Friday, June 17, 2016

WAZIRI POSSI AIWAKILISHA VYEMA AFRIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUTOKOMEZA UMASIKINI NA KULETA USAWA KWA WATU WENYE ULEMAVU


 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Wenye Ulemavu) Mhe.Dkt.Abdallah Possi akichukua dondoo za Mkutano wa 9 wa nchi ambazo
zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Marekani tarehe 15 Juni, 2016.
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa 9 wa nchi ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu wakifuatilia mada wakati wa
mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa New York Marekani Juni
15, 2016.
…………………………………………………………………………………………..
Na.MWANDISHI WETU
Siku ya tarehe 15 Juni, 2016, Mhe. Dkt. Abdallah Possi (MB),
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu alishiriki  katika  Mjadala wa
kutokomeza umasikini na kuleta usawa kwa watu wenye ulemavu. Majadiliano hayo
yalikuwa ni moja ya mikutano muhimu iliyolifanyika katika Mkutano wa 9 wa nchi
ambazo zimeridhia Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu uliofanyika New York,
Marekani.
Mwenyekiti wa majadiliano hayo alikuwa ni Bi. Ellen Maduhu,
Afisa katika ofisi ya uwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
ambaye pia ni Makamu wa Raisi wa Kamati ya Mkutano wa Nchi ambazo zimeridhia
Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (Vice President of the Conference of
State Parties to the Convention on the Rights of Persons of Disabilities)

No comments:

Post a Comment