Saturday, June 11, 2016

BOT IMETOA SH. MILIONI 273 KUCHANGIA UNUNUZI WA MADAWATI NCHINI.......

BOT IMETOA SH. MILIONI 273 KUCHANGIA UNUNUZI WA MADAWATI NCHINI.......

BO1Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  Majaliwa akiongea na wafanyakazi  wa  Benki  Kuu (BoT)  (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha matembezi  ya  hisani  ya  wafanyakazi  hao kutoka  makao  makuu  ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam yaliyokuwa na lengo la kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50  ya Benki.
BO2Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) kuongea na wafanyakazi wa BoT leo jijini Dar es salaam.
BO3Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiongea kwa niaba ya Wakuu wa mikoa ambao mikoa yao ina matawi ya Benki Kuu nchini mara baada ya kuhitimishwa kwa matembezi ya hisani  ya  wafanyakazi  BoT yaliyoanzaia kutoka  makao  makuu  ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam, matembezi hayo  yalikuwa na lengo la kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50  ya Benki.
BO4Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu (kushoto) akimkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) mfano wa hundi ya Sh. 273,089,338 leo jijini Dar es salaam kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuchangia ununuzi wa madawati.
BO5Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akionesha mfano wa hundi ya Sh. 273,089,338 aliyokabidhiwa na Benki Kuu leo jijini Dar es salaam ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuchangia ununuzi wa madawati.
BO6Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda (kulia) akimpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) mara baada ya kuongea na wafanyakazi  wa  Benki  Kuu (BoT) (hawapo pichani) baada ya kuhitimisha matembezi  ya  hisani  ya  wafanyakazi  hao leo jijini Dar es salaam.
BO7Baadhi ya wafanyakazi wa  Benki  Kuu (BoT) wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (hayupo pichani) mara baada ya kuhitimisha matembezi  ya  hisani  ya  wafanyakazi  hao kutoka  makao  makuu  ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam yaliyokuwa na lengo la kuchangia ununuzi wa madawati ya shule za msingi na sekondari kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50  ya Benki.
BO8BO9Mmoja wa Wafanyakzi wa Benki Kuu ya Tanzania Gloria Mahina akicheza kufurahia wimbo ulioimbwa na kwaya ya muungano wa wafanyakazi wa BoT kutoka matawi yote nchini ikijumuisha mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Dodoma na Mtwara.
BO10Kwaya ya muungano wa wafanyakazi wa BoT kutoka matawi yote nchini ikijumuisha mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar, Dodoma na Mtwara ikitumbiza baada ya kuhitimisha matembezi  ya  hisani  ya  wafanyakazi  hao kutoka  makao  makuu  ya Benki hadi viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam
BO13Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa  Benki kuu ya Tanzania leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
……………………………………………………………………………………
Hussein Makame-MAELEZO
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) na wafanyakazi wake wa matawi yote nchini kwa kushirikana na baadhi ya Taasisi za kifedha na kampuni za simu nchini, imetoa Shilingi Milioni 273 kuchangia ununuzi wa madawati ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki hiyo.
Fedha hizo zilikabidhiwa leo kupitia hundi ya mfano kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya matembezi ya hisani yaliyolenga kuchangia madawati, yaliyoanzia Ofisi za BOT hadi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kabla ya kukabidhi fedha hizo, Gavana wa BOT Prof. Benno Ndulu alisema lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuongeza ubora wa elimu kupitia upatikanaji wa madawati kwa shule za msingi na sekondari nchini.
“Tunatambua kwamba changamoto hiyo (uhaba wa madawati) ni kubwa, lakini tunaamini mchango wetu utasaidia kupunguza makali ya tatizo hilo na kuongeza idadi ya watoto wetu ambao wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati” alisema Gavana Prof. Ndulu
Akifafanua mchango huo, Gavana Prof. Ndulu alisema kati ya fedha hizo, BOT imetoa Shilingi Milioni 167, Wafanyakazi Milioni 29.8, Taasisi za Kifedha Milioni 22 na kampuni za simu Milioni 54.3 na kwamba madawati hayo yatasambazwa kwenye shule zenye upungufu au ukosefu wa madawati za Dar es Salaam na zilizoko mikoa ambayo Benki hiyo ina matawi yake.
Alitaja mikoa hiyo na fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa BOT wa matawi ya mikoa hiyo kuwa ni Makao Makuu Dar es Salaam waliochangia Shilingi Milioni 22, Mwanza (Milioni 1.24), Chuo cha Benki Mwanza (680,000) Arusha (Milioni 1.23) Mbeya (Milioni 1.186), Mtwara (850,000) na Dodoma (Milioni 1.18).
Alisema taasisi zilizochangia fedha hizo ni Benki ya India Shilingi Milioni 5, Benki ya Habib (Milioni 5), Benki ya Exim (Milioni 5), Benki ya UBA (United Bank for Africa, Milioni 2), Tanzania Mortgage Refinance (Milioni 2), China Community Bank (Milioni 2) na NIC Bank aliyotoa Milioni 1.
Kwa upande wa kampuni za simu zilizotoa fedha ni kampuni ya Vodacom iliyotoa Dola za Kimarekani 10,000, kampuni ya Tigo Dola za Kimarekani 10,000 na kampuni ya Selcom iliyotoa Dola za Kimarekani 5,000.
Akizungumza baada ya kupokea hundi ya mfano, Waziri Mkuu Majaliwa alisisitiza fedha hizo zitumike kama zilivyokusudiwa na yeyote atakayetumia fedha hizo kinyume na malengo achukuliwe hatua mara moja.
Katika kuthamini sekta ya elimu nchini, Gavana Prof. Ndulu alisema benki hiyo ilianzisha Mfuko wa Udhamini wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo hadi sasa umetoa ufadhili kwa wanafunzi 22 kusoma shahada za kwanza na za uzamivu katika vyuo vikuu hapa nchini katika masomo ya sayansi, hisabati, uchumi, fedha, uhasibu na TEHAMA.
“Lengo kubwa la mfuko huu ni kuhamasisha wanafunzi wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati yakiwemo masomo kuhusu gesi na mafuta.Katika idadi hiyo, 16 ni wanafunzi wa kike na waliobaki 8 ni wanaume” alisema Gavana Prof. Ndulu.
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ilianza kutoa huduma kwa wananchi mnamo tarehe 14 Juni mwaka 1966 na Juni 14 mwaka huu inatimiza Miaka 50 na katika kuadhimisha miaka hiyo wafanyakaz wa matawi yote nchini wanafanya matembezi hayo ili kutoa mchango kwa jamii.

No comments:

Post a Comment