Friday, April 15, 2016

JINSI YA KUJIAJIRI KATIKA UFUGAJI.

JINSI YA KUJIAJIRI KATIKA UFUGAJI.
Written by roryamaendeleo

JINSI YA KUJIAJIRI KATIKA UFUGAJI.
Wengi wetu tumekuwa tukilalmika kuwa ajira ni ngumu pindi tunapo maliza elimu zetu,na wengi wetu tumekuwa tukitegemea elimu tunayoipata iwe kigezo cha kupata ajira serikalini,jambo ambalo limekuwa potofu na hata kufikia hatua ya kujiingiza katika makundi ambayo si rafiki.lakini mbali na wengi wetu wenye kisomo cha kulidhisha,lakini pia kuna wengine ambao hawana elimu ya kutosha katika ngazi za kidato cha nne ,sita ,au chuo,lakini hali hii haitufanyi tukashindwa kujitafutia chanzo cha kujipatia kipato pasipokutegemea serikali kutuajiri.

Huu ni ugonjwa ambao tumekuwa tukiumwa kila siku tena unawaarhiri vijana wengi ambao wamekua wakidhani kazi nzuri ni serikalini.
Ili tuondokane na ugonjwa huu wa kutegemea kazi za serikalini hatuna budi sis wenyewe kubadilika na kuanza kupanga mikakati ambayo itaweza kutufanikisaha katika kujipatia kipato,aidha kwa hili litafanikiwa tu kama tutaweza kutumia mazingira tulionayo na elimu vizuri kujiingizi kipato.

Leo tutaangalia jinsi gani mtu anaweza kujiajiri katika ufugaji,inajulikana kwamba kunaaina nyingi za ufugaji,kuna ufugaji wa Ng’ombe,Mbuzi.Nguruwe,kuku,na bata hii yote ni aina ya ufugaji ambo umegawanyika katika kiwango cha mtaji wake,kwa mfano ili ufuge n’ombe unahitaji mtaji mkubwa alikadhalika na wanyama wengine tofauti na ufugaji wa viumbe hai aina ya ndege.

Bila kupoteza muda leo tutaangalia jinsi gani tunweza kujipatia kipato katika ufugaji wa kuku,ehee huyu huyu kuku ambaye tuna mnunua kwa shilingi 5000/600,lakini kumbe tunaweza pia hata sisi tukawafuga na kujitengenezea fedha hizo hizo ambazo tumekua tukitoa kwa watu wengine4 kununua kuku,ufugaji wa kuku huu ni kuku wa kienyeji ambao wameonekana mjini hawana soko kutokana na kuku wa kizungu (Broila) kuchukua soko kubwa.
Idadi ya kuku.
Ujasiriamlai huu auhitaji kiwango ama idadi ya kuku wengi ndiyo uweze kujiajiri katika ujasiliamli wa ufugaji wa kuku,kwani kwa kutambua kuwa kuku na wanyama wengine uzaliana,kwa hiyo unaweza kuanza na kuku wachache tu,ukapata kuku wengi kwa kufuata njia za kijasiriamali,kwa kuanza tuanzie na kuku 5 ambao wanaweza kutupatia kuku 200 kwa miezi 6 tu.

Anza na kuku majike(temba)watano wenye rika la umri mmoja au ambao wapo tayari katika kutetea na kupandwa na jogoo,temba hawa wameke katika banda moja ambalo litakuwa na jogoo mmoja ambaye ni wa mbegu,watunze katika mazingira mazuri na kuwapatia chakula kinachohitajika ili kiweze kujenga afya ya kuku huyo na kuweza kutaga mayai yenye ubora,chakula ambacho utatumia ni chakula kilichi na mchanganyiko kamili wa virutubisho na lishe kwa mwili wa kuku yaani wanga,protini,Chokaa,na Chumvichumvi,kwa kufanya hivi utakuwa umemjengea kuku afya iliyobora katika kukuletea mayai yaliyo na afya ambyo yatasabaisha kuengua watoto wenye afya pia.

Baada ya kuona wameanza kutaga mayai,na wameanza kuatamia,ni muda sasa umfika kwa wewe kuchagua mayai yapi yakuatamiwa,kwa kawaida unaweza usijue aina ya vifaranga wakiwa bado katika mayai,ili uweze kutambua,mayi madogo ni mayai yaliyo na vifaranga jike,huku mayai makubwa ni vifaranga dume(jogoo).
Kuku utaga mayai kufikia hata 26-30 kwa kila msimu unapofika wakutaga,chugua mayai 12 -15 na umuweke kila kuku mara baada ya kwajengea viota vya kuatamia mayai,viota hivi lazima view na usalama wa kutosha ambapo wanayama kama kenge,vicheche,na nyoka wasiweze kuleta usumbufu na kula mayai.
Kama kuku wanataga mayai 24 yagawe mara mbili,wamu ya kwanza wawekee mayai 12 ukisubiri kuenguliwa ,mengine ukiyahifadhi,baada ya kuenguliwa  vifaranga hivyo,hakikisha umewakea mazingira mazuri ya kuishi ikiwamo banda lenye joto la wastani wa 21c-33c kwa vifaranga vyenye umri wa kuanzia wiki 1-5.
Kuenguliwa vifaranga (5kuku x12mayai=60vifaranga),baada ya kuenguliwa kwa vifaranga vya kwanza,kwa kawaida kuku anapomaliza kuatamia mayai,asipoona watoto,ni rahisi kwa kuku huyo kuendelea kuatamia kwa siku 21 zingine,hivo kwa mayai yaliobaki 12 mengine muweke alalie tena kwa siku 21 mbele,kwahiyo katika wiki 6 kuku atakua amelalia marambili kwa msimu mmoja wa kutaga mayai,na hesabu ya vifaranga iatakua hivi.5x 12=(60)x2=120vifaranga,inamaana kwamba kwa wiki 6 utakua na vifaranga 120 kwa msimu mmoja.
Kuku anayeatamia mayai maranyingi unyonyoka manyoya hivyo unapomuwekea mayai mengine ayaatamie akikisha unampatia chakula chakutosha kama vile mchunga,mchicha na maji paoja na vyakula vya madini kama vile dagaa waliosagwa,kwa kufanya hivi utakua umewawezesha kuku kuishi katika hali ya afya bora na wataweza kuendelea kutaga mayai kwa wingi huku wewe ukipata faida ongezeko la kuku.
Angalizo..uleaji wa vifaranga si jukumu la kuku tena bali kulea ni jukumu la kwako,kumlea katika mazingira ya usafi wa banda ili kumuondolea hatari ya kushambuliwa na maginjwa,vijidudu kama utitili nk.
Aidha,mara baada ya kuenguliwa kwa mayai ya awamu ya pili,kuku wataweza kuka kwa wiki 2 au 3 na kuanza kutaga tena katika msimu pili wa kutaga mayai.
Jinsi ya kuwalea kuku na kupata masoko….itaendelea

No comments:

Post a Comment