Monday, July 11, 2016

Nyingine ya mwaka!! kuhusu waliokua wakifanya mapenzi chumba jirani na cha Mahakama kesi ikiendelea


Screen Shot 2014-05-22 at 11.26.43 AMKatika vituko vikubwa au vioja Mahakamani nilivyowahi kuvisikia kutoka Tanzania, vyote nilivipata kutoka 88.1 Mwanza pale ambapo Mahabusu mmoja alitumia njia ya kuvua nguo na kujipaka choo ili akitoroka mtu aogope kumshika lakini hakufanikiwa… pia kituko kingine ni cha May 2014 ambacho Mahabusu mmoja alivua nguo na kupaza sauti kwamba amesingiziwa kesi ya mauaji na anashikiliwa kwa kipindi kirefu.
Kituko kingine cha tatu leo kinatoka Italia ambapo Jaji mmoja ameamua kusimamisha kesi baada ya kuona wafanyakazi wawili wa Mahakama hiyo wakifanya mapenzi kwenye chumba cha jirani wakati kesi ikiendelea.
Jaji Anna Ivaldi alishtuka na kumuomba mwendesha mashtaka anyamaze baada ya kuona tukio hilo ndani ya ofisi pembeni ya mahakama ambapo wawili hao walidhani kioo kilichoua na tinted pembeni yao kisingeweza kumpa nafasi mtu wa upande wa pili kuona kinachoendelea ndani.
Taarifa kutoka kwenye Mahakama hiyo zinaamplfy kwamba mmoja kati ya wawili hao anatambulika kuwa yuko kwenye ndoa  na hii ni kwamujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Mahakama.
Screen Shot 2014-05-22 at 11.27.10 AMBaada ya hii ishu ilibidi tu Jaji aamuru kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka wakati mwingine muda mfupi tu baada ya wakili Sabrina Monteverde kuanza kuzungumzia kesi ya hiyo ya Mmorocco Yasin Mahmoud ambae anashtakiwa kuua jambazi katika bandari nchini Italy mwaka jana.
Mmoja kati ya waliokuwemo mahakamani amesema “wakili ndio kwanza alianza kuzungumza, jaji akasikia kelele za mahaba na alipoangalia juu na kuona miili miwili ikiwa uchi ilifanya kila mtu akatazama ambapo tuliona watu wawili wakifanya mapenzi na inaonesha walikua hawajui kama wanaonekana na wakati tunawatazama bado walikua wanaendeleza.
Kesi ilisimamishwa na wawili hao waliondoshwa eneo hilo na kupata mshtuko ambapo majina yao hayajatajwa huku mzungumzaji wa Genoa Court  akisema kesi imesimamishwa kwa muda na tukio hilo limeshashughulikiwa na haitakuwa sawa kuzungumzia zaidi
.

No comments:

Post a Comment