CCM: UKAWA WAKIMCHAFUA RAIS DK. MAGUFULI TUTAKULA NAO SAAHANI MOJA KUMTETEA
Monday, June 6, 2016
NA RORYA
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM), kimeonya vikali
juu ya mkakati wa viongozi wa UKAWA, wa kufanya ziara mikoani, katika kile ambacho wanakiita ni
kwenda kuishitaka serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Dk. John Magufuli kwa wananchi.
Aidha
CCM kimesema, daima hakitavumilia juu ya jambo lolote ambalo litaonekana kuwa na nia ovu ya
kumchafua Rais Dk. Mafuli na kitakula sahani moja na UKAWA katika kampeni hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, jana, Msemaji wa CCM, Christopher
Ole Sendeka, alisema, wamesikitishwa na
kauli zinazotolewa na wapinzani
ya kupinga kasi ya Rais Dk.
Magufuli hususan katika dhama yake ya utumbuaji majipu, kubana bajeti na
matumizi ya serikali pamoja na kuzitafutia ufumbuzi changamoto za wananchi katika sekta
mbalimbali.
Sendeka
alisema, upo mkakati mchafu ambao wapinzani wamekuwa wakipanga kwa nia mbaya ya kutaka kuchafua taswira ya
Rais Dk. Magufuli , mkakati ambao amedai hauwezi kuungwa mkono na wananchi.
Alisema,
tangu Mei 16 mwaka huu baada ya Kikao
cha Kamati Kuu ya CHADEMA, habari za mwanzo zilianza kuandikwa katika vyombo
mbalimbali vya habari juu ya yaliyojiri katika mkutano huo.
Alisema, mkakati huo
unaegemea katika kuandaa umma kwa kile kinachoitwa kwenda kumshitaki
Rais Dk. Magufuli kwa wananchi.
“Kwamba
Serikali ya Rais Dk. Magufuli inaidaiwa kuendesha nchi kifashist na
inalenga kuipeleka nchi katika utawala wa kidikteta ambao haujazoeleka katika nchi
yetu,”alisema Sendeka.
Alisema,
kipindi
cha nyuma moja ya mambo ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama
vyote ni ufisadi, rushwa na suala la
serikali kutokuwa na maamuzi, ambapo baada ya uchaguzi mkuu uliopita,
baada ya Rais Dk. Magufuli kuchaguliwa amesimama kidete kupambana na
mambo hayo licha ya kwamba yapo katika, ilani , sera za msingi na
kiapo cha
uanachama cha CCM.
“Wenzetu
mara baada ya kumpata mgombea wao
(Edward Lowassa), ujasili wa kuzungumzia rushwa na ufisadi ulipungua.
Kwa sababu ambazo kila mtanzania anajua
kwamba ni kwanini wamekosa utashi wa kuendelea kulikemea suala hilo la rushwa ,
ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma,”alisema Sendeka.
Alisema,
baada ya Rais Dk. Magufuli, kuingia Ikulu, mapambayo dhidi ya mambo hayo
ameyafanya kwa kasi ya aina yake, ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya rushwa, kuziba mianya ya upotevu wa fedha
za serikali, kubana matumizi kwa kufuta
bajeti kubwa za Sikukuu, kufuta safari za nje pamoja na wakati mwingine
kuelekeza fedha katika maeneo ambayo yanamatatizi makubwa.
Alise,
Rais Dk. Magufuli alichokuwa anafanya ni kumalizia ngwe ya mwisho ya bajeti ya
mwaka wa fedha 2015/16 na kwamba atafanya vizuri zaidi baada ya bajeti ya mwaka
wa fedha 2016/17 kupitishwa.
“Katika
mapambano hayo, ambayo
rais ameyafanya kwa utashi mkubwa,
tunajua kwamba yamegusa watu wengi . Hakuna mashaka kwamba katika nchi
hii tayari kuna watu ambao wametengeneza utajiri wa muda mfupi ambao
unatia ukakasi unaoweza kumuudhi mtu yoyote mwenye mapenzi
na nchi hii,”alisema Sendeka.
Alisema utendaji huo ulifanya kupokea sifa nyingi zilizoelekezwa kwa Rais juu ya utendaji wake,
lakini baada ya kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA, walibaini wazi bila mashaka kwamba
anayoyafanya Rais Dk. Magufuli yanapandisha chati ya CCM kwenda juu. Kwa sababu
serikali iliyopo madarakani ndiyo
inayokijengea chamas uhalali na uhalali wa chama chochote unsajengwa na
utendaji wa serikali iliyopo madarakani.
“Serikali iliyopo madarakani isipo tekeleza matarajio
ya wananchi, uhalali wake haupo. Vitendo vya Rais Dk. Magufuli, hakuna mashaka
kwamba watanzania wameunga mkono na
Dunia imeunga mkono. Hata umoja wa
mataifa kupitia Shirika la Maendeleo (UND) imeunga mkono uwajibikaji huo,
katika mapambano ya rushwa , ukusanyaji mapato na nidhamu ya uwajibikaji
kwa watumishi wa umma,”alisema Sendeka.
Alisema,
inashangaza kuona kwamba CHADEMA wanadai suala la kupambana na rushwa na
ufisadi Rais Dk. Magufuli amepora kwao
na kusahau kwamba , ajenda hiyo ilikuwa ni ya CCM na TANU.
“Kilicho
fanyika ni kumpata kada ambaye anaweza kusimamia na kutekeleza hayo, jambo
ambalo limeanza kuwafanya wapinzani kuamini kwamba itaua
upinzani, na kwamba hofu yao ni uwezekano wa kupoteza wabunge wengi katika uchaguzi mkuu wa 2020 ni
mkubwa,”alibainisha msemaji huyo.
Alisema
baada
ya kufanya tathimini hiyo ndipo walipokubariana kwenda kwa wananchi
wakiwa na ajenda ya kupotosha umma juu ya utendaji wa Rais Dk.
Magufuli na serikali yake.
“Walianza
na kampeni ya rais ya utumbuaji wa majipu na wao kupitia kwa mgombea wao wa
urais Lowassa kisha kwa mwenyekiti wa CHADEMA , Freeman Mbowe, walikemea ajenda hiyo kwamba inaukiukwaji wa haki za
binadamu.
Kwamba
unapokwenda bandarini nakukuta makontena 2000 au 3000 hayajalipiwa kodi
unamuacha huyo Kamashna na wasaidizi
wake na kwamba hiyo ndiyo haki ya
binadamu?” alihoji Sendeka.
Alisema viongozi hao pia waliponda kwamba serikali ya
Rais Dk. Magufuli inatanguliza vitendo kuliko fikra.
“Hivi
jamani, umemkuta mtu na kila dalili za
kufanya ufisadi, unamuacha na kuanza kufikiria jambo la kufanya.
Serikali ya
Magufuli inasema kaa pembeni, jitetee kisha hatua zaidi zinachukulia .Hii ni kwa nia njema ya
kueta maendeleo ya nchi kwa kutumia
vyanzo vya mapato yetu, kutoa huduma muhimu zinazostahili kwa wananchi.
Na
kazi hiyo ameifanya kwa ufanisi mkubwa kwa muda mfupi aliokaa katika
uongozi,”alibainisha Sendeka.
Aliongeza
“Sasa haya yamewaudhi. Walijaribu kupima kina cha maji wamebaini kwamba
hawayawezi na wamebaini kwamba watanzania wote wamechoka na wanaunga mkono
hatua hizi za rai,”
Sendeka
alishangazwa na wapinzani kulalamikia
hatua ya Rais Dk. Magafuli kutumbua majipu
kwamba ni udikteta na ufashisti wakati rais ania njema ya kutetea
wanyonge na maslahi mapana ya taifa.
Alisema
binafsi
anamuunga mkono Lowassa kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kwamba,
kazi yake kubwa sasa ni kukigeuza CHADEMA kutoka kuwa katika
kikundi cha wanaharakati na kuwa chama kamili.
“Najiuliza
kama miaka 20 zaidi ya uwepo wa CHADEMA
hakikuweza kubadilika kutoka katika kikundi cha wanaharakati mpaka Lowassa
alipo kikuta na kutaka kukibadilisha ndani ya miaka minne ijayo kiweze kuwa chama kamili cha siasa nina
uhakika muda huo hautoshi,” alisema Sendeka.
Aliongeza, ”Lakini
najiuliza kama Magufuli anatumbua majibu wapinzani wanadai
ni dikteta na fashist. Magufuli anaziba
mianya ya rushwa wanachukia. Najiuliza
wametumwa nanani? Kumwakilisha nani? Kutetea maslahi ya nani? Na nani
kawafadhili?
”
Alisema ni dhahiri anayetetea ufisadi anawasemea waliotumbuliwa na ambao mianya yao
ya rushwa imezibwa.
Sendeka alisema,
wakati ufusadi ulivyo kuwa ukifanyika
katika sekta muhimu, wapinzani hawakuacha Bunge wala vikao na kwenda kuitisha
mikutano kwa wananchi na kuwaambia kwamba bandari na TRA kuna ufisadi.
“Wakati
wa kashfa ya ukwepaji wa kodi ya sukari hakuna aliyetoka kwenda kwa wananchi
kuitisha mikutano au kuingia barabarani kuandamana kwa sababu kodi haijalipwa. Wakati
wa kashfa ya Escrow, hakuna chama
kilicho funga safari kwenda mikoani kuitisha mikutano na kuwaeleza
wananchi kwamba kuna ufisadi huo,”alisema
Sendeka.
Alisema,
inshangaza kuona wakati serikali inajitahidi kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi,
wapinzani wanajipanga kwenda mikoani kupinga hatua hizo kwa kile wanachokiita kushtaki serikali kwa wananchi.
.
“Dhamira
ya wenzetu sasa ni kujitahidi kutumia
nguvu zao na zawale wanaowatuma kuchafua
jina la Dk. Magufuli bila kuelewa kwamba Watanzania
hasa wanyonge wataendelea kutumia
jina la Rais huyu kama alama kuu na muhimu , katika mapambano dhiti ya
ukiritimba, ufisadi, na viongozi
na watendaji wanaokubali kufanya kazi ya ukuwadi kwa manufaa yao binafsi huku wakiyaweka pembeni maslahi ya
taifa,” alisema Sendeka.
Alisema
CCM haipingi ziara hizo za viongozi,
lakini daima hakitavumilia ikiwa
mikutano yao italenga katika kumchafua rais.
“Wakijaribu
kuchafua rais, watakapo CCM nayo itakanyaga pia. Watakapo ondoa mguu wao
nasisi tunaweka mguu wetu ili kuwaeleza ukweli wananchi juu ya kazi kubwa inayofanywa
na serikali. Tunawasemaji wengi na
tunauwezo wa kufika popote,” alisema Sendeka.
Aliongeza, ”Watanzania
watapima, kauli ya watu wanaotetea mafisadi, wakwepa kodi na wala rusahwa na
CCM inayotetea wananchi wanyonge ili waweze kufaidi matunda ya nchi yao,”
Alisema,
kama hoja zao ni hizo, za kumchafua Rais
Dk. Magufuli CCM inawaonea huruma, na
wasifiriki watanzania walio timamu watawaunga mkono.
“Siyo tu kwamba watanzania hawatawaunga mkono, bali watawashangaa na heshima yao
itashuka. Watanzania wanaakili, hawawezi kutetea wezi wakati rais anafanya kazi nzuri ya
kuwatetea,”
No comments:
Post a Comment