Friday, June 17, 2016

JK BALOZI WA HESHIMA MAENDELEO YA KILIMO, AFRIKA, KARIBIANI NA PASIFIKI


NA BASHIR NKOROMO
……………………………….
KITUO cha Ufundi cha Kilimo na Maendeleo Vijijini (Technical Centre for
Agricultural and Rural Cooperation, CTA) chenye makao makuu mjini
Wageningen, Uholanzi kimemteua Rais Mstaafu Dk. Jakaya  Kikwete kuwa
Balozi wa Heshima (Goodwill Ambassador) wa Maendeleo ya Kilimo katika
Mabara ya Afrika, Karibiani na Pasafiki.
Katika barua iliyokabidhiwa na mjumbe wa Bodi ya CTA, Prof. Faustin Kamuzora,
CTA wameainisha kuwa Dk. Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Taifa,
ameteuliwa kwa kutambua mchango wa juhudi zake katika kukiendeleza
kilimo nchini Tanzania na barani Afrika.
Katika wadhifa wake huo mpya, CTA imemuomba Dk.  Kikwete aweze kuiwakilisha
katika makongamano ya kimataifa ambapo atazungumzia umhimu wa
kukiendeleza kilimo kwa ajili ya kutoa fursa ya ajira zenye staha kwa
vijana na wanawake katika nchi za barani Afrika, Karibiani na Pasifiki.
Pia ataisaidia CTA katika kuandaa makala na kufanya mahojiano na
waandishi wa habari katika nchi mbalimbali.
Dk. Kikwete amekubali uteuzi huo na kuahidi kushirikiana na CTA katika
kutekeleza mambo ambayo ameombwa kuisaidia na taasisi hiyo ambayo ni
ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Kundi la nchi za Afrika, Karibiani na
Pasifiki wenye makao makuu mjini Brussels, Ubelijiji.
Prof. Kamuzora ambaye pia ni Katibu Mkuu, Mawasiliano ni mjumbe wa Bodi ya
CTA akiwakilisha nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa miaka mitano
tangu 2013 hadi 2018.

No comments:

Post a Comment