Monday, July 11, 2016

Theresa May kuwa waziri mkuu wa Uingereza



Image copyrightGETTY IMAGES
Image captionTheresa May kutangazwa waziri mkuu wa Uingereza
Katika saa au siku kadhaa zijazo, Waziri wa maswala ya ndani wa Uingereza, Theresa May, atatangazwa kinara mpya wa chama cha Conservative, na waziri mkuu mpya wa Uingereza.
Hii ni baada ya mpinzani wake mkuu katika kinyanganyiro ya kuwania kiti cha uaziri mkuu mbunge Andrea Leadsom, kujiondoa.
Andrea Leadsom ameamua kumuunga mkono mpinzani wake, Theresa May kuwania kiti hicho, huku akisema kuwa anatakiwa kutimiza uungwaji wake mkono wa kujiondoa kwa Uingereza kutoka muungano wa jumuia ya mataifa ya EU na kutoa fursa kupatikana kwa haraka kwa waziri mkuu mpya.
Image copyrightAP
Image captionMay atachukua pahala pake David Cameron aliyejiuzulu baada ya kushindwa katika kura ya maoni
Wakuu wa chama cha Conservative kwa sasa wanajadiliana ili kumuidhinisha Bi May, kuchukua nafasi hiyo na kuwa waziri mkuu wa pili wa kike nchini Uingereza baada ya Bi Margaret Thatcher.
Wakati huo huo, Mbunge Angela Eagle ametangaza rasmi nia ya kumn'goa Jeremy Corbyn kama kinara mkuu wa chama cha Leba.

No comments:

Post a Comment