Tuesday, June 30, 2015

KILA SAA MAPENZI…MAPENZI…HIVI HAMNA MENGINE YA KUFANYA?

Mpenzi msomaji wangu, wiki iliyopita utakumbuka nilizungumzia suala la kuwajali wapenzi wetu. Niligusia suala ya kuwapa nafasi watuchune.
apo walioshituka kuona kichwa kile cha habari lakini kiukweli sikumaanisha kuchuna kule ambako wanawake micharuko hufanya hasa kwa waume za watu, nilimaanisha utayari wa kila mmoja kumsaidia mwenzake kifedha. Mkeo akitaka pesa ili aende saluni kama zipo, mpe! Akihitaji pesa akanunulie vipodozi na nguo kama pesa zipo, mpatie.
Tusibaniane pale ambapo Mungu ametujaalia uwezo wa kuwafanya wenza wetu waonekane watu mbele ya wenzao. Hili ni kwa mke na mume na hata wapenzi wa kawaida. Baada ya kugusia hayo, nigeukie sasa kwenye mada yangu ya wiki hii.
Ndugu zangu, nimekuwa nikipokea malalamiko mengi kutoka kwa baadhi ya wanawake wakielezea kukerwa kwao na tabia za waume zao kuendekeza sana tendo la ndoa. Wanaume wanaoweka mbele suala hili husimamia kwenye ile pointi kwamba, kufanya mapenzi na wake zao kila wanapojisikia ni haki yao ya ndoa.
Hali hii imewafanya baadhi ya wanawake kufikia hatua ya kuomba talaka kutoka waume zao kutokana na kushindwa kuhimili vishindo. Wanaume wengi huwa wagumu sana kuzitoa talaka na ndiyo maana wakati mwingine wanawake hulazimika kwenda mahakamani kudai talaka japo si wote wanaodai kwa kukimbia tendo la ndoa.
Wanaoendelea kuwepo kwenye ndoa na wanaume wanaohusudu mapenzi, hulazimika wakati mwingine kujifanya wanaumwa ili kuepukana na kero hii. Kimsingi ndoa haiwezi kunoga bila kuwepo suala la kukutana faragha na hili linaelezwa hata kwenye vitabu vya dini.
Tunaponyimana licha ya kuwakera wenza wetu lakini pia tunamkasirisha Mungu ambaye anatutaka tufanye hivyo ili tuzaliane. Hata hivyo, kila kitu kina kipimo chake na kikizidi inakuwa ni tatizo. Wazungu wanasema; ‘Too much is harmful’.
Hili lipo hata kwenye suala la mapenzi. Ukiwa kila wakati utataka kukutana na mpenzi au mwenza wako faragha, hata ile raha iliyotarajiwa haiwezi kupatikana, matokeo yake itakuwa ni karaha. Nalazimika kuandika makala haya kutokana na ukweli kwamba, huko mtaani kuna baadhi ya watu wameliweka sana mbele suala hili.
Yaani wao kila wakati ni mapenzi… mapenzi…mapenzi….Usiku kucha hawataki hata wenzao wapumzike. Ni mchakamchaka mwanzo mwisho. Sasa huku ni kukomoana au kitu gani? Wengine wapenzi wao hawajisikii kufanya tendo hilo kutokana na kuumwa au kutokuwa na hamu.
Hiyo ni hali ya kawaida kwa binadamu lakini utashangaa mwanaume anakuja na kulazimisha mambo. Huku ni kuumizana na raha haiwezi kupatikana kwa njia hii. Katika lile tendo furaha inapatikana pale kila mmoja anapokuwa anajisikia kuwa faragha na mwenzake.
Ni tendo takatifu linalohitaji maandalizi ya kimwili na kifikra kwa hiyo tusipelekeshane. Wakati mwingine tuzikontroo hisia zetu. Katika hili naomba nishauri yafuatayo; Kwanza tujitahidi sana kujitoa kwenye kundi la watu wenye pepo wa ngono. Tukiwa kwenye kundi hili, si kwa mwanaume tu bali hata kwa wanawake ni lazima tutakuwa ni watu wa kuwaza kufanya mapenzi kila wakati.
Tuwe watu wa kuzishughulisha akili zetu kwa kufanya kazi na kuwaza mambo ya kimaendeleo na si kila wakati kutaka kuwa na wapenzi watu faragha. Itaendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment