![DIAMOND](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tFeIrWbzI7b0SNgMu49kREW9_9PUn0Bk3sVeRl1mILTusUjHyMLl3TqfgOjckH_LeUgKkJNLW3U7F7T8h2kDJVk206IoCVChQ3kXQ9B-bkk7QelskgWG0Cs9xREAn6dCISb6EIvnT51P-R328Jav8ThzdSCbA5Fw=s0-d)
Imekuwa
story ambayo kiukweli kwa mtu anayefuatilia muziki haitaji hata
kusimuliwa kilichokuwa kinaendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja kati ya
Davido na
Diamond Platnumz ambao ilidaiwa kwamba wameingia kwenye beef au kutoelewana.
![bl](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tgZaWZKzVuPNNoql-Fgx8NwveITWG7eCHAywhnv5ziwwwaZAiXEkVFuKmxDMF1jevj9GPcjEk7XLZdPOLO-jJ7Kb3CicFowmU6UtBUUXpNIXX6alJonAjzgGNmniUgzpivBmAWZYiOBFKg44tQ5Ju-cPZN=s0-d)
Ukaribu wa mastaa hao wawili ulizaliwa baada ya collabo ya
My Number One Remix,
baadae mambo yakageuka, kukawa na kama uhusiano mbaya na kila kitu
kilikuwa kikibebwa na story za mitandaoni hasa Facebook na Instagram,
mashabiki kwa upande mwingine huenda ndio waliohusika pia kuifanya ishu
kuwa kubwa zaidi.
Davido aliwahi kupost picha ya Bendera ya TZ alafu akaweka alama ya love.. leo Meneja wa
Diamond Platnumz, Hamis Taletale aka
Babu Tale amepost picha inayowaonesha wakiwa pamoja,
Diamond,
Davido, na Mameneja wa
Daimond,
Salam na
Babu Tale mwenyewe.
Pia Davido alipost picha akiwa na mastaa
wengine pamoja na Diamond Platnumz kama inavyoonekana hapa chini na
kuandika with my ni*** na akamention Diamond kwenye Instagram.
![Davido Diamond Yemi Alade Pantoraking](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_uGJ1kR0EmKY8lPOLQFEw803NEKP9V6i6zWaS4oVriPfFA5hKbb-wEVA2ioIcAN320HBNgEPT-10jOvJwFzUK34Fpw-kwn6pZCzX4dWwF6v0FCLbv9gDb4sBJE8XhVUy-i3X0eyMV4Kdyh-aeE8wbAK1mJEDNYDZ04q8S5gpV475nk78BdWHnhSGk5mSbDt7zAeBo7-7w=s0-d)
Yemi Alade, Ricardo, Diamond, Davido na Pantoraking.
No comments:
Post a Comment