BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA TTB YAFANYA MKUTANO KWA MARA YA KWANZA
Bodi ya Wakurugenzi wa TTB. Kutoka kushoto ni Bw. Agustine Kungu H. Olal, Bw. Mark Leveri, Bibi Zubein Mahita, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (Mwenyekiti), Bi Devota Mdachi (Katibu), Bw. Ibrahimu Mussa na Balozi Josiph Sokine
Bw. Ibrahimu Mussa (katikati) mmoja kati ya wajumbe wa TTB akiongea wakati wa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi huku wajumbe wenzake Bibi Zubein Mhita (kulia) na Bw. Agustine Kingu H. Olal (kushoto) wakimsikiliza kwa makini.
Mkuu wa Kitengo cha IT cha TTB bw. Rossan Mduma (wa kwanza kulia) akiwaelezea wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi namna tovuti maalumu ya TTB (Portal) inavyofanyakazi na inavyoweza kutumiwa na wadau mbalimbali wa Utalii.
…………………………………………………………………………………………………
Na: Geofrey Tengeneza
Bodi mpya ya Wakurugenzi wa TTB iliyoteuliwa hivi karibuni imekutana leo katika ofisi za TTB jijini Dar es salaam katika mkutano wake wa kwanza toka iingie madarakani.
Mkutano huo ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya wajumbe wa Bodi hiyo kufahamu zaidi kazi na majukumu ya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB) ulifanyika chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na kuhudhuriwa pia na Menejimenti ya TTB.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi alitumia pia mkutano huo kuwatambulisha wajumbe wa Menejimenti ya TTB kwa Mwenyekiti na Wakurugenzi hao wa Bodi. Bodi ya wakurugenzi iliyoteuliwa mwezi Mei mwaka huu ina wajumbe sita ambao ni Bw. Ibrahimu Mussa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA; Balozi Joseiph Sokoine , Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda; Bw. Mark Leveri, Mtaalamu wa filamu na matangazo.
Wengine ni Bw. Richard Rugimbana, Bw. Richard Rugimbana, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Bibi Zubein Muhaji Mhita, Bibi Zabein Muhaji Mhita, Mbunge Mstaafu na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi Msataafu na Bw. Agustine Kungu H. Olal, Kamishna Msaidizi wa Sera na Uchumi, Wizara ya fedha na Mipango. Mjumbe mwingine ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi.
Mwenyekiti na Wajumbe hao wa Bodi ya Wakurungenzi wa TTB watakuwa madarakani kwa miaka mitatu kuanzia tarehe 24/04/2016 hadi tarehe 23/04/2019 .
No comments:
Post a Comment