Thursday, April 14, 2016

Lesoni

Apr
7
Somo la 3: Fundisho Mlimani
Somo limetafsiriwa na Mgune Masatu

(Mathayo 5)

Somo hili limetafsiriwa kutoka katika Copr. 2011, Bruce N. Cameron, J.D. Marejeo yote ya maandiko yametoka kwenye tafsiri ya New International Version (NIV), copr. 1973, 1978, 1984 International Bible Society, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo. Nukuu kutoka kwenye tafsiri ya Biblia ya NIV inatumika kwa ruhusa ya Wachapishaji wa Biblia wa Zondervan. Majibu yaliyopendekezwa yanapatikana kwenye parandesi (kwenye mabano). Somo limekaa kimtazamo kwamba mwalimu anatumia ubao au sehemu nyingine yoyote ambayo inaweza kuonekana na wanafunzi. Kama huwa una kawaida ya kupokea somo hili kwa njia ya barua pepe na hukulipata kwa juma moja, unaweza kulipata kwa kubofya kwenye www.lesoni.blogspot.com kwa lugha ya Kiswahili na http://www.GoBible.org kwa lugha ya Kiingereza pamoja na lugha nyingine kama vile Kifaransa, Kijerumani. Omba kwa ajili ya uongozi wa Roho Mtakatifu unapojifunza.

Utangulizi: Fundisho Mlimani ni wasilisho la kushangaza sana. Hata hivyo, kuna mitazamo tofauti kuhusiana na fundisho hilo. Wengine wanadhani kuwa ni “orodha ya kanuni” zitakazotumika tutakapokuwa mbinguni – na hivyo fundisho hilo halituhusu kwa sasa. Wengine wanadhani kuwa fundisho hilo limedhamiria kutufanya tuhitimishe kuwa haiwezekani kufikia viwango vya Mungu, na hivyo tunasukumwa kuitegemea neema. Wengine wanalichukulia fundisho hilo kama changamoto kwao ili kuboresha matendo yao ya haki kwa kiwango cha juu. Mtazamo wangu ni kwamba Fundisho Mlimani linatuonesha kwamba neema sio tu suala la wokovu, bali pia ni suala la mtindo wa maisha. Mungu anatupatia wito wa kutegemea uwezo wake katika mambo yote, na hiyo inajumuisha namna tunavyoishi. Hebu tuzame kwenye somo hili linalotafakarisha ili tujifunze zaidi!

No comments:

Post a Comment