Monday, July 11, 2016

Samsung yafeli mtihani wa kuwa ndani ya maji


by rorya maendeleo
Image copyrightGETTY
Image captionSamsung yafeli mtihani wa kuwa ndani ya maji
Simu ya kisasa ya Samsung Galaxy S7 inayopigiwa upatu kuwa na uwezo wa kustahimili kuwa chini ya maji imefeli majaribio ya shirika la moja la kutathmini ubora wa bidhaa za kielektroniki.
Programu ya simu hiyo ya Samsung Active ilizima punde baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji.
Kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa bidhaa, Consumer Reports ilirejelea jaribio hilo kwa mara ya pili wakitumia simu tofauti na kama ile ya kwanza ikafeli.
Kampuni ya kutengeza simu hiyo ya Samsung ikijitetea imesema huenda simu hizo zilikuwa ni mbovu na hivyo kuruhusu maji kuingia ndani.
Image copyrightAP
Image captionSimu hizo za Samsung zilizima baada ya kutumbukizwa ndani ya maji
Simu hizo zilitumbukizwa ndani ya mapipa ya maji na kutolewa baada ya dakika.
Simu hizo za Samsung zilizima.
Kulikuwa hata na maji katika eneo la kamera za simu hizo mbali na viputo.
Image captionKampuni inayotengeza simu hizo kutoka Korea Kusini Samsung imejitetea vikali ikisema kuwa Galaxy S7 Active, inayouzwa Marekani imefanyiwa majaribio kabambe na hata kupewa cheti maalum cha IP68.
Kampuni inayotengeza simu hizo kutoka Korea Kusini Samsung imejitetea vikali ikisema kuwa Galaxy S7 Active, inayouzwa Marekani imefanyiwa majaribio kabambe na hata kupewa cheti maalum cha IP68.
Hati hiyo maalum inathibitisha kuwa simu hizo zinauwezo wa kustahimili kutumbukizwa ndani ya maji.
Consumer Reports iligonga vichwa vya habari kote duniani ilipotambua kuwa simu aina ya Iphone 4 ilikuwa na matatizo ya ya kifaa cha kuungia mbali.
''kwa kawaida tumekuwa tukiamini pale mtengezaji wa bidhaa akituambia kuwa bidhaa yake inaweza kustahimili hata kutumbukizwa ndani ya maji, lakini leo tulipojaribu kuhakiki madai ya Samsung tuligundua kuwa simu hizo zinazima baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji ''
''Bila shaka wale walionunua simu hizo kwa imani kuwa haitoharibika hata baada ya kutumbukizwa ndani ya maji, watalazimika kutafuta ridhaa kutoka kwa watengenezaji,,,''
Image captionConsumer Reports iligonga vichwa vya habari kote duniani ilipotambua kuwa simu aina ya Iphone 4 ilikuwa na matatizo ya ya kifaa cha kuungia mbali.
Simu hiyo ilianza kuuzwa mwezi juni mwaka huu.
Mwaka uliopita Sony, iliwaonya watumiaji wa bidhaa zake kuwa kulikuwa na uwezekano kuwa simu zake zitaharibika zikitumika ndani ya maji.
Samsung inatarajiwa kutangaza faida kubwa zaidi baada ya mauzo yaliyozidi matarajio ya simu hiyo aina ya Galaxy S7.

No comments:

Post a Comment