Saturday, June 11, 2016

Mtihani wa Marekani wafutwa Korea Kusini na Hong Kong



Image copyrightAFP
Image captionChuo kikuu cha California nchini Marekani
Mtihani unaowapa nafasi wanafunzi wa kigeni kuingia katika vyuo vikuu vya Marekani umefutwa nchini Korea Kusini na Hongkong baada ya vifaa vya mtihani huo kuibwa.
Mtihani huo umefutwa saa chache tu kabla ya wanafunzi zaidi ya 5000 kutahiniwa.
Mtihani huo, unaotolewa na shirika la Marekani la ACT unatumiwa na vyuo vikuu vya Marekani kutathmini wanafunzi wa kimataifa.
Kila mwaka, maelfu ya wanafunzi huwa wanaomba nafasi ya kusomea vyuo vikuu vya Marekani.

No comments:

Post a Comment