Monday, July 11, 2016

Ureno mabingwa wa Ulaya 2016



UrenoImage copyrightGETTY
Image captionNi mara ya kwanza kwa Ureno kushinda Euro
Ureno wameshinda michuano ya kandanda ya Ulaya, Euro 2016, kwa kuwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika dakika za ziada kwenye mchezo wa fainali mjini Paris.
Goli la ushindi lilifungwa na Eder katika dakika ya 110, na kusababisha huzuni kubwa kwa mashabiki wa Ufaransa waliofurika kwenye uwanja wa Stade de France.
Image copyrightGETTY
Ilikuwa furaha kubwa kwa mashabiki wa Ureno. Hii ni mara ya kwanza Ureno kushinda michuano mikubwa.
Ureno walicheza kwa kujituma na ushirikiano bila ya mchezaji wao nyota Cristiano Ronaldo aliyetoka kutokana na kupata jeraha la goti katika kipindi cha kwanza.
EderImage copyrightGETTY
Image captionEder asherehekea na wenzake baada ya kufunga
Ufaransa ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa, lakini hawakuweza kuzitumia vyema nafasi walizopata.

No comments:

Post a Comment