Monday, July 18, 2016

MSAMA AMPONGEZA WAZIRI NAPE KWA KUKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII, ASEMA ANAUNGANA NAYE KATIKA VITA HIYO

MSAMA AMPONGEZA WAZIRI NAPE KWA KUKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII, ASEMA ANAUNGANA NAYE KATIKA VITA HIYO

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Action Mart Bw Alex Msama akionyesha Stika za TRA zinazodaiwa kutolewa kimyemela na Baadhi ya watumishi wa TRA waso waaminifu kwa kushirikiana na watu wanaorudufu kazi za wasanii kinyemela ili kujipatia kipato Msama Amempngeza Waziri wa Habari , Uramaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kwa kazi aliyoifanya kutoka ofisini na kuenda kwenye maduka mbalimbali Kariakoo kwa ajili ya kusaka wezi wa kazi feki za wasanii 
Amesema Jambo hilo limemtia moyo kama mpigania haki wa kazi za wasanii ambaye amekuwa akipambana kila siku ili wasanii waweze kufaidika na jasho lao na ataendelea na kazi ya kuhakikisha wezi wote wa kazi za sanaa wanashughulikiwa kisheria na kuwafanya wasanii nao wanafaidi jasho lao.
2
Bwa Alex Msama akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam.
3Bw. Alex Msama akionyesha baadhi ya stika za TRA zinazodaiwa   kuibiwa na kugawiwa kinyemela kwa wauzaji wa Kazi feki za wasanii.
4
Hii ni moja ya CD feki iliyobandikwa stika za TRA.
5Bw. Alex Msana akionyesha CD Feki na Stika zinazodaiwa kutuolewa kinyemela na baadhi ya watumishi wa wasio waaminifu

No comments:

Post a Comment