Tuesday, July 5, 2016

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA ZANZIBAR.........


AZ1Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba,alipowakumbusha  majukumu yao na kuwataka wafanye  kazi sheria na taratibi kwa kazi iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
AZ2Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba,alipowakumbusha  majukumu yao na kuwataka wafanye  kazi sheria na taratibi kwa kazi iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016
AZ3
Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakiwa katika mkutano uliofanywa  na Rais kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambao mkutano huo umewataka  wakuu hao kutekeleza majukumu yao kama sheria za Utumishi zinavyoeleza na sio kufanya kazi kwa  mazoea,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
AZ4Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kukumbushwa majukumu yao katika  maeneo yao kazi,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.

TIGO, MILVIK KUSHIRIKIANA KUTOA BIMA WATAKAYOIMUDU WATANZANIA

Meneja wa Milvik nchini, Tom Chaplin(wa pili kushoto),akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuanzisha huduma  mpya ya Bima iliyoboreshwa ya Bima Mkononi. Wengine kwenye picha Mkuu wa huduma  za Fedha Tigo Afrika), Ruan Swanepoel(wa pili kulia), Meneja wa promosheni  Tigo pesa,Mary Ruta (kushoto) na  Kulia ni Meneja wa maendeleo ya Biashara Resolution Insurance,Zamaradi Mbega.
Dar es Salaam  Julai 4, 2016- Tigo Tanzania itashirikiana na na Milviki Tanzania  na kampuni ya bima ya Resolution kuanzisha huduma  mpya ya Bima iliyoboreshwa  ikijulikana Bima Mkononi. Tigo imekuwa ikitoa huduma  kama hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita  kwa wateja wake zaidi ya 500,000 kupitia Tigo Bima.
Huduma ya Bima Mkononi inatoka huduma ya kipekee  kama vile bima ya maisha, ugonjwana ajali kwa mtu binafsi kwawateja ambao wanaotumia huduma ya Tigo Pesa.
AAkitangaza kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin alisema, “Huduma hii itasaidia kuziba pengo  kati ya wateja  na hivyo kuongeza  upenyezaji wa huduma hiyo kwa njia ya simu katika maeneo yaq mjini na vijijini nchini Tanzania, tunaamini Bima Mkononi  itakuwa ni kicdhocheo kikubwa  cha kusukuma ujumuishwaji wa  huduma za fedha  katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania kuzifikia huduma za bima  wanazozimudu kutoka kwenye simu zao.”  
Chaplain aliongeza, “Tunawaomba Watanzania  ambao  hawajaweza kuzifikia  huduma za afya ambao wanazimudu  ao  bima ya kawaida ya afya  kuanza kutumia huduma hii  kwa sababu  inatoa ulinzi dhidi ya majanga ya kifedha  na afya duni kwao na familia zao.”  
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Kuzinduliwa kwa huduma hii  kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuboresha mageuzo katika mfumo wa maisha ya kidijitali na katika kuongoza kwake  katika kutoa teknolojia ya kisasa  na ubunifu  kwa kuwezesha huduma ya Bima Mkononi kufikiwa kupitia Tigo Pesa.”
Aliongeza, “Huduma hii mpya  itakuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo  kuipata huduma ya bima kwa urahisi  kwa sababu huduma ya Bima Mkononi  inalenga kuwapatia Watanzania  njia mbadala  kwa bima za afya na maisha.”
Aliipongeza Milvik  kwa ushirikiano wake  na kuahidi kuwa Tigo imelenga  kuendelsa  kuunga mkono  kupitia huduma ya Tigo Pesa.
Hivi karibuni Tigo ilizindua  kampeni mpya   ya NITIGOPESA ambapo wateja kutoka mitandao yote  ya simu  wanaweza kupata huduma za  kifedha kutoka kwa wateja na wafanyabiashara kote nchini.

No comments:

Post a Comment