Sunday, June 5, 2016

Ukawa wadai miradi ya maji bungeni

Ukawa wadai miradi ya maji bungeni

HAMIDU Hassan Bobali, Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni Wizara ya Maji ameitaka serikali itoe tathmini ya mradi wa kuvipatia maji vijiji 10 uliotekelezwa mwaka wa fedha wa 2015/2016, anaandika Wolfram Mwalongo.


Bobali amesema mradi huo ulitekelezwa pasipo kufanyika kwa upembuzi yakinifu kwenye maeneo yaliyo paswa kuchimbwa kwa visima hivyo.

Aidha amesema, visima vingi vilijengwa na tasisi za Dini ya Kiislamu na Kikristo na fedha hizo zikiingia mfukoni mwa watendaji wachache huku halmashauri zikidai kutekeleza mradi huo.

Hata hivyo katika kitabu cha mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2016/17 kuhusu miradi ya Maji Vijijini inaonesha kuwa, imejengwa miradi mipya ya maji 975 katika vijiji 1,206 kwenye vituo 24,129 katika Halmashauri 148.

Kambi ya Upinzani Rasmi Bungeni imeitaka serikali takwimu zikaeleza kwa uwazi kwa kila Halmashauri, kata gani, kijiji gani kati ya hivyo vijiji 1,206 na vituo 24,129 vipo katika kitongoji kipi, kwa mtiririko huo ni dhahiri hata maswali kwa Serikali yatapungua au udanganyifu unaofanyika utapungua kama sio kumalizika kabisa.

Waitara aiangukia serikali

Mwita Waitara, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, imeitaka serikali kuhakikisha inaweka huduma ya vituo vya polisi katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na matukio ya uhalifu yaliyoshamiri, anaandika Pendo Omary.


Akizungumza na MwanaHALISI Online jana Jijini Dar es Salaam, Waitara amesema “ jimbo zima la Ukonga hakuna kituo kikubwa cha polisi hata kimoja. Kwa sasa tunatumia kituo cha Stakishari kilichopo jimbo la Segerea. Hata vituo vidogo vilivyopo vinafugwa saa 12:00 jioni”.

Waitara amesema kituo cha Stakishari ambacho wanakitumia kwa sasa, uwezo wake wa kuhudumia majimbo mawili ni mdogo. Hasa kutokana na kutokuwa na usafiri wa uhakika pindi askari wa kituo hicho wanapohitajika kutoa huduma katika majimbo hayo.

“Askari wa Kituo cha Stakishari wanalazimika kutumia gari ya OCD. Inapotokea OCD kaondoka na gari, basi huduma ya polisi inayotumia gariinakosekana,” amesema Waitara.

Aidha, Waitara amelitaja tukio la Disema, mwaka jana la uvamizi, uporaji wa fedha na mauaji ya askari wawili kwenye Benki ya CRDB Tawi la Chanika kama moja ya matukio ya kiharijfu yanayochangiwa na kutokuwepo vituo vya polisi katika jimbo hilo.

“Mara baada ya kupata nafisi ya kuongoza jimbo hili tayari nimeshirikiana na wananchi. Tumeanza mchakato wa ujenzi wa vituo vikubwa vya polisi vitatu ambavyo vitakuwa kata za; Kivule, Msongora na kata ya Zingiziwa. Tunaiomba serikali na Jeshi la Polisi ituonge mkuno katika kutatua tatizo hili.” amesema Waitara.

No comments:

Post a Comment