Thursday, June 9, 2016

NAMNA YA KUPATA MTOTO WA KIUME

NAMNA YA KUPATA MTOTO WA KIUME


son

Kupata mtoto wa kiume ni jambo linalohitaji ushirikiano wa pande zote mbili, yaani mke na mume na ni jambo linalohitaji hatua kwa hatua na kwa umakini, ingawa njia nitakayoeleza hapa haimaanishi kuwa inaweza kufanya kazi kwa asilimia 100.  Bali ni njia ambayo imekuwa ikitumika mara kwa mara na ndiyo njia rahisi na ukiifuata unaweza ukapata kwa asilimia 75.

Mwaka 1960 mwanasayansi Landrum Shettles aliandika kitabu kinachohusu uchaguzi wa jinsi ya mtoto.  Mwanasayansi huyo wa tiba ndiye aliyeileta nadharia yake iliyojikita zaidi katika vitu vilivyomo ndani ya seli, yaani malighafi za kijenetiki ziitwazo chromosomes ambayo ndiyo inayotumika na kama ikifuatwa vizuri basi huweza kuwa na mafanikio.

Sayansi ya kijenetiki inaeleza kuwa mwanamke huwa na mbegu ya XX na ya kiume huwa na XY, na pale yai la kike linaporutubishwa hutokea mgawanyiko wa seli na mbadilishano wa malighafi za kijenetiki hutokea.

Hivyo kiumbe kinachotungwa yaani mtoto, huwa na nusu ya malighafi za kijenetiki kutoka kwa mama na nusu nyingine kutoka kwa baba, na akipata mbegu XX huwa ni jinsi ya kike na akipata XY ni wa kiume.
Kiasilia mbegu Y huwa ni ndogo kimaumbo, zina mwendokasi mkubwa lakini hufa mapema ukilinganisha na za kike X ni kubwa, hazina kasi, lakini huishi kwa muda mrefu.  Kwa kutumia ufahamu huu ndipo mwanasayansi Shettels aliweka nadharia ambazo zinatumika katika uchaguzi wa jinsia.

Kuna hatua tano za kufuata kwa umakini ili uweze kufanikiwa, ingawa haimaanishi kuwa ni lazima ufanikiwe kwani hatua hizi huongeza nafasi zaidi ya kupata jinsi ya kiume na kwa yule atakayehitaji jinsi ya kike afanye kinyume cha hatua hizi.

Hatua ya kwanza
Hatua ya kwanza ni kugundua wakati wa ovulation, ama siku ambayo yai la kike linatoka.  Hiki ni kipindi ambacho yai la mwanamke lipo tayari kurutubishwa na mbegu ya kiume hivyo mimba huweza kutungishwa.

Ili kugundua kuwa upo katika ovulation, inabidi kufuatilia yafuatayo: Inabidi uwe na chati ya kuangalia na kufuatilia ute wa kizazi unaotoka ukeni, maana muda mfupi kabla ya ovulation ute huwa wa majimaji na wa kuvutika hufanana kama vile wa mayai ya kawaida, nikimaanisha ya kuku, ambayo yamezoeleka kwa wengi.

Ni vizuri kupanga chati hii kwa zaidi ya miezi mitatu ili kusudi uwe na uzoefu wa kugundua tofauti ya ute.  Vilevile inabidi uwe na chati ya kuweka rekodi ya joto la chini la mwili wakati ukiwa umepumzika, nikiwa na maana mara nyingi ukiwa umelala.

Joto la chini la mwili hupanda kwa nyuzi joto 0.5 sentigredi kipindi cha ovulation.  Ni vizuri chati hii iwe pamoja na ya ute wa kizazi, kusudi uweze kufuatilia mabadiliko haya kwa pamoja.

Kipimo cha kugundua ovulation ni kipimo ambacho huangalia wingi wa homoni aina ya Lutenizing ambayo hutolewa kwa wingi kipindi hiki.  Kipimo hiki ni vizuri kufanya mara mbili kwa siku, kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 9:00 mchana.  Vilevile kati ya saa 11:00 jioni na saa 4:00 usiku.

Hatua ya pili
Hii ni hatua ya kutegea wakati muafaka wa kufanya tendo la ndoa.  Ni vizuri kufanya tendo la ndoa kipindi cha saa 24 kabla ya ovulation na saa 12 baada ya ovulation.  Kwa sababu tindikali na utelezi katika ute wa kizazi hupungua na hivyo husaidia mbegu za mwanaume hasa aina ya Y kusafiri haraka na kulifikia yai la mwanamke na kulirutubisha.

Hatua ya tatu
Pendelea mtindo au staili inayofanywa na wanyama kama mbuzi wakati wa tendo la ndoa, yaani mtindo wa mwenza wako kuinama.
Mtindo huu huwezesha mlango wa uzazi kuwa karibu na sehemu ya kiume pia kuingia umbali mrefu zaidi ndani ya uke, hivyo basi mbegu za kiume humwagwa karibu na shingo ya kizazi na kulifikia yai haraka zaidi.

Hatua ya nne
Ni muhimu mwanamke kufika kileleni kabla ya mwanaume; kufika kileleni kwa mwanamke husaidia kubadili mazingira katika uke kuwa ya ukakasi (alkaline) hivyo kusaidia mbegu za kiume “Y” kuwa imara zaidi.  Uke kuwa na tindikali huipunguza uimara wa mbegu ya kiume.

Hatua ya tano
Hii ni kwa upande wa mwanaume.  Ni vizuri kuvaa nguo zisizoweka joto kali na kubana.  Unapaswa kuvaa chupi au nguo ambazo hupwaya na zimetengenezwa kwa pamba.  Nguo za ndani zinazobana ambazo huongeza joto hupunguza idadi ya mbegu za kiume.  Joto pia hupunguza ubora na utengenezaji wa mbegu za kiume.

Vilevile inabidi kunywa vinywaji vyenye caffeine kabla ya tendo la ndoa.  Hii huongeza nguvu ya mbegu za kiume aina Y.

Mambo mengine ya kuzingatia ni mlo.  Hakikisha unakula vizuri wiki moja kabla na siku ya tendo.  Tafiti zinaonyesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye sukari huiwezesha mbegu ya Y kuimarika zaidi na kuongeza nafasi ya kupata mtoto wa kiume.  Vyakula hivi ni kama matunda matamu, vyakula vya wanga na vinywaji vyenye glukosi.

Vyakula vingine ni kama vile nyama nyekundu, mayai, maziwa, vyakula vya baharini kama vile samaki, kamba na pweza.

Kwa upande wa mwanamke, anapaswa kula zaidi vyakula visivyo na tindikali kama vile kuepuka kula matunda yenye uchachu na vyakula jamii ya kunde kupitia kiasi.

Mambo mengine ni kuzingatia mazingira ya tendo lenyewe, hakikisha upo vizuri kiafya, kimwili na kiakili.  Usiwe na msongo wa mawazo na sonona kwa sababu huleta mwingiliano na tendo, hivyo kulifanya kuwa dhaifu.

Ni vyema pia kutafuta mazingira mazuri ya kufanyika kwa tendo lenyewe.  Lengo ni kuwa na utulivu wa kimwili na kiakili pia.  Hii itakuepusha pia na usumbufu utakaoweza kuleta mwingiliano na tendo lenyewe.

No comments:

Post a Comment