Bunge la Rwanda laidhinisha muhula wa 3
- Saa 6 zilizopita
Wabunge
nchini Rwanda wamepitisha mswada utakaoidhinisha kubadilishwa kwa
vipengee vya katiba vitakavyoruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa
muhula wa tatu.
Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita
mamilioni ya raia nchini Rwanda wamekuwa wakitia sahihi pendekezo la
kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya
kukamilika kwa muhula wake wa pili.Kupitishwa kwa mswada huo sasa kunatoa fursa ya kufanyika kwa kura ya maoni ya iwapo ni haki kuruhusu uongozi wa zaidi ya mihula miwili au la.
Rais Kagame mwenyewe amesema kuwa huo utakuwa ni uamuzi wa raia wa nchi hiyo wenyewe.
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu wanasema kuwa utawala wa Rwanda unakandamiza uhuru wa kujieleza na hivyo kunyamazisha vyombo vya habari na upinzani.
Iwapo kura hiyo ya maoni itafaulu basi sheria itakuwa imefungua mlango kwa rais Paul Kagame kuwania hatamu ya tatu mwaka wa 2017.
Rais Kagame alichaguliwa kwanza katika mwaka wa 2003.
No comments:
Post a Comment