Bajeti na hivyo Bajeti ya
Serikali haijazingatia hoja za ukaguzi ili kuboresha mfumo
wa matumizi ya fedha za umma. Ni vema utaratibu wa
zamani wa ripoti kutolewa mwezi Aprili urejewe ili
wabunge waweze kutumia ripoti hizo wakati wa kamati
katika kujadili makadirio ya Bajeti za Wizara mbalimbali.
2) Taarifa kama miaka iliyopita bado sio nzuri. Mapato
mengi ya Serikali bado yanapotea. Uk. 53 wa Taarifa
unaonyesha kuwa mizigo inayoingizwa nchini kupita
kwenda nchi jirani zinazotumia bandari zetu hubakia nchini
na kuingizwa sokoni hivyo kukwepa kodi. Mwaka
2013/2014 mizigo ya transit iliyobaki nchini kiudanganyifu
ilikuwa zaidi ya bidhaa 6000 kwa mujibu wa Taarifa ya
CAG. Hivyo kodi ya tshs 836 bilioni haikulipwa kwa mizigo
hiyo sawa sawa na 10% ya makusanyo yote ya kodi za
ndani. Tshs 836 bilioni ilipotea mwaka 2013/14 peke yake.
Wakati hili linatokea Serikali ipo ukata mkubwa na
kushindwa kuendesha miradi yake mbalimbali. Fedha
iliyokwepwa idara ya forodha peke yake inalipa Madeni
yote ya wakandarasi wa barabara wanaoidai TANROADS
na riba kulimbikizwa kila mwaka. Fedha hii ingelipa Madeni
yote ya mfuko wa PSPF wanayoidai Serikali. Fedha hizi
zingeweza kulipia miradi 2 mikubwa nchini ya BVR na
vitambulisho vya Taifa ambayo inasuasua kutokana na
ukata.
Natoa wito kwa CAG kwanza kuweka wazi orodha ya
bidhaa hizo zilizobakia nchini na kuingizwa nchini bila
kulipa kodi. Vile vile CAG aweke wazi wafanyabiashara
wote walioagiza bidhaa hizi na vyombo vya kiuchunguzi
vichukue hatua za kuwashtaki wafanya biashara hawa
mara moja.
Natoa wito kwa Kamati ya Bunge ya PAC kuwaita mara
moja maafisa wa TRA kujieleza mbele ya kamati kuhusu
suala hili na kuandaa taarifa maalumu bungeni ili kuanika
uoza huu unaopoteza mapato mengi sana ya Serikali.
3 ) CAG kaonyesha kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana
kitengo cha maafa cha ofisi ya Waziri Mkuu ambapo tshs
163 billioni za chakula cha maafa hazikukusanywa katika
kipindi cha miaka 5 iliyopita. Huu ni kama mrija wenye
wastani wa tshs 32 bilioni kuchotwa kwa kisingizio cha
chakula cha maafa kwa wananchi. Kwa malezo ya CAG ni
kwamba Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wamekula
fedha za chakula cha misaada. Maana hakuna uthibitisho
wa kuwa mahindi yaliyogawanywa na taarifa kutolewa na
Wakala wa Akiba ya Chakula (NFRA). Kitengo cha maafa
ofisi ya PM kimekuwa mrija wa wizi wa fedha za umma,
wizi ambao umekuwa ukifanyika bila ya kugunduliwa kwa
miaka 5 sasa. ACT Wazalendo inaisihi Kamati ya Bunge ya
PAC kufanya uchunguzi maalumu kwenye kashfa hii ya
tshs 163 bilioni katika Ofisi ya Waziri Mkuu na Wakala wa
Hifadhi ya Chakula ( NFRA).
4) ACT Wazalendo inalitaka Bunge kuchukua stahiki dhidi
ya Wizara ya Ujenzi kufuatia ripoti ya CAG kuonyesha kuwa
Wizara ilidanganya Bunge katika kupitisha Bajeti ya tshs
252 bilioni ambapo kati yake tshs 87 bilioni ziliibiwa au
matumizi yake kutoeleweka.
5) ACT Wazalendo inampongeza CAG kwa kuendelea na
zoezi la kisheria la kukagua mahesabu ya vyama vya siasa.
Hii inaweka misingi ya uwajibikaji kuanzia kwenye vyama
vya siasa, taasisi muhimu sana katika ujenzi wa
demokrasia. Vyama vya siasa vichukulie ripoti ya CAG
kama changamoto ya kutoa kwanza kibanzi kwenye
macho yao ili kuwa na ‘ moral standing’ ya kupambana
dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma nchini.
Zitto Kabwe
Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo

No comments:

Post a Comment