MAANA HALISI YA 666. Nimaka toka roryamaendeleo Blog.
Wapendwa!
Tarehe ambayo 666 Ilikuwa ubaoni ....
Sehemu
hii ndogo kuhusiana na nambari 666 nimeitoa kwenye, sura moja ndani ya kitabu kinacho kwenda kwa
jina la “FREEMASON; Dunia usiyo ifahamu”,
.... Kwa watafiti huru wa mambo ya UFO na
New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia debe taarifa hizo kwa
lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake atakuwa na ‘damu
takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.
Mmoja
anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali duniani,
ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu
na Ukristo na
bila kusahau kwenye imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons.
Hiyo ni 666 katika lugha yake ya asili ...
Wote
wanasubiri juu ya kuja kwa Messiah, ambaye atakaye kuja kuuokoa ulimwengu.
Kutokana na mafunzo na falsafa za kimasonia ni kuwa Masiha wa kwanza, yaani
Yesu alikuja kwa ajili ya kusimamisha ufalme wa mbinguni, lakini Masiha wa mara
ya pili ambaye ni …? Atakuja kuisimamisha New World
Order chini ya
utawala wake.
Kuhusiana
na Masiha huyo, Freemasons wa daraja la 33 Manly P.
Hall, katika kitabu chake cha “The Secret Destiny of America ameandika
hivi,
“Jawabu la mpango huu wa siri ni World Order chini ya mfalme mwenye
nguvu za kimaajabu. Mfalme huyu anatokana na ukoo wa wenye damu tukufu; hii ni
kusema, anatokea kwenye asasi ya Illuminati na walio na hekima, anatokana na
familia ya mashujaa ya binadamu walio wakamilifu”
Mtu
aliyetajwa na Hall sote tunamjua ni nani, ametajwa vizuri kwenye vitabu
vitakatifu, hasa kwenye mafundisho ya Kiislamu. Wasomi na watafiti huru dini zote watakubaliana na mimi kwamba hakuna
dini iliyo weza kuelezea vyema maisha yatakayo kuja na alama zake, maisha ya
kaburi na maisha ya motoni na peponi kama Uislamu, na mtu huyu ametajwa vilivyo
na alama zake mbalimbali katika mafunzo hayo ya Uislamu.
...
.... vurugu za New Age, lakini kwa kiasi fulani vurugu hizi zinawiana na yule
mmoja anaye ngojewa, tumchambue kidogo kwa mustakabali wa sura hii (Sura hii
kwenye kitabu hicho nimeipatia jina la: Wageni Wanarudi Tena ...) Tukianza na kitabu cha Ufunuo kwenye biblia tunakutana na
habari maarufu sana ya ‘mnyama’ kama ifuatavyo.
“Anataka
kila mmoja – mkubwa na mdogo, tajiri na maskini, mtumwa na aliye huru wapewe
chapa kwenye mkono wa kulia au katika paji la uso. Hakuna atakaye nunua au
kuuza chochote pasipokuwa na chapa, ambayo ni jina la mnyama au ile namba
inayowakilisha jina lake. Inahitaji hekima kufahamu mambo haya. Yeye aliye na
ufahamu na aihesabu namba ya mnyama huyo, kwa kuwa ni namba ya kibinadamu.
Namba yake ni 666” .
Mbali
na kuwa na tafsiri mbalimbali juu ya mnyama huyo ni nani na anawakilisha nini
kwenye maelezo hayo hapo juu, watu wengi wame chukuliwa sana na maneno ya
mwisho ya kipengele hicho, yaani 666. Lakini mbali na hilo dunia ya leo tunaona
ni namna gani ilivyo mezwa na vitu mbalimbali kutoka, alama na nembo, mpaka
majina na herufi za 666. Nami pia sitajikita katika kutaka kufahamu pembe au
kichwa au kinywa cha mnyama huyo kinawakilisha kitu gani ila nitakwenda moja
kwa moja kwenye jina lake nalo ni 666.
Wakati
nilipo kuwa nasoma hadithi za Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) kuhusu
Dajjal na vitimbi vyake nilikuwa nashangaa kwa nini Mtume (Rehema na amani ziwe
juu yake) amekuwa akituonya mara kwa mara juu yake, wakati ameshatuambia muda
mrefu kuhusu alama zake ambazo itakuwa ni rahisi kwetu sisi kumtambua na
kumkana, Mpaka nilipokuja kufahamu Freemasons ni nani na wanafanya nini ndipo
nikafahamu kuwa ni kweli Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuwa na haja
ya kutuonya sana juu ya mtu huyo. Wanao muandalia kiti chake cha Utawala wa
Dunia tayari wameshatufunga kwenye minyororo yake hata kabla ya Dajjal mwenyewe
hajafika itakuwaje ndugu yangu Dajjal mwenyewe atakapo kuja?
666 ---- Kwa Wagiriki wa zamani wakati kila namba ilikuwa ni sawa na
herufi, namba 6=W, yaani namba sita inachukuliwa ni sawa na herufi W. www kwenye
mtandao wa internet, ingeweza kuwa W, au WW lakini mtu fulani akachagua iwe WWW yaani 666! Hivyo
ufunguo wa tovuti yoyote ni 666! Yaani badala ya kuanza na jina la Mola Wetu mtukufu kama
inavyo paswa watu Fulani wanataka tuanze na jina la ‘mnyama’, 666.
Sarafu
ya Ulaya Euro ina Nyota 6 upande wa chini, na Nyota 6 upande wa juu na mistari 6 inayounganisha nyota hizo, hivyo kutengeneza jina la mnyama, 666!
Bar Code ya bidhaa zote za duniani ambazo zitauzwa nje ya mpaka wa nchi
husika lazima ziwe na namba 666, iko hivi, mistari mingi, mingi unayoiona katika Bar Code hizo, mistari
hiyo huwakilisha namba, nayo nambari sita (6) huwakilishwa na ‘bars’ au mistari miwili mirefu kushinda mingine, daima
utaiona mistari hiyo mwanzo kabisa, katikati na mwisho mwa Bar Code, wakati
mwingine utaona wame kuandikia nambari sita (6) chini ya
‘bars’ hizo mbili au wakati mwingine hawaandiki chochote, lakini lazima
utaitambua tu, kwa vile yenyewe ni mirefu kupita mistari mingine, huenda hata
kwenye kitabu hichi unacho soma ukaiona, au tizama bidhaa yoyote kutoka nje ya
nchi yako, au inayo uzwa nje ya nchi yako na utaiona. Namba ya kwanza daima ni 6, namba ya
katikati ni 6 na namba ya mwisho ni 6 vilevile, jina la ‘mnyama’ yaani 666.
Bar Code mpya ya Urusi kwa ajili ya kufuatilia watu wake ni 666,hii ni sawa
na microchip (somo kuhusu mikrochip nitaliposti wakati mwingine).
Bunge
la Ulaya lina viti 679, kila kiti kimoja ni kwa ajili ya mtunga sharia mmoja,
mathalani kiti namba 663 ni kwa ajili ya Rep Souchet, 664 kwa ajili ya Thomas-Mauro,
665 kwa ajili ya Zizzner na kiti namba
667 kwa ajili ya Rep Cappato. Wakati siti hizo zikiwa na majina ya wanachama
wanao vikalia, kiti kimoja hakina jina la mwanachama anaye kikalia, na pia
vilevile hakikaliwi na yoyote, kiti hicho ni namba 666.
Haswa
kiti hicho ni kwa ajili ya mmoja anaye ngojewa, ambaye bado kufika, lakini
nafasi yake ipo tayari inamsubiri. Ni kama muhuri wa Marekani ‘The Great Seal’ wenye nembo ya
jicho moja na piramidi ambalo halijakamilika, muhuri huu nao unasemekana unamsubiri
mmoja anaye ngojewa ambaye mpaka sasa tunamjua kama mnyama mwenye jina la 666!
Nembo
ya Umoja wa Ulaya ni ngao ya mwanamke aliyepanda mnyama! Mwanamke
huyu naye ametajwa kwenye kitabu cha ufunuo.
“Kisha,
Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi
juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya
makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”
Lakini
tukiachana na Umoja wa Ulaya, sehemu nyingi duniani, makampuni, wasanii wafanya
biashara, wanasiasa na hata viongozi wa kidini kwa namna mbalimbali wamekuwa
wakiipeperusha alama na nembo hii ya 666 kwa kila mtu kuona, na mazingira hayakuonesha kama vitu hivyo
vimefanywa kwa bahati mbaya tu, bali kwa makusudi mazima.
Lakini
ni nini hasa maana ya jina hili 666? Je tunaweza kumjua mmoja anaye ngojewa kwa kutumia jina hilo?
Wakristo wengi wanafahamu kuwa 666 ni alama ya Mpinga
Kristo ambaye Waislam wanamuita Masih
Dajjal. Katika moja
ya hadithi za mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) inasema. Hata kama ataleta
machafuko makubwa, neno Kafir litakuwa wazi limeandikwa katikati ya macho yake
(ana macho mawili ila moja ni chongo halioni
ndiyo maana mara nyingi anajulikana kama mwenye jicho moja), maelezo mengine yanasema neno hilo litaandikwa ‘Kaf’, ‘Fa’, ‘Ra’ kwa uwazi kabisa
ili kila mtu aone.
“Hakuna
nabii aliyetumwa isipokuwa aliwaonya watu wake kuhusiana na muongo mwenye jicho
moja. Yeye ana jicho moja, lakini Mola wako si mwenye jicho moja, na baina ya
macho yake pata andikwa ‘kaafir.”
Kwenye
Lugha ya Kiarabu herufi zilizo tajwa hapo ziko hivi; ر ف ق Kama tutazigeuza herufi hizo chini juu tutapata kitu
kinachofanana na 666. Lakini kutokana na mafunzo ya mtume (Rehma na Amani ziwe juu
yake) herufi hizo zitaonekana kama zinavyo tamkwa kwenye lugha ya Kiarabu.
Wasomaji
waelewe kwamba alama/namba 666 inatokana na tafsiri ya namba za Kigiriki kuja kwenye lugha ya
kingereza nazo zinawakilisha jina la mtu ambaye wengi wanamuita Mpinga Kristo.
Kwa hiyo tukiangalia kwa undani tunaona kuna majina mawili hapo, jina la Kristo na kuna jina
la Mpinga Kristo. Jina hili Kristo
Kigiriki ni Christos ambapo katika maandishi ya Kigiriki lingeandikwa hivi Χ ξ ς, ambapo kwa
Wagiriki namba zilitumika badala ya herufi, jina hilo lilisomeka hivi ,yaani (Chi, Xi na Sigma) kwa
hiyo (chi) = 600 nayo ni
herufi ya kwanza ya jina lake. (xi)= 60 inawakilisha
nyoka na ni mfano wa herufi ‘E’ na (sigma) = 6 herufi ya
mwisho ya jina lake, na ambapo jumla yake tunapata ni 666 kama
ilivyoelezewa kwenye ufunuo 13:18 Namba hizo za Kigiriki zilizotumika badala ya jina Kristo.
Ilikuwa ni miaka 60 ya baraza la Umoja wa Mataifa, lakini umeona wakuu
walivyo idizaini hiyo sitni na kusoemka 666, si kwa bahati mbaya hiyo
jooo!!!! Some one get paid and perfome his job so well
Kama nilivyo elezea hapo juu ukizitamka namba
hizo unapata sauti hii Xes au Ches sawa na sauti
ya “Jes” kwa Jesus. Herufi “J” ni
herufi inayotokana na herufi “I” nayo ni ya mwisho kuingizwa kwenye herufi za
lugha ya kingereza mnamo karne ya 16 na inatamkwa kama “Ye” na hii ndiyo
maana jina Jesus linapoingizwa kwenye Kiswahili linatamkwa kama Yesu ambayo ni
sawa na “Xes” Kigiriki na “Jes” kingereza. Wagiriki jina hili Christos (Kristo) wamelichukua
kutoka kwenye lugha ya Kiaramaiki kwa Wayahudi wa kale ambapo lilikuwa na
maudhui yaleyale ya Jesus (Yesu)/
Yeshua/ Messiah.
Nadhani jamaa unamjua, lakini umeona nyuma yake kuna kitu gani ...?!!!
Tunapo
tizama moja ya maana ya majina hayo yaani Jesus/Yesu/Yeshua/Messiah/Kristo
ni “Mpakwa
Mafuta”. Kwa maneno
mengine Kristo ni mtu mwenye upako, mtu aliye pakwa mafuta kama alama ya uteule
wake. Leo duniani kuna wetu wengi wanao jinadi kuwa wanao upako, yaani
wamepakwa mafuta, kwa maneno mengine watu hao ni Kristo na au Yesu, na au
Yeshua na au Messiah.
Unaiitaje tena hii? Mi sikumbuki labda geuza kompyuta yako chini juu, juu chini unaweza kuisoma .... lol
Watu hao pia wanafanya mambo ya maajabu, wanaponya watu
maradhi mbalimbali, wanawapatia utajiri na kadhalika, yote haya hayana shida,
kama mtu kapewa kipawa cha kuweza kufanya hayo si jambo la ajabu, lakini kuna
wale wanao dai wanaweza kufufua watu, hili nina mashaka nalo, lakini jambo
lililo na utata zaidi ni wao kujipamba na sifa isiyo yao, sifa ya Kristo, ni
wazi watu hao wanajiita wao ni Yesu, hata hivyo kuja kwa watu hawa
kumeshaelezewa katika vitabu vitakatifu ikiwemo Biblia na hapa si mahala pake
na wale ambao wanahisi hili lina wagusa na warejelee vitabu vya dini zao kupata
ukweli wa mambo.
Kerry yupo kazini, lakini mbele yake kuna 666
Hivyo
namba/alama 666 inayo maana ya Kristo lakini kama tulivyoona mwanzo kuwa namba/ alama hiyo ni jina na
ambapo tunapata majina mawili yaani jina la Kristo na
Jina la Mpinga Kristo je Freemasons
wanamaanisha jina lipi wanapo tumia 666?
Upo Hapo?????
Turudi
kwenye lugha ya Kiarameiki ambapo neno Messiah lenye maana ya Kristo ndipo
lilipotoka, neno hilo lina maana ya Msema kweli, Msema Uongo, mtu mwenye
kasoro, mtu wa kuzunguka dunia nzima,
maana hizo chache zinatosha kutupatia jibu letu. Sifa ya kuwa na Kasoro ni sifa
ya Masih Dajjal/ Mpinga Kristo kwani kati ya macho yake mawili moja ni chongo yaani halioni na
hii inahusishwa na alama ya jicho moja kwenye nembo za Freemasons. Sifa ya
kusema uwongo ni sifa ya Masih Dajjal/
Mpinga Kristo na hii pia ni
sifa waliyonayo Freemasons. Sifa ya Kuzunguka dunia nzima nayo ni Sifa ya Masih Dajjal kutokana na
mafundisho ya Kiislam ataizunguka dunia nzima kwa siku arobaini tu.
Hivyo sifa
moja inayobakia ya kusema Ukweli hii ni sifa ya Mtume wa Mungu Masihi Issa
(Yesu) hivyo moja kwa moja tunapata picha kuwa Freemasons wanapotumia
namba/alama 666 wanamaanisha jina gani, Masihi
Dajjal/Mpinga Kristo. Jina hilo
lipo kwenye shilingi mpya ya Euro, kwenye Bar Code ya bidhaa za Marekani ,
kwenye nembo za Microsoft kutaja kwa
uchache ila kiuhakika ziko kila kona na kwa njia moja ama nyingine tunazitumia
kufanikisha mambo yetu ya kila siku bila kufahamu.
Wale
wanao jinadi kuwa wa upako nao hawaunguki katika sifa za mtume wa Mungu Mmoja
bali katika sifa za Mpinga Kristo, kama nilivyokwisha elezea kuna ambao
wamepatikana wakijibadilisha na kuwa Nyoka, tuna waona wanavyozunguka dunia
nzima leo kwa mahubiri yao, kuna wanao dai kuwa wanafufua watu, ni hii ni moja
kati ya uwongo mkubwa atakao kuja nao Mpinga
Kristo atadai ana
fufua watu na atafanya hivyo lakini kiuhakika hatamfufua mtu bali mashetani
anao shirikiana nao ndiyo watakao jibadilisha na kuwa katika umbile na sura ya
mtu fulani aliyekufa na kudai yeye ndiye mtu huyo aliyefufuka.
Freemasons
ni wasimamizi wa mlango, na punde tu au muda kidogo mwenye mlango atasimama
mahala pake, naye si mwingine bali ni Dajjal / Mpinga
Kristo ambaye mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake)
amemtaja kama hivi,
“Nimewaeleza
mengi kuhusu Dajjal kiasi kwamba nahofia mtakuwa hamjamuelewa, Dajjal ni mfupi,
vidole vyake ni vipana na mwili wake umejaa nywele, ana jicho moja linaloona na
jingine lisiloona ... kama utamuona fahamu kuwa Mungu wako si jicho moja.”
Inajulikana
kuwa kabla ya kuja kwake kuna watu wataandaa njia na mazingira ya kuja kwake,
mfumo wa kufanya mambo ya watu hao utabeba sifa zote za Dajjal, kwa maneno
mengine waandaaji wa njia hiyo si wengine bali ni Freemasons. Jicho moja ni
mojawapo ya njia ya kumtambua Dajjal na jicho moja ni moja alama za Freemasons, Dajjal ni muwaji na
katili kwa wale watakao mpinga, atakuwa na nguvu ya kuwapa watu aridhi kubwa
zaidi au kuiharibu itategemea na jinsi gani watu hao watamfuata, sawasawa na
Freemasons wa magharibi kupitia World Bank wanazishikilia na kuzivunja vunja
nchi za Dunia ya Tatu kiuchumi kama haziendi na kufanya kulingana na sera zao.
IMF na mikopo yake ya ‘maendeleo’ imekuwa kama mitego juu ya nchi hizi
inawawekea riba kubwa ambayo daima inazifanya nchi hizo kuinama juu ya kila
kitakachosemwa na Freemasons hao ambacho si kingine ila ni sera zinazo za
kuporomosha uchumi wao na kuziacha masikini daima watumwa wa kuomba omba.
Njia
nyingine ambayo Dajjal ataitumia kuwalazimisha watu wamfuate ni kwa kusambaza maradhi.
Atakuwa na uwezo wa kusambaza maradhi na kuyatibu kiusahihi na sawasawa. Kwa
kutumia nguvu hiyo atawavuta wengi katika dini yake, dini ya Freemasons au
kiuwazi zaidi ni ya kishetani. Tunawaona Freemasons pia wakicheza na maisha ya
watu kwa njia kama hii, ushahidi mwingi unaonesha kuwa aina nyingi za virusi wa
maradhi mbalimbali ukiwemo UKIMWI vimetengenezwa maabara na baadaye vikatumiwa
kwa majaribio kwenye miili ya binaadam.
Dajjal atawadanganya watu kwa kujitangaza mwenyewe na sifa za Mungu
aliyetukuka. Freemasons nao wanatumia kila walilo nalo kuziondoa amri za Mungu
kwa kuweka amri zao kama wao ndiyo Mungu na ndiyo wanao uwezo wakufanya lolote
watakalo, wanatumia teknolojia mbayo hawataki watu wajue kuwa wanayo kuyatawala
maisha ya watu na kila kitu chao, wanata kuona na kusukia kila unachofanya,
wanatumia genetic kuharakisha maumbile na kuyabadilisha kutokana na wanavyo
taka wao. Waharibifu hawa hawaoni mipaka na wala hawatambui sheria kwani vyote
hivyo ni wao wameviweka.
Kama
ilivyo kwenye filamu ya Independence Day, watatujengea mazingira ya kukubali
serikali moja chini ya kiongozi mmoja wa kidunia kama njia ya pekee ya
kupambana na ‘adui kutoka nje ya
dunia’. Watatupatia
kiongozi wao huyo kama nembo ya umoja dhidi ya wote wanao pingana na serikali
hiyo wakiwemo hao ‘wageni’.
No comments:
Post a Comment