Friday, June 10, 2016

BODI YA PBPA YAZINDULIWA RASMI.

BODI YA PBPA YAZINDULIWA RASMI.

 BP2Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Nishati,Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo wapili kushoto, akimkabidhi vitendea kazi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja ( PBPA) Dkt. Steve Mdachi( wa pili kulia) wanao shuhudia ni mjumbe wa bodi hiyo Salum Mnuna( kulia) na Mkurugenzi wa PBPA Michael Mjinja( kulia)
BP3Wajumbe wa Bodi ya PBPA pamoja na watendaji wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( katikati) mara baada ya kuzindua rasmi bodi hiyo.
BP1Baadhi ya wafanyakazi wa PBPA wakifuatilia uzinduzi wa bodi yao katika ukumbi wa mikutano wa Wakala huyo jijini Dar es salaam hivi karibuni.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Zuena Msuya, Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo amezindua Bodi ya Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja  nchini (PBPA).
Akizungumza mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jijini Dar es salaam, Dkt Pallangyo alisema kuwa PBPA inapaswa kufanya kazi kama ilivyoelekezwa ili kuleta ufanisi kwa taifa.
Alisema kuwa Bodi hiyo imeaminiwa na ndiyo maana imepewa dhamana ya kusimamia Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja nchini, hivyo ni vyema kuthibitisha uaminifu huo kwa kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa.
Wakala huo ulianzishwa rasmi mwaka 2015 kwa lengo la kusimamia usalama wa mafuta ya Petroli, Diseli, Mafuta ya ndege JET na Mafuta ya taa; Pia, kuhakikisha uwepo wa mafuta nchini wakati wote na kuhakikisha kuwa wale wote walioagiza mafuta wanapata  malipo stahiki na kwa wakati.
Aidha Dkt Pallangyo alisema kuwa bodi hiyo inapaswa kumshauri Waziri wa Nishati na Madini juu ya muundo mzima la uagizaji mafuta kwa pamoja ili kuongeza ufanisi wa huduma hiyo.
Majukumu menhine ni kusimamia mapato na matumizi ya wakala huyo, ajira, usalama kazini na miongozo yote inayohusu PBPA.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi husika Dkt. Steve Mdachi aliahidi kuwa hawataingusha Serikali na pia watatimiza kile kilichokusudiwa ili kuleta tija na ufanisi kwa taifa.
Dkt. Mdachi alisema kuwa kazi yao ya kwanza ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa PBPA wanakuwa katika mazingira mazuri na bora ya kazi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.
Bodi ya PBPA imeteuliwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni na itaongozwa na wajumbe watano akiwemo Mwenyekiti pamoja na wajumbe wanne.

No comments:

Post a Comment