MIZIMU YA OSAMA YAMTESA OBAMA ALAZIMIKA KUMFUFUA OSAMA BIN LADE.
Niliisha
kwisha kuelezea katika makala zangu zilizo tangulia, ambazo zilichapishwa wenye
gazeti la mtanzania kuwa kuna uwezekano mkubwa Bin Laden alishakufa tangu 2001,
lakini maadui zetu hawatatangaza kifo chake mpaka watakapo maliza kazi na jina lake.
Nilisema hayo nikiambatanisha na ushahidi wa
kutosha wa namna gani Osama anaweza kuwa ameshakufa kuliko kuwa hai, na
nikaongezea kuwa maadui zetu watakapo maliza kazi na jina lake hawatosema
wamemkamata bali wamemuua, tena kwa kikosi maalum.
KILIKUWA NI KIKOSI MAALUM
Na ndicho
kilicho tokea. Inaonekana nilikuwa sahihi tangu mwanzo.
Sina
haja ya kurudia tena hapa kuwa ni namna gani utawala wa Bush ukishirikiana na
serikali vivuli za siri na asasi za siri walivyoweza kufanikisha 9/11 na
kumrushia lawama zote Bin Laden. Lakini huenda baadaye nikarusha post zinazo
muhusisha Bush moja kwa moja na 9/11, Ila nitakachozungumzia hapa kwa kina ni
mustakabali wa ajenda nzima baada ya kifo cha bin Laden.
Kuna
ushahidi wa kutosha kuwa bin Laden alishakufa tangu 2001.
Kwa kuanzia wakati
Obama anatangaza kifo cha Osama Bin Laden kupitia kwenye luninga, kile ambacho
watu wengi walikuwa hawakifahamu ni kuwa Obama alikuwa ni mtu wa tisa kwenye
orodha ya viongozi wakubwa kiserikali kutangaza kifo hicho, yaani hiyo ilikuwa
ni mara ya tisa kwa Osama kutangazwa kuwa amekufa.
Mr. OBAMA NA STAFF WAKE WAKIFUATILIA KWA MAKINI 'TUKIO'
Bin
Laden alikuwa na tatizo la figo na alikuwa akihitaji mashine ya kusafishia damu
, hili limeelezwa mara kadhaa na viongozi wa kiserikali wananchi mbalimbali,
hivyo alishakufa muda mrefu hata kabla Obama hajakitangaza kifo hicho na yeye
kuwa ni mtu wa tisa kufanya hivyo. Ni kama Osama amekufa mara tisa na kufufuka
kila mara.
Wakati
shambulizi la 9/11 likitokea, Osama alikuwa amelezwa kwenye hospitali ya
kijeshi Pakistan akitibiwa tatizo lake hilo la figo. October 2001, Bin Laden
alitokea kwenye video akiwa kavalia kijeshi na kajifunga kilemba, mwili
umedhoofu na anaonekana kukonda.
BIN LADEN ALIVYOONEKANA MWAKA 2001, OKTOBA
Disemba
2001 akatokea kwenye video nyingine, akiwa kavalia kijeshi na kilemba, lakini
hapa alionekana amechoka zaidi na afya yake imedhoofu maradufu kiasi kwamba
hakuweza hata kunyanyua mkono wake wa kushoto.
BIN LADEN ALIVYOONEKANA MWAKA 2001, DISEMBA
Ilipofika
Disemba 26, 2001, Fox News ilirusha habari iliyoichukua kutoka katika gazeti la
Pakistan Observer ikisema kuwa viongozi wa Taliban walitangaza rasmi kifo cha
Osama mapema mwezi Disemba 2001, na kwamba alizikwa ndani ya masaa 24 kama
zilivyo taratibu za Kiislam.
TAARIFA YA TALIBAN JUU YA KIFO CHA OSAMA MWAKA 2001.
Januari
18, 2001, Rais wa Pakistan Pervez Musharraf alinukuliwa akisema kuwa, Osama Bin Laden alishakufa. Musharaf akaendelea kusema kuwa
alifahamu Osama amechukua mashine mbili za kumuwezesha kuishi kama njia ya
kusafishia damu yake kwa vile figo yake imekufa na mazingira ya kuhama hama
anayoishi, pamoja na wataalam ambao wanahitajika kuziendesha mashine hizo, na
umeme pia, ni vigumu kusema kuwa Osama yuko hai, na picha zake za hivi karibuni
zinamuonesha amezidi kudhoofu.
Julai
17, 2001, kiongozi wa FBI kwenye kitengo cha kupambana na ugaidi, bwana Dale
Watson alisema haya:
‘Mimi
binafsi nafikiri Osama hayuko pamoja nasi tena’
October
2001, rais wa Afighanstan na kibaraka wa Illuminati, Hamid Karzai kupitia
kwenye mahojiano na CNN alisema hivi,
‘ Naamini Bin
Laden ameshakufa.’
Novemba
2001, Senator Harry Reid alisema kuwa ameambiwa kwamba Osama alikufa kwenye
tetemeko la aridhi lilitokea Pakistan October, 2005.
September
2006, kitengo cha ujasusi cha Ufaransa kilivujisha habari kuwa Osama bin Laden amefia Pakistan.
Novemba
2, 2007, aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistan Benazir
Bhutto alisema kwenye mahusiano na kituo cha Al-Jazeera kuwa Osama bin Laden ameshauwawa na akamtaja
muuaji wa Osama kuwa ni Omar Sheikh. Bhutto aliishi wiki moja tu baada ya
mahojiano hayo, aliuwawa na mtu wa kujitoa muhanga.
Machi
2009, mtu aliyeshikilia wadhifa kwenye kitengo cha ulinzi cha Marekani na
ambaye ni profesa katika chuo cha Buston bwana Angelo Codevilla alisema kuwa Elvis Presley anaweza kuwa hai lakini si Osama.
Mei
2009, kiongozi wa Pakistan, Asif Ali Zardari alisema kuwa, mashirika ya kijasusi ya Marekani hayajasikia chochote kutoka kwa
Osama kwa miaka saba na sidhani kama bado yupo hai.
Leo hii
Obama kaongezeka kwenye orodha ya watu hao mchanganyiko waliotangaza kifo cha
Osama. Wengine wanaweza kusema taarifa za viongozi hao walio tangulia kabla ya
Obama hazina ushahidi wa kutosha bali ni maneno matupu.
Lakini
Pia taarifa ya Obama haina ushahidi wowote zaidi ya picha za mtu ambaye
anaonekana nusu ni Osama, nusu mtu mwingine. Hata hivyo picha hizo
tumeshazigundua kuwa ni za kughushi.
INGAWA BINA LADEN 2001 ALIKUWA MZEE SANA,
LAKINI ALIPOKUFA MWAKA 2011 ALIONEKANA KARUDI KUWA KIJANA, KAMA
ALIVYOKUWA AKIONEKANA KWENYE MIAKA YA 90, MAAJABU HAYA ...
Picha
ya mtu asiyefahamika ambayo imeunganishwa na ile ya Osama ilikuwepo kwenye
mitandao mikubwa kwa muda wa miaka miwili, kabla ya tarehe 1 Mei ambapo Obama
alituambia kuwa picha hiyo ni ya Osama.
Picha hiyo ya mtu asiyefahamika ilikuwepo
kwenye mtandao wa The Mail, Times, Telegraph, Sun na Mirror, hata hivyo
mitandao hiyo iliiondoa picha hiyo kimyakimya baada ya kufahamika kuwa ni ya
kughushi.
Picha
ya Osama iliyounganishwa na picha ya mtu asiyefahamika ni ya mwaka 1998. Ndio
maana kwenye picha hiyo anaonekana amekufa akiwa bado na afya, wakati video
yake ya mwaka 2001 Disemba alikuwa amedhoofu kiasi hawezi hata kunyanyua mkono
wake wa kushoto.
Hivyo
kama unashaka na kifo cha Osama kwa vile walio tangulia kusema kabla ya Obama
hawana ushahidi basi kuwa na shaka na taarifa ya Obama pia kwani ushahidi wake
ni wakutengeneza.
Hakuna
aliyeioyana maiti ya Osama, (hata samaki kwenye bahari ambayo mwili wa Osama
umetupwa wanadai hawajauona mwili wake, ha hah ha hah ha …. Cheka kwa afya)
Obama
na uongozi wake bado unajadili ikiwa kuna haja ya kuzitoa picha zingine ama la.
Mazishi yake yamefanyika ndani ya masaa 12, baharini, ajabu wanasema hakuna
nchi ambayo ingekubali kuupokea mwili huo. Sidhani kama wangwauliza Alshabab
kama wanautaka ama la, nadhani alshabab wangefurahia kuwa na kaburi la Osama
ndani ya Somalia ...
Ni vipi
tukachukua maneno yao yasiyo na ushahidi watu ambao mpaka leo wanaendelea
kutudanganya kuwa ni Osama ndiye aliyehusika na shambulizi la 9/11?
Osama
ametangazwa amekufa nini kinafuata.
Kama
nilivyo kwisha kusema kuwa kifo hicho kingetangazwa pale tu, Illuminati
watakapo kuwa hawana haja na jina hilo kwenye ajenda yao.
PICHA ILIYO FANYIWA 'ADOBE' YA 'OSAMA' AKIWA AMEKUFA
Ndio kusema jina la
Osama limeshamaliza kazi yake?
Ndiyo wameshamaliza kazi na jina la Osama na
sasa watatumia mzimu wa Osama kuifikisha ajenda pale inapotakiwa.
Au kwa
maneno mengine jina la Osama lilikuwa muhimu katika kufanikisha uvamizi wa
Afighanstan na Iraq na kuzizorotesha baadhi ya nchi kiulinzi na kiusalama kama
vile Pakistani, sasa tunakwenda kwenye hatua ya pili ya vita dhidi ya ugaidi,
hatua ambayo haitakuwa na maana kuitangaza kama Osama atakuwa bado yupo hai,
hivyo ‘Osama Must Go’ kama walivyokuwa wakisema Wakenya dhidi ya Moi ... huwezi
kuanzisha vita vingine wakati vile vya awali kunayo kila dalili na ushahidi
kwamba umeshindwa ... NA WAKATI WA KUINGIA HATUA YA PILI YA VITA DHIDI YA
UGAIDI ULIKUWA UMEFIKA, HIVYO ‘GAIDI’ LAZIMA AONDOLEWE ILIKUTOA NAFASI YA ‘KUFUNGA
VITABU’ VYETU HASA UKICHUKULIA KWAMBA HATUA YA PILI INGEKUWA NA MKANGANYIKO WA
HABARI KAMA ‘GAIDI’ ANGEKUWA BADO YUPO HAI.
Kwa
wale waliokuwa wanafuatilia taarifa za kifo cha Osama kupitia vyombo vya habari
watakuwa waligundua kitu kimoja muhimu ambacho kinapaswa kufanywa na mzimu wa
Osama Bin Laden. Taarifa za kifo cha
Osama ziliambatana na hofu na vitisho
kwa taifa la Marekani kuwa wafuasi wa Osama bin Laden watalipiza kisasi cha
kiongozi wao.
Uwongo
mtupu watalipiza vipi kifo cha Osama ambaye alishakufa karibu miaka 10 iliyopita?
Haikuchukua muda wale wanaojiita ni viongozi wa Talibani wakaanza kutoa taarifa
kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa watalipiza kisasi cha kiongozi wao.
Moja na moja ni mbili, wanaojiita Talibani, Al-Qaeda, Al-Shabab na wengine
watakao kuja lao na Illuminati wote ni kitu moja, tumeshaona Osama alishakufa
muda mrefu lakini kwa vile ajenda ilitaka kuendelea kulitumia jina lake
hawakutangaza, na wala viongozi wa Al-Qaeda na Talibani hawakuwaambia
walimwengu kuhusu hilo, taarifa za awali za kifo chake zilizo tokana na
Talibani hazikutangazwa tena, wala wakati CIA na wenzake wakishirikiana
kutengeneza video na audio za kughushi za Osama, Talibani wala Al-Qaeeda
hawakuja kusema kuwa video na sauti hizo ni za kughushi, walinyamaza kimya,
kwani ndivyo ajenda ilivyo taka, na wao na Illuminati ni pande mbili za
shilingi, leo Illuminati wanatutangazia kifo cha Osama kwa mara ya tisa
Talibani na Al-Qaeda wanajitokeza na kuthibitisha kifo, lakini hawaishii hapo
na mrithi wa Osama wanamchagua.
MOJA YA VIDEO FAKE ZA OSAMA ZILIZO TOLEWA NA
FBI, WALIKUWA NAZO NYINGI SANA KILA PALE ILIPOHITAJIKA MOJA, WALIZINDUA
HASA KUPITIA ALJAZEERA, NA ZILIKUWA ZINAUZA KWELI, MPAKA AUDIO, BUSH
NDIYO ALIFAIDIKA SANA MAUZO YAKE MPAKA AKACHAGULIWA MARA YA PILI KUWA
RAIS WA MAREKANI, NAFIKIRI BUSH ATAMISI SANA BIN LADEN.
Waongo,
wanafiki na wahaini wakubwa, wanaurubuni umma wa Kiislam kwa kujifanya wana
uchungu na kifo hicho na kwamba wataendelea kuutetea Uislamu, lakini kumbe
wanafanya kinyume chake kabisa, wao na Illuminati lao ni moja. Haijachukua muda
vibaraka hao wa Illuminati walifanya shambulizi Pakistan na kuuwa watu wapatao
80 katika kile walichokiita kulipiza kisasi cha Osama, lakini tunajua
hawalipizi kisasi bali wanaiandaa Pakistan na nchi zingine za Kiislam kushiriki
kwenye WWIII. Na hii kwa taarifa yako ndiyo hatua ya pili ya vita dhidi ya
Ugaidi.
Hivyo
ndivyo mzimu wa Osama utakavyo endelea kutumika, wale wana jinadi kuwa ni
Talibani na Al-Qaeda wataendelea kushambulia maeneo mbalimbali duniani kwa
kisingizio cha kulipiza kisasi cha kiongozi wao. Wataachiwa wasambae kila kona
ya dunia, leo kuna makelele mengi yanapazwa kuwa tayari wapo ndani ya Afrika
Mashariki kupitia kwa ndugu zao wa Al-Shabab ambao nao walitangaza kujiunga na
Al-Qaeedah kuwa kitu kimoja.
Tanzania
na sisi hatupo salama kwenye, si kwamba hatupo salama kwa vile KUNAUGAIDI
TANZANIA! HAPANA, HATUPO SALAMA KWA VILE TANZANI AHAKUNA UGAIDI, KAMA AMBAVYO
DUNIANI HAKUNA UGAIDI LAKINI JUHUDI ZA MAKUSUDI ZIMEFANYA NA WANAO PIGANA ‘VITA
DHIDI YA UGAIDI’ KUTENGENEZA JINAMIZI HILO DUNIANI, NA JUHUDI HIZO NAONA
ZINAANZA KUSHIKA MIZIZI HAPA TANZANIA, NA TARATIBU WANAANZA KUTENGENEZA
MAZINGIRA YA UHASAMA BAINA YA WAISLAMU NA WAKRISTO ILI KUTOA MWANYA WA JINAMIZI
HILO KUWEPO HAPA TANZANIA.
Picha kubwa inaonekana kuwa katika moja ya
mashambulizi haya ya kulipiza kisasi, kuna kubwa ambalo litafanyika baina ya mwaka huu na
mwaka unao kuja kiasi kwamba athari ya shambulizi hilo, litaweza kuipigisha
ajenda hatua nyingine kubwa kama tukio la 9/11 lilivyo fanya.
Kipengele
hicho hapo juu nilikiandika muda mrefu sana wakati bado naandika makala kwenye
gazeti la Mtanzania, hivyo sikuwa nikifahamu ni tukio gani kubwa litakalo fuata
katika kuwasogeza walimwengu uso kwa uso na WWIII .... Ila sasa nimefahamu.
Nadhani
hatua hiyo kubwa itakuwa ni ya mwisho kuelekea kwenye WWIII au kuandaa
mazingira ya mwisho ya vita hivyo vikubwa vinavyo subiriwa ili NWO isimame.
Endelea
kufuatilia habari kwa makini na utaona mzimu huu wa Osama utakavyo tumika
kufanikisha hilo. Kitu kingine cha kuangalia ni tarehe, utakumbuka ni September
1991 Bush baba aliitangaza ajenda hii rasmi ndani ya bunge la Marekani, Miaka
11 baadaye tukio kubwa na la muhimu la kufanikisha ajenda likatokea, nalo ni
maarufu kama 9/11. Tukiwa tumebakiza miezi michache kabla ya miaka 11 kutumia
baada ya 9/11 kifo cha Osama kinatangazwa, hii ni muhimu kwa sababu kwa kutumia
kifo hicho tukio jingine kubwa la kuipigisha ajenda hatua linahitajika, tizama
kalenda yako vizuri, baina ya mwaka huu na mwaka ujao utausikia mzimu wa Osama
ukifanya kazi nyingine muhimu kwa ajili ya ajenda.
Tukio
lenyewe ni kile kinacho endelea Mashariki ya Kati hivi sasa na kile
kinachoendelea kwa baadhi ya nchi za Kiarabu zinazo patikana kwenye ukanda wa
Afrika.
Waingereza
kwa kutumia mamluki wao baada ya kuiangusha dola ya kiislamu kwenye WWII, Dola
ya Ottoman, eneo la Mashariki ya kati ambalo mwanzo lilikuwa chini ya Dola hilo
lilikuwa ni kubwa sana, hivyo kwa harakaharaka Freemason wa Magharibi
hawakuweza kulihamishia eneo lote kwa familia zao za kishetani za Illuminanti, waliacha
maeneo hayo kwa watu ambao walishirikiana nao kuiangusha Dola hiyo ya Kiislamu
na lengo lao kubwa wakati huo ilikuwa ni mafuta na utaona baina ya hapo mafuta
yote ya Mashariki ya Kati yalihamishiwa kwa wamiliki wa Ulaya.
Illuminanti
wa Ulaya wakishirikiana na vibaraka wao wa Mashariki ya kati ambao wakijiita ni
waislamu wakaanza kuvuna mafuta, lakini juu ya yote kwa kutumia mafuta hayo
Illuminanti wakishirikiana na vibaraka wao wakazizamisha nzhi zinazo endelea
katika mzigo mkubwa wa madeni na kuipatia Marekani U-Super Power baada ya
kuamua kuwa mafuta yote yauzwe kwa sarafu ya Dola.
Sasa
vibaraka wamelishwa na kunenepa mpaka wakasahau kuwa wao ni wanasesere mbele ya
Illuminanti na wanamilikiwa na Illuminanti, katika hatua hii ni vigumu mno
kumuambia kibaraka kuwa, mafuta peke yake siyo lengo la sisi kukuweka hapo,
tunataka kuitawala dunia nzima ukiwemo wewe mwenyewe na wananchi wako.
Hivyo
watu wengine walio andaliwa vyema na wenye maono mapana ya ajenda na mitazamo
yake, wenye kufikiri kama ajenda inavyo taka, ndiyo wanao takiwa kuingia hapo
kwenye hivyo viti, hivyo vibaraka wa zamani lazima waondoke kupisha vibaraka
wapya watakao visogeza vita dhidi ya ugaidi kwenye mlango wa WWIII.
Hichi ndicho
kinacho zikumba nchi za Kiarabu hivi sasa, yanayo itwa mapinduzi si chochote si
lolote ni moja ya mipango kamambe, iliyo pangwa na kuratibiwa vyema katika
kufanikisha zimwi la ugaidi kwenye hatua ya pili. Viongozi hawa wapya ndio
watakao ulazimisha umma wa Kiislamu kuungana dhidi ya magharibi, na hiyo ndiyo
kazi yao wanayo pewa. Hilo ndiyo lengo la vibaraka hao wapya, hawa ndiyo
watakao washa cheche zitakazo lipua nyuklia ya kwanza kwenye uwanja wa WWIII.
Karata
ya mwisho ya mchezo mzima ni kuwaingiza waumini wa Kiislam kwenye uwanja wa
vita dhidi ya ulimwengu. Vita hivi ndivyo vitakuwa vita vikubwa kupiganwa
kwenye uso wa dunia, tangu historia ya binaadam ilipo anza kuandikwa. Vita hivi
ndivyo vitakuwa vita vikubwa kuliko vyote katika zama zetu, vita hivi vitaitwa
WWIII, na baada ya hapo wanategemea kusimamisha NWO.
No comments:
Post a Comment